ras jeff kapita
JF-Expert Member
- Jan 4, 2015
- 22,152
- 33,899
Wtz wanapenda sana rushwa kuliko mishahara yao ya halaliMtanzania hawezi kuishi bila rushwa
Ova
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wtz wanapenda sana rushwa kuliko mishahara yao ya halaliMtanzania hawezi kuishi bila rushwa
Ova
Nyie si mko vijijii kuna mashamba limeni
Kama hujaridhika na maslahi ni heri uache tu kibarua kuliko kuibawewe mwenyewe si unaona
Bora hata hao wameongeza wanawake,mi huba ndo sielewi mwelekeo wake kila siku watu wanaanzisha mapenzi hovyohovyo sijui maudhui yake ni yapi yaani hata direction haieleweki kila siku watu wanapendanaMpali ilikuwa ya moto pale mwanzoni bwana.
Alipozidi kuongeza wanawake hadi wazungu ikapoteza ladha.
Watu wanachukulia poa..Watu hawajui tu, hayo maigizo yamewashika watu sana.
Mimi nilikuwa nayadharau hadi nilipochangamana na watu ndio nikajua.
Hakuna mshahara usiotosha ukijiwekea mipango na utaratibu mzuri, ila dhahama ni ile ile more money more problemsmshahara hautoshi...
Pole endelea nayo tena inanoga mbona mi kila ikiisha natamani kujua nini kiliendelea,kiukweli naielewa sanaMimi niliiachia njiani, sawa.
Hukosi huduma kakwambia nani? Unapotezewa tu utahangaika kwenye korido za NSSF mpaka ukomeUkikosa hiyo laki 3 hukosi huduma na unastahili
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Kama mshahara wa mkurugenzi dstv hautoshi sisi waalimu wa daraja la iii B vijijini tusemeje
Tz taifa la hongo!This is exclusive!
Mkurugenzi wa vipindi wa kitengo cha tamthilia za kiswahili zinazoruka kupitia kisimbuzi cha DSTV mwanamama Mtanzania Barbara Kambogi sambamba na msaidizi wake bwana Onesmus Ndarite yeye akiwa ni Mkenya wamesimamishwa kazi kwa tuhuma nzito za rushwa.
Mwanamama huyo na msaidizi wake walijijengea mfumo wao mahususi wa kuwezesha kuruka kwa sinema hizo za Kiswahili ndani ya kitengo hicho.
Mfumo huo ukiwa ni upigaji kwa pande zote, kwa madairekta kutakiwa kutoa hongo tamthilia zao zipate nafasi ndani ya DSTV, na huku haohao madairekta watakachopokea kutoka DSTV walitakiwa kugawana fungu na Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.
Hali hiyo ilidumu kwa kipindi kirefu, ikapelekea hadi wakawa sehemu ndani ya tamthilia za Jua Kali pamoja na Huba.
Ndio maana tamthilia hizo zinaikaribia Isidingo kwa ukaribu kwa mlolongo wa vipindi vyake visivyoisha!
Wazalishaji wa tamthilia hizo maarufu wanaofahamika ni mwanamama aliyejizolea sifa kubwa Leah Mwendamseke (Lamata) na Aziz Mohamed, ila nyuma ya pazia walikuwepo Mkurugenzi na msaidizi wake.
Ubadhirifu huo wa madaraka katika kitengo hicho uliingia sura mpya baada ya ingizo jipya la tamthilia ya Chanda.
Mkurugenzi kama ilivyo ada alitaka fungu liwekwe kama ulivyo utaratibu, mtayarishaji wa tamthilia hiyo bwana Isike Samweli alikataa kutoa ‘ushirikiano’
Ndipo balaa lilipozuka!
Mtayarishaji huyo (Isike Samweli) hapo awali alitayarisha tamthilia ya Pazia, na alitoa ushirikiano hadi alipokataa kwenye tamthilia yake mpya ya Chanda.
Alipokataa akaundiwa zengwe la kukatishwa kwa tamthilia yake hiyo ambayo bado ilikuwa inaendelea…
Bwana Isike hakukubalina na hilo, na kwa kuwa walikuwa na ‘ushirikiano’ hapo awali kwenye tamthilia ya Pazia alitunza ushahidi wote wa ushirikiano aliowahi kuwapa Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.
Bwana Isike alienda mbali zaidi kwa kumwaga ugali baada ya Mkurugenzi kutishia kumwaga mboga yake.
Alituma email kwenda makao makuu Afrika ya Kusini akiambatanisha na ushahidi wote wa miamala ya ‘ushirikiano’ aliowahi kuutoa.
Baada ya tuhuma hizo nzito zenye ushahidi kufika makao makuu, ndipo Mkurugenzi huyo na msaidizi wake waliposimamishwa kazi kwa haraka kupisha utaratibu mwingine kufanyika wa kushuhulikia hilo.
Pichani ni mwanamama Barbara Kambogi, na mtayarishaji aliyeundiwa zengwe bwana Isike Samweli.
Nikiripoti kutokea hapa JF kupitia chanzo changu makini,
Nifah.
View attachment 2825510View attachment 2825511
Mtafanya na sisi Wazee tuhamie mitaa ya Watu maarufu(Celebrates forum) ili kuja kusoma huo Ubuyu.Nimeshapoa.
Huo ubuyu wa moto ni next weekend, wala usijali kabati langu halikaukiwi ubuyu.
Tutakuwa na holidays nzuri, tuombe uzima na kukiombea chanzo changu pia.
Nimemshangaa sana huyo member kwa kuihusishanisha tabia ya wizi na uanaume, huyo inaonekana ni mtu aliyelelewa kwa kuaminishwa kwamba wanawake siku zote ni innocent na waaminifu na hawana kabisa kasumba za udokozi wala ujambazi, na ndio maana ameonesha kushangazwa na hii habari.Wizi ni tabia za kiume?. Mbona siku hizi kuna wamama wezi wengi tu.
Kupiga pesa mimi huwa napiga in situations ambapo naempiga anakuwa hafahamu chochote.
Ila ile kutengeneza mazingira kwamba mpigwaji ajue kabisa kwamba nampiga ishu za hivyo huwa sifanyi. Zile style kama za kiafande kwamba niungie tukamilishe jambo hizo huwa sifanyagi.
Ila unataka mzigo flani na najua unapopatikana hapo lazma nikuongezee sifuri mbele kisha ukituma hela najilipa juu kwa juu.[/color=red] Au kwenye supplies ya bidhaa huwa tunafanya sana michezo sisi watu wa sales.
Mbongo anakwambia pesa ni pesa haijalishi umeipata vipi maana hakuna sehemu utakayoenda kuitumia wataikataa kisa umeipata kwa njia isiyokuwa ya halali.Kupiga pesa isivyo halali kwa namna yeyote ile ni kubaya.
Kumbe Isike nae sio msafi kihivyo? Ila hayo ni maisha binafsi…Bwana isike pesa za tamthilia zilimzidi,akawapangia nyumba machoko sinza,aliona wanawake hawafai,ukipeleka tamthilia hapo,wahuni wanakwambia tutakupa 8m kwa episode,Ila utabaki na sita,mbili zao
Nipe dili ustaadhatHuyo Mtanzania na Mkenya wizi na ufisadi upo ndani ya dna zao.
Sababu zinajulikana.
Nafikiri sababu umeijua leo sasa, huenda baada ya hili sakata hizo tamthilia zitaisha.Bora hata hao wameongeza wanawake,mi huba ndo sielewi mwelekeo wake kila siku watu wanaanzisha mapenzi hovyohovyo sijui maudhui yake ni yapi yaani hata direction haieleweki kila siku watu wanapendana
Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
Ngoja nijaribu kuifuatilia tena, kwakuwa nilianza kuiona tokea mwanzo haitonipa shida.Pole endelea nayo tena inanoga mbona mi kila ikiisha natamani kujua nini kiliendelea,kiukweli naielewa sana
Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
Shaka ondoa, pele limepata mkunaji.Mtafanya na sisi Wazee tuhamie mitaa ya Watu maarufu(Celebrates forum) ili kuja kusoma huo Ubuyu.
Fanya hivyo ili kumuenzi mdau pamoja na kulipa uhai Jukwaa la Macelebrates maana tangu atutoke Warumi Jukwaa bado halijapata mrithi wake japo baadhi wanajaribu lakini inaonekana viatu vyake vimekosa mtu sahihi.