Kumekucha DSTV, Mkurugenzi wa vipindi Maisha Magic Bongo na msaidizi wake wasimamishwa kwa rushwa!

Hata hizo huba,jua Kali unaona ni ndani,sijui hawawezi andika story za nje!!
😂😂😂😂😂
Wanapenda sana mteremko.


Juzikati bekitatu wetu anapambana kuangalia sijui mchezo gani huko Azam.
Nikamwambia sasa mchezo kama huo,watu wanashinda ndani..fungua chupa za chai ,wanakula
Mara wamelala
Wanafua..mbona hata wewe unaweza kucheza.

Kiukweli mm napenda michezo ya ngumi
Wafumuane ngumi za uhakika ndio naona kweli hapa muigizaji ameitolea jasho Sanaa yake.
 
Movie ukiwa begginer kubali kutumika,utakula ukikua,usitegemee kulipwa wakati unaanza
 
Mpaka upatikane ushahidi usio na shaka kama wa Isike, habari za kusikia tu hazina mashiko Mkuu.
basi sawa. najuta kujifanya kiherehere. acha niendelee kujitafitia ugali wangu.

alijisemea "mama kizmkazi", kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake.

ila kuna jambo nimenotisi kati ya wewe na hao jamaa waliondolewa dstv, pia wewe na wahusika wa chaneli ya sinema zetu.
 
Yupi huyo Sophia?
Aisee

Kama ni kweli basi ni balaa.
 
Ni wachache sana wanakula jasho halali kwenye hii dunia hasa hasa Africa. Ukienda kwa mafundi lazima upwige, wafanya biashara wengi wanakwepa kodi , rushwa police, mahakamani, hospital, traffic, kwenye miradi mikubwa, mabenki kwenye kupata mikopo, bado hao wala rushwq wa kubwa. Yaani ni mwendo wa kuzidiana tu viwango.
 
sura tu na huyo dada barbara kambogi inasema mengi na kama ana mume basi huyo mume atakuwa ananyanyasika nae na anapelekeshwa mno
 
Pole sana Ila ndio maisha ya ofisini hayo. Nilishafurahishwa hamu sina Ila kwa wazungu kuna unafuu mkubwa sana tofauti na kwa races nyingine za business as usual
Wazungu hawa hawa ambao wamenyonya waafrika miaka na miaka. Na wao pia wanapiga madili hatari,ni viwango tu vinayofautiana.
 
Mimi ni mtoa habari tu Mkuu, sihusiki kwa namna yoyote na wala sifahamiani na mhusika yeyote.

Sikuwa na maana mbaya kukujibu vile, ushahidi ni muhimu kabla ya kuchukua hatua yoyote.
 
Laana za Ki Africa hizi, Mambo ya hili bara la Giza ni magumu sana.
Bara la giza tumejikita kwenye rushwa, mabeberu kwenye ushoga na kuchochea vita Duniani kwa maslahi yao. Hata hao wachina wanatoa hela.ndefu Africa ili kupata miradi mikubwa. Huko Amerika ya kati na kusini ndio wauza madawa wamebomea
Kila bara lina dhambi ambazo inazimudu vizuri. Hii ndio dunia, ni uwanja wa vita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…