Kumekucha DSTV, Mkurugenzi wa vipindi Maisha Magic Bongo na msaidizi wake wasimamishwa kwa rushwa!

Kumekucha DSTV, Mkurugenzi wa vipindi Maisha Magic Bongo na msaidizi wake wasimamishwa kwa rushwa!

Hata hizo huba,jua Kali unaona ni ndani,sijui hawawezi andika story za nje!!
😂😂😂😂😂
Wanapenda sana mteremko.


Juzikati bekitatu wetu anapambana kuangalia sijui mchezo gani huko Azam.
Nikamwambia sasa mchezo kama huo,watu wanashinda ndani..fungua chupa za chai ,wanakula
Mara wamelala
Wanafua..mbona hata wewe unaweza kucheza.

Kiukweli mm napenda michezo ya ngumi
Wafumuane ngumi za uhakika ndio naona kweli hapa muigizaji ameitolea jasho Sanaa yake.
 
Kuna dogo nilikuwa napiga naye stori
Ni upcani actor..Kuna kazi alisema atakuwepo inakuja ila ilivyokuja hakutokea

Kumuuliza ,akasema walishindwana malipo...hela ndogo mno akaona bora aipige tu chini.

Pia malipo yanategemea na character Yako na jina lako pia.
Wenye majina Makubwa unakuta mpunga angalau unaeleweka..
Beginners ndio hivyo mnabargain.

Maproducer wanafanya hivyo ili nao wabaki na chochote kitu..
Ndo maana wengine anaamua acheze tu uswahilini mwanzo mwisho ili abane bajeti kama mambo yenyewe ndio hayo ya kutoa hongo
Movie ukiwa begginer kubali kutumika,utakula ukikua,usitegemee kulipwa wakati unaanza
 
Mpaka upatikane ushahidi usio na shaka kama wa Isike, habari za kusikia tu hazina mashiko Mkuu.
basi sawa. najuta kujifanya kiherehere. acha niendelee kujitafitia ugali wangu.

alijisemea "mama kizmkazi", kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake.

ila kuna jambo nimenotisi kati ya wewe na hao jamaa waliondolewa dstv, pia wewe na wahusika wa chaneli ya sinema zetu.
 
nifah pitapita na pale azamtv. nasikia msimamizi wa chaneli ya sinema zetu ambayo imepewa jukumu la kuonyesha local tv series, ana michezo kama ya huyo wa dstv.

na yeye ni mwanamama/mwanadada pia. sasa unaambiwa usipotoa kwake ushirikiano wa rushwa , series/movie yako hata iwe bora kiasi gani, haiwezi kukubaliwa kuonyeshwa na azamtv.
Yupi huyo Sophia?
Aisee

Kama ni kweli basi ni balaa.
 
Ni wachache sana wanakula jasho halali kwenye hii dunia hasa hasa Africa. Ukienda kwa mafundi lazima upwige, wafanya biashara wengi wanakwepa kodi , rushwa police, mahakamani, hospital, traffic, kwenye miradi mikubwa, mabenki kwenye kupata mikopo, bado hao wala rushwq wa kubwa. Yaani ni mwendo wa kuzidiana tu viwango.
 
This is exclusive!

Mkurugenzi wa vipindi wa kitengo cha tamthilia za kiswahili zinazoruka kupitia kisimbuzi cha DSTV mwanamama Mtanzania Barbara Kambogi sambamba na msaidizi wake bwana Onesmus Ndarite yeye akiwa ni Mkenya wamesimamishwa kazi kwa tuhuma nzito za rushwa.

Mwanamama huyo na msaidizi wake walijijengea mfumo wao mahususi wa kuwezesha kuruka kwa sinema hizo za Kiswahili ndani ya kitengo hicho.

Mfumo huo ukiwa ni upigaji kwa pande zote, kwa madairekta kutakiwa kutoa hongo tamthilia zao zipate nafasi ndani ya DSTV, na huku haohao madairekta watakachopokea kutoka DSTV walitakiwa kugawana fungu na Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.

Hali hiyo ilidumu kwa kipindi kirefu, ikapelekea hadi wakawa sehemu ndani ya tamthilia za Jua Kali pamoja na Huba.
Ndio maana tamthilia hizo zinaikaribia Isidingo kwa ukaribu kwa mlolongo wa vipindi vyake visivyoisha!

Wazalishaji wa tamthilia hizo maarufu wanaofahamika ni mwanamama aliyejizolea sifa kubwa Leah Mwendamseke (Lamata) na Aziz Mohamed, ila nyuma ya pazia walikuwepo Mkurugenzi na msaidizi wake.

Ubadhirifu huo wa madaraka katika kitengo hicho uliingia sura mpya baada ya ingizo jipya la tamthilia ya Chanda.
Mkurugenzi kama ilivyo ada alitaka fungu liwekwe kama ulivyo utaratibu, mtayarishaji wa tamthilia hiyo bwana Isike Samweli alikataa kutoa ‘ushirikiano’
Ndipo balaa lilipozuka!

Mtayarishaji huyo (Isike Samweli) hapo awali alitayarisha tamthilia ya Pazia, na alitoa ushirikiano hadi alipokataa kwenye tamthilia yake mpya ya Chanda.
Alipokataa akaundiwa zengwe la kukatishwa kwa tamthilia yake hiyo ambayo bado ilikuwa inaendelea…

Bwana Isike hakukubalina na hilo, na kwa kuwa walikuwa na ‘ushirikiano’ hapo awali kwenye tamthilia ya Pazia alitunza ushahidi wote wa ushirikiano aliowahi kuwapa Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.

Bwana Isike alienda mbali zaidi kwa kumwaga ugali baada ya Mkurugenzi kutishia kumwaga mboga yake.
Alituma email kwenda makao makuu Afrika ya Kusini akiambatanisha na ushahidi wote wa miamala ya ‘ushirikiano’ aliowahi kuutoa.

Baada ya tuhuma hizo nzito zenye ushahidi kufika makao makuu, ndipo Mkurugenzi huyo na msaidizi wake waliposimamishwa kazi kwa haraka kupisha utaratibu mwingine kufanyika wa kushuhulikia hilo.

Pichani ni mwanamama Barbara Kambogi, na mtayarishaji aliyeundiwa zengwe bwana Isike Samweli.

Nikiripoti kutokea hapa JF kupitia chanzo changu makini,

Nifah.

View attachment 2825510View attachment 2825511
sura tu na huyo dada barbara kambogi inasema mengi na kama ana mume basi huyo mume atakuwa ananyanyasika nae na anapelekeshwa mno
 
Pole sana Ila ndio maisha ya ofisini hayo. Nilishafurahishwa hamu sina Ila kwa wazungu kuna unafuu mkubwa sana tofauti na kwa races nyingine za business as usual
Wazungu hawa hawa ambao wamenyonya waafrika miaka na miaka. Na wao pia wanapiga madili hatari,ni viwango tu vinayofautiana.
 
basi sawa. najuta kujifanya kiherehere. acha niendelee kujitafitia ugali wangu.

alijisemea "mama kizmkazi", kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake.

ila kuna jambo nimenotisi kati ya wewe na hao jamaa waliondolewa dstv, pia wewe na wahusika wa chaneli ya sinema zetu.
Mimi ni mtoa habari tu Mkuu, sihusiki kwa namna yoyote na wala sifahamiani na mhusika yeyote.

Sikuwa na maana mbaya kukujibu vile, ushahidi ni muhimu kabla ya kuchukua hatua yoyote.
 
Laana za Ki Africa hizi, Mambo ya hili bara la Giza ni magumu sana.
Bara la giza tumejikita kwenye rushwa, mabeberu kwenye ushoga na kuchochea vita Duniani kwa maslahi yao. Hata hao wachina wanatoa hela.ndefu Africa ili kupata miradi mikubwa. Huko Amerika ya kati na kusini ndio wauza madawa wamebomea
Kila bara lina dhambi ambazo inazimudu vizuri. Hii ndio dunia, ni uwanja wa vita
 
Back
Top Bottom