Kumekucha DSTV, Mkurugenzi wa vipindi Maisha Magic Bongo na msaidizi wake wasimamishwa kwa rushwa!

Kumekucha DSTV, Mkurugenzi wa vipindi Maisha Magic Bongo na msaidizi wake wasimamishwa kwa rushwa!

This is exclusive!

Mkurugenzi wa vipindi wa kitengo cha tamthilia za kiswahili zinazoruka kupitia kisimbuzi cha DSTV mwanamama Mtanzania Barbara Kambogi sambamba na msaidizi wake bwana Onesmus Ndarite yeye akiwa ni Mkenya wamesimamishwa kazi kwa tuhuma nzito za rushwa.

Mwanamama huyo na msaidizi wake walijijengea mfumo wao mahususi wa kuwezesha kuruka kwa sinema hizo za Kiswahili ndani ya kitengo hicho.

Mfumo huo ukiwa ni upigaji kwa pande zote, kwa madairekta kutakiwa kutoa hongo tamthilia zao zipate nafasi ndani ya DSTV, na huku haohao madairekta watakachopokea kutoka DSTV walitakiwa kugawana fungu na Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.

Hali hiyo ilidumu kwa kipindi kirefu, ikapelekea hadi wakawa sehemu ndani ya tamthilia za Jua Kali pamoja na Huba.
Ndio maana tamthilia hizo zinaikaribia Isidingo kwa ukaribu kwa mlolongo wa vipindi vyake visivyoisha!

Wazalishaji wa tamthilia hizo maarufu wanaofahamika ni mwanamama aliyejizolea sifa kubwa Leah Mwendamseke (Lamata) na Aziz Mohamed, ila nyuma ya pazia walikuwepo Mkurugenzi na msaidizi wake.

Ubadhirifu huo wa madaraka katika kitengo hicho uliingia sura mpya baada ya ingizo jipya la tamthilia ya Chanda.
Mkurugenzi kama ilivyo ada alitaka fungu liwekwe kama ulivyo utaratibu, mtayarishaji wa tamthilia hiyo bwana Isike Samweli alikataa kutoa ‘ushirikiano’
Ndipo balaa lilipozuka!

Mtayarishaji huyo (Isike Samweli) hapo awali alitayarisha tamthilia ya Pazia, na alitoa ushirikiano hadi alipokataa kwenye tamthilia yake mpya ya Chanda.
Alipokataa akaundiwa zengwe la kukatishwa kwa tamthilia yake hiyo ambayo bado ilikuwa inaendelea…

Bwana Isike hakukubalina na hilo, na kwakuwa walikuwa na ‘ushirikiano’ hapo kabla kwenye tamthilia ya Pazia alitunza ushahidi wote wa ushirikiano aliowapa Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.

Bwana Isike alienda mbali zaidi kwa kumwaga ugali baada ya Mkurugenzi kutishia kumwaga mboga yake.
Alituma email kwenda makao makuu Afrika ya Kusini akiambatanisha na ushahidi wote wa miamala ya ‘ushirikiano’ aliowahi kuutoa.

Baada ya tuhuma hizo nzito zenye ushahidi kufika makao makuu, ndipo Mkurugenzi huyo na msaidizi wake waliposimamishwa kazi kwa haraka kupisha utaratibu mwingine kufanyika wa kushuhulikia hilo.

Pichani ni mwanamama Barbara Kambogi, na mtayarishaji aliyeundiwa zengwe bwana Isike Samweli.

Nikiripoti kutokea hapa JF kupitia chanzo changu makini,

Nifah.

View attachment 2825510View attachment 2825511
Uvaaji wa suruali yake tu unatia mashaka
 
Hii mbona ipo kila mahali ?, Hata ngazi a Nchi hizi ni zile zinaitwa 10%, Unadhani Msemo wa Mkono Mtupu Haulambwi walimaanisha nini ?

Hata hao anaowapelekea Kesi kulaumu (unless ni owners kabisa) huenda nao wana mgao katika hii kitu (huenda na yeye kufika hapo alipo kuna waliochukua mgao)

It's a Dog eat Dog World....
 
Unazungumzia wa mkurugenzi wa DSTVmkuu?huyo ana nini hadi uone hawezi kula rushwa?

Zungumzia wa waziri fulani serikalini huku mshahara ukiambatana na allowance chungu mbovu lakini bado huwa wanakunja noti,ukiona mikataba mibovu tunayoingizwa na hao viongozi usidhani ule ni utashi wao kuna kitu behind.
Kadri mshahara unavyokuwa mkubwa, ndio kadri ambavyo dau lake la rushwa linavyokuwa kubwa.
 
Unazungumzia wa mkurugenzi wa DSTVmkuu?huyo ana nini hadi uone hawezi kula rushwa?

Zungumzia wa waziri fulani serikalini huku mshahara ukiambatana na allowance chungu mbovu lakini bado huwa wanakunja noti,ukiona mikataba mibovu tunayoingizwa na hao viongozi usidhani ule ni utashi wao kuna kitu behind.
Kwahiyo ndio tuhalalishe rushwa kila mahali?
Unajua ni kiasi gani watu wanakwamishwa kwa kushindwa kutoa rushwa?

Mfano hapa kama Isike asingetunza ushahidi tamthilia yake ilikuwa inapigwa chini!

Huyo Isike ana watu wengi nyuma yake, kuanzia washiriki mpaka wafanyakazi wa kawaida wanaotegemea mafanikio ya tamthilia wapate namna za kuendeleza maisha yao!
 
Back
Top Bottom