KUTATABHETAKULE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 5,159
- 5,070
...uuuuui twafa....Kama mshahara wa mkurugenzi dstv hautoshi sisi waalimu wa daraja la iii B vijijini tusemeje
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
...uuuuui twafa....Kama mshahara wa mkurugenzi dstv hautoshi sisi waalimu wa daraja la iii B vijijini tusemeje
Pesa yako tu chawa wako wengiSasa nifanyeje jamani? Kwani wewe unao boss?
50/50Wanawake wengine wana tabia za kiume!💔
Usiutamani ufahari wa mtu muovu utapotea.Ila Tanzania kwenye rushwa na wizi hatuchekani. Ukiwa muadilifu, deal za ofisi zinakupitia pembeni na unaweza undiwa dengee ili ufukuzwe kama nafasi yako inawaletea watu kikwazo kwenye michakato yao.
Ubaya sasa, kheri uwe muadilifu na mshahara uwe unaeleweka. Ila kwa wengi ndio wale wanaishi maofisini kwa depression, unakomaa na mshahara halafu uliowazidi vyeo wanakuzidi maisha
Nope wala sikubaliani na mambo mengi sana yanayoendelea bali it is what it is.... Sekta zote kuna Umimi na Its not how good your product is bali how good your connections are... Especially kwenye entertainment industry it has always been this way..., Its just the way it is.... Hata redio mbao kama haujatoka bila kuwapa ma-Dj faranga ngoma yako huenda isipigwe... au ukijifanya mjanja unaweza ukawa blacklisted..., huenda ndio maana huyo jamaa kaamua kwanza ajulikane na kazi zake zijulikane ndio kapata nguvu za kubishaKwahiyo tuhalalishe rushwa?
Duh rushwa ni mbaya sanaThis is exclusive!
Mkurugenzi wa vipindi wa kitengo cha tamthilia za kiswahili zinazoruka kupitia kisimbuzi cha DSTV mwanamama Mtanzania Barbara Kambogi sambamba na msaidizi wake bwana Onesmus Ndarite yeye akiwa ni Mkenya wamesimamishwa kazi kwa tuhuma nzito za rushwa.
Mwanamama huyo na msaidizi wake walijijengea mfumo wao mahususi wa kuwezesha kuruka kwa sinema hizo za Kiswahili ndani ya kitengo hicho.
Mfumo huo ukiwa ni upigaji kwa pande zote, kwa madairekta kutakiwa kutoa hongo tamthilia zao zipate nafasi ndani ya DSTV, na huku haohao madairekta watakachopokea kutoka DSTV walitakiwa kugawana fungu na Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.
Hali hiyo ilidumu kwa kipindi kirefu, ikapelekea hadi wakawa sehemu ndani ya tamthilia za Jua Kali pamoja na Huba.
Ndio maana tamthilia hizo zinaikaribia Isidingo kwa ukaribu kwa mlolongo wa vipindi vyake visivyoisha!
Wazalishaji wa tamthilia hizo maarufu wanaofahamika ni mwanamama aliyejizolea sifa kubwa Leah Mwendamseke (Lamata) na Aziz Mohamed, ila nyuma ya pazia walikuwepo Mkurugenzi na msaidizi wake.
Ubadhirifu huo wa madaraka katika kitengo hicho uliingia sura mpya baada ya ingizo jipya la tamthilia ya Chanda.
Mkurugenzi kama ilivyo ada alitaka fungu liwekwe kama ulivyo utaratibu, mtayarishaji wa tamthilia hiyo bwana Isike Samweli alikataa kutoa ‘ushirikiano’
Ndipo balaa lilipozuka!
Mtayarishaji huyo (Isike Samweli) hapo awali alitayarisha tamthilia ya Pazia, na alitoa ushirikiano hadi alipokataa kwenye tamthilia yake mpya ya Chanda.
Alipokataa akaundiwa zengwe la kukatishwa kwa tamthilia yake hiyo ambayo bado ilikuwa inaendelea…
Bwana Isike hakukubalina na hilo, na kwakuwa walikuwa na ‘ushirikiano’ hapo kabla kwenye tamthilia ya Pazia alitunza ushahidi wote wa ushirikiano aliowapa Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.
Bwana Isike alienda mbali zaidi kwa kumwaga ugali baada ya Mkurugenzi kutishia kumwaga mboga yake.
Alituma email kwenda makao makuu Afrika ya Kusini akiambatanisha na ushahidi wote wa miamala ya ‘ushirikiano’ aliowahi kuutoa.
Baada ya tuhuma hizo nzito zenye ushahidi kufika makao makuu, ndipo Mkurugenzi huyo na msaidizi wake waliposimamishwa kazi kwa haraka kupisha utaratibu mwingine kufanyika wa kushuhulikia hilo.
Pichani ni mwanamama Barbara Kambogi, na mtayarishaji aliyeundiwa zengwe bwana Isike Samweli.
Nikiripoti kutokea hapa JF kupitia chanzo changu makini,
Nifah.
View attachment 2825510View attachment 2825511
Kwahyo huyu mama alikuwa anatembea nani? Nafikiria namna alivyofaidiSi tu kutaka fungu la kumi, bali walikuwa wanatembea na wasanii wanaotaka kazi zao zionyeshwe Dstv.
Kikubwa pesa ipatikane, wale wwngine wanatumia rasilimali zao na yeye anatumia cheo chakeSasa Mkurugenzi nae tutamuweka sawa na wauzaji kweli?
Mimi siyo chawa.Pesa yako tu chawa wako wengi
Ongea na Lucas mwashambwa 😂😂
Ishi kulingana na kipato chako, au ibia wanafunziKama mshahara wa mkurugenzi dstv hautoshi sisi waalimu wa daraja la iii B vijijini tusemeje
Na wanaangalia wakiwa na wanao.Kumbe kuna watu wanaangaliaga hivyo
Vipindi
Ova
Kuna familia kuanzia saa 12 jioni hadi saa 4 usiku ni tamthilia bandika bandua. Yaani hata taarifa ya habari ya saa 2 usiku unaangalia kupitia youtube kwani remote hugusi na TV yenyewe moja tu.Shemeji zenu wanafanya tunaangalia.
Jua kali na Huba hazinipiti siku hizi......
Sio kweli, tupo sisi watoto wa kimasikini na tunaishi vizuri tu huku makazini kwa uadilifu.Kufanya kazi private sector ni kujitafutia stress hasa kwa watoto wakimasikini huko wanatakiwa watoto wakishua kwasababu wana back up la sivyo pressure na kisukari zitakuondoa mapema.