Kumekucha DSTV, Mkurugenzi wa vipindi Maisha Magic Bongo na msaidizi wake wasimamishwa kwa rushwa!

This is exclusive!

Mkurugenzi wa vipindi wa kitengo cha tamthilia za kiswahili zinazoruka kupitia kisimbuzi cha DSTV mwanamama Mtanzania Barbara Kambogi sambamba na msaidizi wake bwana Onesmus Ndarite yeye akiwa ni Mkenya wamesimamishwa kazi kwa tuhuma nzito za rushwa.

Mwanamama huyo na msaidizi wake walijijengea mfumo wao mahususi wa kuwezesha kuruka kwa sinema hizo za Kiswahili ndani ya kitengo hicho.

Mfumo huo ukiwa ni upigaji kwa pande zote, kwa madairekta kutakiwa kutoa hongo tamthilia zao zipate nafasi ndani ya DSTV, na huku haohao madairekta watakachopokea kutoka DSTV walitakiwa kugawana fungu na Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.

Hali hiyo ilidumu kwa kipindi kirefu, ikapelekea hadi wakawa sehemu ndani ya tamthilia za Jua Kali pamoja na Huba.
Ndio maana tamthilia hizo zinaikaribia Isidingo kwa ukaribu kwa mlolongo wa vipindi vyake visivyoisha!

Wazalishaji wa tamthilia hizo maarufu wanaofahamika ni mwanamama aliyejizolea sifa kubwa Leah Mwendamseke (Lamata) na Aziz Mohamed, ila nyuma ya pazia walikuwepo Mkurugenzi na msaidizi wake.

Ubadhirifu huo wa madaraka katika kitengo hicho uliingia sura mpya baada ya ingizo jipya la tamthilia ya Chanda.
Mkurugenzi kama ilivyo ada alitaka fungu liwekwe kama ulivyo utaratibu, mtayarishaji wa tamthilia hiyo bwana Isike Samweli alikataa kutoa ‘ushirikiano’
Ndipo balaa lilipozuka!

Mtayarishaji huyo (Isike Samweli) hapo awali alitayarisha tamthilia ya Pazia, na alitoa ushirikiano hadi alipokataa kwenye tamthilia yake mpya ya Chanda.
Alipokataa akaundiwa zengwe la kukatishwa kwa tamthilia yake hiyo ambayo bado ilikuwa inaendelea…

Bwana Isike hakukubalina na hilo, na kwa kuwa walikuwa na ‘ushirikiano’ hapo awali kwenye tamthilia ya Pazia alitunza ushahidi wote wa ushirikiano aliowahi kuwapa Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.

Bwana Isike alienda mbali zaidi kwa kumwaga ugali baada ya Mkurugenzi kutishia kumwaga mboga yake.
Alituma email kwenda makao makuu Afrika ya Kusini akiambatanisha na ushahidi wote wa miamala ya ‘ushirikiano’ aliowahi kuutoa.

Baada ya tuhuma hizo nzito zenye ushahidi kufika makao makuu, ndipo Mkurugenzi huyo na msaidizi wake waliposimamishwa kazi kwa haraka kupisha utaratibu mwingine kufanyika wa kushuhulikia hilo.

Pichani ni mwanamama Barbara Kambogi, na mtayarishaji aliyeundiwa zengwe bwana Isike Samweli.

Nikiripoti kutokea hapa JF kupitia chanzo changu makini,

Nifah.

View attachment 2825510View attachment 2825511

Laana za Ki Africa hizi, Mambo ya hili bara la Giza ni magumu sana.
 
Mimi naona hili jambo ni zuri sana katika sanaa ya maigizo bongo, italeta mapinduzi kwa kazi bora kupitishwa bila rushwa iliyozaa maigizo na waigizaji wabovu.
Huko kwenyewe kwenye sanaa kuna rushwa kubwa ya ngono.

Ndio maana wamejazana mabinti,warembo,wenye matako makubwa nk nia wapateplatforms ya kuonekana na madanga.kwa wanaume mashombeshombe,mahb kibao nk,talent hawana ila uzuri ndio uliowapa nafasi. Tena huko kwenye kambi zao wanagongana sana.
 
Kwahiyo ndio tuhalalishe rushwa kila mahali?
Unajua ni kiasi gani watu wanakwamishwa kwa kushindwa kutoa rushwa?

Mfano hapa kama Isike asingetunza ushahidi tamthilia yake ilikuwa inapigwa chini!

Huyo Isike ana watu wengi nyuma yake, kuanzia washiriki mpaka wafanyakazi wa kawaida wanaotegemea mafanikio ya tamthilia wapate namna za kuendeleza maisha yao!
cheque inatolewa ya million 200 ila mpaka inamfikia mwenye tamthilia yake hapo si haba mtu anakunja 50M tu. Aanze kuwagaia wachezaji movie utashangaa kila mtu kapata million 3 tamthilia nzima 🤣🤣🤣
 
This is exclusive!

Mkurugenzi wa vipindi wa kitengo cha tamthilia za kiswahili zinazoruka kupitia kisimbuzi cha DSTV mwanamama Mtanzania Barbara Kambogi sambamba na msaidizi wake bwana Onesmus Ndarite yeye akiwa ni Mkenya wamesimamishwa kazi kwa tuhuma nzito za rushwa.

Mwanamama huyo na msaidizi wake walijijengea mfumo wao mahususi wa kuwezesha kuruka kwa sinema hizo za Kiswahili ndani ya kitengo hicho.

Mfumo huo ukiwa ni upigaji kwa pande zote, kwa madairekta kutakiwa kutoa hongo tamthilia zao zipate nafasi ndani ya DSTV, na huku haohao madairekta watakachopokea kutoka DSTV walitakiwa kugawana fungu na Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.

Hali hiyo ilidumu kwa kipindi kirefu, ikapelekea hadi wakawa sehemu ndani ya tamthilia za Jua Kali pamoja na Huba.
Ndio maana tamthilia hizo zinaikaribia Isidingo kwa ukaribu kwa mlolongo wa vipindi vyake visivyoisha!

Wazalishaji wa tamthilia hizo maarufu wanaofahamika ni mwanamama aliyejizolea sifa kubwa Leah Mwendamseke (Lamata) na Aziz Mohamed, ila nyuma ya pazia walikuwepo Mkurugenzi na msaidizi wake.

Ubadhirifu huo wa madaraka katika kitengo hicho uliingia sura mpya baada ya ingizo jipya la tamthilia ya Chanda.
Mkurugenzi kama ilivyo ada alitaka fungu liwekwe kama ulivyo utaratibu, mtayarishaji wa tamthilia hiyo bwana Isike Samweli alikataa kutoa ‘ushirikiano’
Ndipo balaa lilipozuka!

Mtayarishaji huyo (Isike Samweli) hapo awali alitayarisha tamthilia ya Pazia, na alitoa ushirikiano hadi alipokataa kwenye tamthilia yake mpya ya Chanda.
Alipokataa akaundiwa zengwe la kukatishwa kwa tamthilia yake hiyo ambayo bado ilikuwa inaendelea…

Bwana Isike hakukubalina na hilo, na kwa kuwa walikuwa na ‘ushirikiano’ hapo awali kwenye tamthilia ya Pazia alitunza ushahidi wote wa ushirikiano aliowahi kuwapa Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.

Bwana Isike alienda mbali zaidi kwa kumwaga ugali baada ya Mkurugenzi kutishia kumwaga mboga yake.
Alituma email kwenda makao makuu Afrika ya Kusini akiambatanisha na ushahidi wote wa miamala ya ‘ushirikiano’ aliowahi kuutoa.

Baada ya tuhuma hizo nzito zenye ushahidi kufika makao makuu, ndipo Mkurugenzi huyo na msaidizi wake waliposimamishwa kazi kwa haraka kupisha utaratibu mwingine kufanyika wa kushuhulikia hilo.

Pichani ni mwanamama Barbara Kambogi, na mtayarishaji aliyeundiwa zengwe bwana Isike Samweli.

Nikiripoti kutokea hapa JF kupitia chanzo changu makini,

Nifah.

View attachment 2825510View attachment 2825511
Sijui unasumbuliwa na nin

Wew na kilemba chako hata hamfanan na kuwa utopolo [emoji41][emoji41][emoji41]
 
Ila Tanzania kwenye rushwa na wizi hatuchekani. Ukiwa muadilifu, deal za ofisi zinakupitia pembeni na unaweza undiwa dengee ili ufukuzwe kama nafasi yako inawaletea watu kikwazo kwenye michakato yao.

Ubaya sasa, kheri uwe muadilifu na mshahara uwe unaeleweka. Ila kwa wengi ndio wale wanaishi maofisini kwa depression, unakomaa na mshahara halafu uliowazidi vyeo wanakuzidi maisha
Watu wanapiga mishindo wanajenga Mbweni na Kigamboni majengo ya kisasa we unakalia uzalendo mavi. Uzalendo haulipi sikuhizi we ukipata channel ishi tu.
 
Back
Top Bottom