Mkuu, hivi wanaposema cyber attack inamaanisha nini? Sasa hapo chopper gunships zinahusika vipi, ingawa unasema picha haziusiani na matukio, sasa inazibanfika hapa ukiwa na lengo la ku-pre empty kitu gani? Mnapenda penda sana ku- exaggerated mambo hasa yanayo husu Israel na maadui zake.
Serikali ya Iran inasema kilicho tokea ni power outage kutokana na kuingiliwa kwa mfumo wa kuzalisha umeme wa kuendeshea mitambo yao, hii si mara ya kwanza mitambo ya Iran ya kuzalishia plutonium kuingiliwa na virus na kuisabibishia uharibifu.
Hapa naona magazeti pamoja na vyombo vya habari vingine vya huko Israel vinaweka chumvi mno, eti "uharibifu ulikuwa mkubwa mno kuliko Iran inavyo sema/kili!"
Binafsi naona hujuma hizo zimetekelezwa na Israel intel agents au Wairan wasaliti wanao lipwa na Israel kuhujumu efforts za Iran kizalisha plutonium,kumbuka Iran ina raia-wengi wenye asili ya Israel/Jews kama ilivyo Taifa la Urusi kuna Jews wengi tu.
Hujuma hii bila shaka imetekelezwa na Israel baada ya kukasirishwa na utawala wa Merikani/Biden kutaka kuwa na mazungumzo na Iran yenye lengo la kuiondolea Iran vikwazo vya kiuchumi kama Wairan watakubali ku-comply na mashariti ya kusitisha vinu vyake kuzalishaji weapon grade Plutonium.
Ni wazi Biden na utawala wake hawawezi kukubali kuwa blackmailed na Natenyahu ambaye ni Waziri Mkuu wa Israel anae g'ang'ania kwenye madaraka na anatamani sana majeshi ya USA na washirika wake kuishambulia Iran.