Kumekucha: kamati ya waamuzi (ZFF) yasema Simba ilipendelewa

Kumekucha: kamati ya waamuzi (ZFF) yasema Simba ilipendelewa

Maelezo ya mwakilishi wa kamati hayaja conclude moja kwa moja kuwa haikuwa kona

Kilichojadiliwa ni opinions za wana kamati kwa jinsi walivyoona


Kamati imeonesha wasiwasi wa lile tukio kutokuwa kona na ndio maana wamesema "kwa jinsi walivyoona wao hawakuona connection ya Kigili kuugusa ule mpira so mpira ulikuwa ni goal kick"
 
Kamati ya waamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), imesema kuwa Mwamuzi Nasri Salum hakustahili kuipa Simba kona iliyoifanya ipate bao la kusawazisha, katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, wakati ikicheza na Singida Fountain Gate jana kwenye Uwanja wa Amaan.

Katika mchezo huo, Simba iliibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida wa mchezo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Waziri Shekha amesema uamuzi wa kuipa Simba kona katika dakika za nyongeza, haukuwa sahihi na kwa mwamuzi huyo alifanya makosa, japo kamati hiyo haiwezi kumpa adhabu.

"Nilikwambia kwamba tutachunguza na tumekutana leo, tumebaini kwamba kulikuwa na makosa ya mwamuzi. Haikupaswa kuwa kona. Hakuna sehemu ambayo mpira ulichezwa na mchezaji wa Singida na kipa akaudakia nje, hivyo haikuwa sahihi kuwa kona,” amesema na kuongeza;

“Ni makosa ya kibinadamu na ndio kosa pekee tumeliona baada ya kupitia ripoti na marudio ila sehemu zingine zote alikuwaa sahihi. Uzito wa kosa alilofanya hautoshi kumpa adhabu refa huyo ukizingatia amekuwa akichezesha vyema mechi nyingi.”
Na Ile penant waliiongelea?
 
Maelezo ya mwakilishi wa kamati hayaja conclude moja kwa moja kuwa haikuwa kona

Kilichojadiliwa ni opinions za wana kamati kwa jinsi walivyoona


Kamati imeonesha wasiwasi wa lile tukio kutokuwa kona na ndio maana wamesema "kwa jinsi walivyoona wao hawakuona connection ya Kigili kuugusa ule mpira so mpira ulikuwa ni goal kick"
Hayo ni maneno yako
1704982251294.jpg
 
Wanatuchosha.

Ngoja tupate hizo milioni 100 kwa kikosi cha bilioni 3.

Hii naona kama biashara kichaa.
 
Wazanzibari wakati mwingine wana ujinga mwingi. Hauwezi kuona FIFA au CAF wanatoa waziwazi ufafanuzi wa namna hii. Kwanza watu wenyewe wanaangalia clip hizi hizi zenye utata tunazoangalia wote.
 
Hii timu isingekuwa inabebwa na waamuzi vilaza, Bodi ya ligi na TFF ya Karia, mpaka muda huu ingekuwa inacheza ligi daraja la kwanza huko.
 
Mi sijui kwanini naona lile lilikuwa kosa la kawaida na linawatokea wengi kilichonishangaza ni kwamba refa kaongeza dk 6 ila zimeisha game ikaendelea ila kolo alivosawazisha tu hapo hapo refa akamaliza mpira. Mi kwangu hiki ndo kilinishangaza.
 
UNa mambo ya kingese kweli
Sio kila anaechangia hoja humu ni mzima. Ukiona alicgokuwa akiandika Jana wakati WA mechi utashangaa Kuna na mgonjwa mwingine alikuwa anaandika majina meengi ya utani ya Simba sijui KAPONA?. Na huyu MUNGU atamfanyia wepesi sio Mzima.
 
Back
Top Bottom