VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Hatimaye, malalamiko ya watanzania kuhusu uhalali na vipengele vya Mkataba kati ya Tanzania na Emirati ya Dubai kupitia Kampuni ya DP World yamewafikia na kuwashtua wahusika. Taarifa za uhakika nilizozipata zinaonesha kuwa DP World wamesikia hoja za wazalendo wa kitanzania na wameguswa nazo.
Katika kutaka kujiridhisha ili kutoa uamuzi juu ya nini cha kufanya, DP World imewatuma nchini Maafisa wake watatu ili kupata undani wa jambo hilo. DP World imewatuma Maafisa wake hao ambao wamewasili nchini jana na wanatarajiwa kuzungumza sirini na makundi tofautitofauti.
Maafisa hao watazungumza na viongozi wa kiserikali na kichama-CCM; viongozi wa TPA; viongozi wastaafu mbalimbali wenye 'kuukubali' na wale 'wa kuupinga' Mkataba huo; wanasheria mbalimbali wenye mtazamo tofauti; wasomi wenye mtazamo tofauti, wanasiasa na wananchi wa kawaida.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa DP World kufanya jambo kama hili ili kuamua cha kufanya kabla ya muda wa kuingia Mikataba Mahsusi kufika. Kwangu mimi, hii ni hatua muhimu na adhimu kwakuwa DP World watayasikia yale yanayofurahisha na kukatisha tamaa kuhusu Mkataba wao.
Rais Samia, nini maoni yako kuhusiana na Mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na DP World?
Mzee Tupatupa wa Lumumba ( safarini kurejea Dar es Salaam)