Kumekucha Madawa ya Kulevya: Kina 'Masogange' wawataja waliowatuma!

Kumekucha Madawa ya Kulevya: Kina 'Masogange' wawataja waliowatuma!

mkuzi

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2013
Posts
1,627
Reaction score
1,459
Staa muuza nyago kwenye video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu za Kibongo, Agnes Gerald ‘Masogange' na shosti wake, Mellisa Edward kabla ya kupandishwa kizimbani kwa msala wa dawa za kulevya ‘unga' Afrika Kusini waliingizwa kwenye chumba cha mateso kwa saa 24 ili kutaja waliowatuma.

Habari kutoka kwa chanzo chetu kilichopo jijini Johannesburg nchini humo zilidai kuwa baada ya kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, walipelekwa polisi ambapo walichukuliwa maelezo.

Ilielezwa kuwa mwanzoni waligoma kueleza mzigo huo wa kilo 150 wa unga ulikuwa wa nani hivyo ikabidi polisi wa upelelezi watafute njia nyingine ya kuwalainisha kwa kuwabembeleza kuwa wakieleza ukweli wataachiwa.

MATESO SAA 24

Chanzo hicho kilisema kuwa baada ya mbinu hiyo kushindikana ndipo wawili hao wakaingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ikiaminika kuwa watasema aliyewatuma.

USHUHUDA

"Unajua Sauzi (Afrika Kusini) huwa hawana utani na ishu za madawa ya kulevya. Jamaa (polisi) wana kila aina ya mbinu ya kumfanya mtu aeleze ukweli.

"Katika kutesa unaweza kuingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ambayo nayo huwa yana steji zake.

"Kwanza utaanzia kwenye chumba kilichojazwa siafu wakubwa na huko unaweza usijue kuwa kuna siafu zaidi ya kuona kitu kama red carpet (zuria jekundu) kuanzia sakafuni, ukutani hadi kwenye dari, kumbe wale wote ni siafu.

"Wakishakuingiza mle ndipo utashangaa wale siafu wanacharuka na kuanza kukung'ata mwili mzima, zoezi hilo hufanyika kwa saa 24. Lazima useme ukweli.

"Kama bado ukijifanya mbishi au nunda ndipo unapelekwa hatua nyingine ya kulazimishwa kujisaidia haja ndogo kwenye waya wa umeme.

"Si unajua tena waya wenye umeme na maji vikikutana nini kinatokea? Lazima itatokea shoti ya kutisha kwani ule waya hufuata sehemu yale maji yanapotokea.

"Kinachofuata ni mtu kupigwa shoti kali ya umeme ambapo lazima utasema tu.

"Hicho ndicho kilichowapata akina Masogange kama wanavyofanyiwa Wabongo wengine wanaokamatwa Mitaa ya Rissik hapa Johannesburg.

WALIOWATUMA

"Baada ya mateso hayo, waliwataja waliowatuma mzigo huo wa unga aina ya crystal methamphetamine wenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8," kilisema chanzo hicho ambacho ni Mbongo ambaye kwa sasa ni mkazi wa Mtaa wa Rissik, Johannesburg, wanapoishi Wabongo kwa kuungaunga aliyewahi kukumbwa na mkasa kama huo.

MTOTO WA KIGOGO ATAJWA

Habari za ndani zilidai kuwa baada ya kupitia mateso hayo, mabinti hao waliwataja watu wawili waliowatuma kusafirisha mzigo huo, mmoja akiwa ni mtoto wa kigogo ambaye ni mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania (jina lipo).

Ilidaiwa kuwa mtoto huyo wa mkubwa ni mjanja wa mjini ambaye alihusika kushughulikia kusafirisha mwili wa msanii Albert Mangweha ‘Ngwea' aliyefia Johannesburg Juni, mwaka huu.

Ilivuja kuwa mwingine aliyetajwa na akina Masogange ni mfanyabiashara maarufu Bongo anayesafiri nje mara kwa mara huku jina la ‘mtoto wa mjini' Mangunga likitajwa zaidi hata na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George Mwakyembe.

Gazeti hili lilipozungumza na Kamanda wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa, alikiri kupewa majina hayo lakini akaliomba gazeti hili kutoyachapisha kwa sasa kuepuka kuvuruga ushahidi.

ULINZI KAMA SHEHE PONDA

Baada ya polisi wa upelelezi na wale wa kimataifa (Interpol) kujiridhisha na maelezo ya mabinti hao, walipandishwa kizimbani kwa mara ya pili Agosti 19, mwaka huu chini ya ulinzi mkali kama ule ‘anaowekewaga' Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda anapofikishwa kwenye mahakama mbalimbali nchini kwa kesi zake za madai ya uchochezi.

WAPANDISHWA TENA KORTINI

Habari kutoka Sauzi zilieleza kuwa akina Masogange walipandishwa tena kizimbani hivi karibuni ambapo tayari kesi yao imeanza kuunguruma ikielezwa kuwa endapo watakutwa na hatia watakula mvua ya kifungo si chini ya miaka 10 kwa sheria za nchi hiyo.

Masogange na Mellisa walinaswa nchini humo Julai 5, mwaka huu wakiwa na mabegi sita yaliyokuwa na mzigo huo wa unga.

======
Mfululizo wa kukamatwa, kesi, hukumu na kuachiwa huru kwa Agnes Masogange kwenye kesi ya Madawa ya kulevya
Masogange ajisalimisha mwenyewe Mahakama a Kisutu
Kupandishwa kizimbani na kusomewa shitaka
Yaliyojili wakati wa kesi ya Masogange
Masogange kupelekwa kwa Mkemia Mkuu
Kesi kusikilizwa
Tetesi za kuachiwa huru
Hukumu
 
Pumbav zao ikiwezekana wanyongwe kabisa mbwa hao, na serikali yetu nayo ishirikiane na Afrika Kusini ktk kuhakikisha kwamba hao wanaotajwa nao wanafikishwa kunakohusika. Tumechoka kuona watu wajingawajinga dizain yao malaya wanaichafua nchi yetu.
 
Magazeti ya Global Publisherz huwa ni wapuuzi sana, yaani wamejaa udaku udaku tu. Kama wanashindwa kutaja wahusika wanaandika habari ili iweje?. Masogange anapaswa kupewa adhabu kali ili iwe ni fundisho kwa Vijana wenye tamaa.
 
Mimi ninachoona hapo hata wakipewa adhabu ya kufa hao sio kwamba tatizo litakuwa limeisha, hivyo ni viji tawi tu, matawi makubwa na mashina yake hayaguswi sasa basi tutafute shina na si kwamba hayajulikani lahasha yanajulikana lakini nani wa kumvisha paka kengele, Tanzania hakuna shamba la unga lakini ndio wasambazaji wakubwa waunga je unatoka wap? Juzi juzi kakamata mchina mchana kweupe na mbeg mzima, jana tena yule Dada hapo hapo hamuoni km kuna chanzo? Na kwa nini wanakamatwa lakini bado wanapita? Inamaana wanaopita ni wengi kuliko wanaokamatwa!
Wito wangu kwa serikali isifanye masihala na swala hiki na wala wasidhani watakuwa kwenye hizo nafasi milele, km unachekelea kudhulika au kunyanyasika kwa mwenzako kesho itakuwa kwako.
Naamini km serikali ikiamua haishindwi. Ila kwa sasa imeamua kutishindana na wauza unga.
 
Pumbav zao ikiwezekana wanyongwe kabisa mbwa hao, na serikali yetu nayo ishirikiane na Afrika Kusini ktk kuhakikisha kwamba hao wanaotajwa nao wanafikishwa kunakohusika. Tumechoka kuona watu wajingawajinga dizain yao malaya wanaichafua nchi yetu.

Iwe fundisho kwa vijana wenye tamaa ili wasitumiwe hovyo.
 
Mbona mambo yako wazi kabisa??
Mwenye Mzigo ni Kinje Ngombale Mwiru. Huyu anajulikana na narudia kusema tena ndiye aliyetumika kumuharibu mtoto wa Sitta ALIYEMZAA kwa mkewe mkubwa aitwaye Valeria(rip).

Huyu tena anashirikiana na Shomar Kimbau sijui kwanini watu wanawaonea aibu hawa watu.
 
Punda hawa wa madawa ya kulevya wanyee debe iwe fundisho.
 
Ha!ha!ha!Leo ndo Mnamjua huyo mtoto wa mwanasiasa mkongwe ngoja niendelee Kupita zangu mpaka kampala kwenye mkutano.
 
kwanini mnaficha si mseme kweli??
\

cc manshiroo
Mwenyewe nashangaa kwann wasiseme ukweli na hao vinara wachukuliwe hatua?maana wanatesa sana vijana wetu,af wao hata hawapati madhara yoyote zaidi ya kujenga minyumba ya fahari na kuishi kama hakuna kitu kinachoitwa kifo,na Mungu awaadhibu
 
Mbona mambo yako wazi kabisa??
Mwenye Mzigo ni Kinje Ngombale Mwiru. Huyu anajulikana na narudia kusema tena ndiye aliyetumika kumuharibu mtoto wa Sitta ALIYEMZAA kwa mkewe mkubwa aitwaye Valeria(rip).

Huyu tena anashirikiana na Shomar Kimbau sijui kwanini watu wanawaonea aibu hawa watu.
huyu kinje toka niko nakua namsikia akitajwa tajwa sijui kwanini huwa watu wanamunea aibu kumuadabisha
 
Huyu masogange wamuache tu jamani! Wasimfunge wanirudishie baibi wetu.
 
Yaani tangu mkubwa aliposema ana orodha ya majina ya wafanya hii biashara na hajawahi chukua hatua yeyote hadi sasa hivi, na juzi wabunge kuzua kizazaa cha kutaka wauza unga watajwe ikawa mizengwe, sina cha kusema.
 
Back
Top Bottom