Kumekucha: Maji kutoka Ziwa Victoria mpaka Dodoma

Kumekucha: Maji kutoka Ziwa Victoria mpaka Dodoma

Wakumbushe tu kuwa wenzetu husimamia mikataba pale Mwanza kuna wamsiri kabisa na ofisi zao kwa ajili ya kutoa ripoti kwa serikali yao kile kinachoendelea pale ziwa Nyanza
Hapa maeneo ya makumbusho niliona wana ofisi ya mwambata wa kijeshi, kwa hiyo kwenye nchi zote ambazo mto nile unapita wameweka watu wao kumulika kila project inayotaka kuanzishwa......kuhusu mradi wa bwawa kule ethiopia wanatunishiana misuli hadi wameomba UN waingilie kati.
 
Juzi kwenye taarifa ya habari nimeona wananchi wa mara wanalalamika hawana maji wakati wapo karibu na ziwa inakuwaje maji yanapelekwa mbali wakati waliozungukwa na maji wanalalamika


Sio Mara tu hata wakazi wa kigoma shida ni hiyo hiyo licha ya kuwepo kwa ziwa Tanganyika jirani.

Ziwa Tanganyika ndiyo ziwa refu kuliko maziwa yote duniani na ziwa lenye kina kirefu la kwanza au la pili duniani.
 
Ni porojo tu na political stunts za uchaguzi uchwara, wilaya ya Magu haina huduma za maji na imepakana na Ziwa Nyanza (Victoria)... itakuwa Dodoma..!!
"Uchaguzi Uchwara" 😃Wajuvi naombeni tafsiri ya neno " UCHWARA"
 
Endapo Jambo Hili Litafanikiwa Hakika Ndugu Zangu Dodoma
Kutumia Maji Ya Visima Toka Mzakwe Itabaki Story
Huu Mradi Ulikuwa Unasemwa Zamani Sana


Dodoma Pia Tutachimba Mtaro Wa Maji Bahari Toka Dar es salaam Yaende Dodoma
kuna eneo la kutosha kutengeneza bahari ya dodoma.

Dar ni mkoani tu mambo yote yako Dodoma😀
 
Mnataka kutumia loophole ya mtifuano uliopo kati ya Misri na Ethiopia, au mnafikiri hao jamaa wamelala....hizi ahadi huwa zinatoka sana kuelekea uchaguzi, lakini mara nyingi hazina uhalisia..
Umetumwa na "kamiliusi"
 
Misri hawawezi kutifuana na sisi,, kwa mradi tuliowapa wa Bwawa la Umeme lazima watakaa kimya. Ila pia ni ujinga eti upo na chakula unakilinda then unakufa njaa wakati jirani yako anakuja anakula na kushiba hicho hicho unacholinda.

Mikataba mingine ni wehu mtupu!!

Binafsi huwa sielewi yale makatazo ya kuvuna samaki Ziwa fulani wakati Nchi jirani zinavua bila kikomo, au samaki wa kule wa kule.?

Ni sawa na hao Wamisri, wanafaidi samaki na kilimo kwa maji kutoka Victoria... wenyeji vikwazo kibao raia wanakufa njaa.!
 
1592922273032.png


Akichimba mtaro unaopeleka maji Chato Aiport
 
Ni porojo tu na political stunts za uchaguzi uchwara, wilaya ya Magu haina huduma za maji na imepakana na Ziwa Nyanza (Victoria)... itakuwa Dodoma..!!
Huu mradi unamiaka kama 10. Hapa maji yalishafika shinyanya. Mashine za kusukuma zikiwashwa kupeleka maji miswingwi tu hapo, unaaanza mgao wa maji mwanza.

Huu mradi JK aliufanikisha kwa 40% toka magu aingie umekwama.
 
Waaache kujadiliWaache kujadili upuuz
Wawafikilie kwanza watu wa mwnza, maji buhongwa yanatoka mara mbili kwa week na kutoka ziwan ni km 5 tu. Mwanza nzima ni 25% ndo wanapata huduma ya maji 24hr
Mkuu bohongwa mtaa wa sawa ya chini(semba) kuna mradi wa kusambaza maji buhongwa yote na maeneo mengine.wachina wapo site wanajenga pampu ya maji.
 
Sasa shauri yako na ujinga wako miaka hamsini unaishi ziwani ujawahi vua samaki wako mwenyewe
Mkuu bohongwa mtaa wa sawa ya chini(semba) kuna mradi wa kusambaza maji buhongwa yote na maeneo mengine.wachina wapo site wanajenga pampu ya maji.
 
Ni porojo tu na political stunts za uchaguzi uchwara, wilaya ya Magu haina huduma za maji na imepakana na Ziwa Nyanza (Victoria)... itakuwa Dodoma..!!
Acha kustaajabu kishabiki mkuu, mbona Tabora yamefika, kuna ugumu gani kuyaunganisha pale Igunga yakaingia Singida and then Dom?
 
Misri anataka lipua yale mabwawa ya Ethiopia
 
Wamisri wako macho na ziwa Victoria hatari.

Ziwa Tanganyika lina maji mengi zaidi ya ziwa Victoria, kwa nini kila mradi wa kusambaza maji serikali yetu inalifikiria ziwa Victoria pekee?

Kwa nini wasitumie maji ya ziwa Tanganyika?

Ziwa Nyasa vilevile.
 
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo amesema Wizara hiyo inatarajia kufanya utafiti mkubwa na usanifu wa mradi mkubwa wa maji wa kuchukua maji kutoka Ziwa Victoria kupeleka Mkoani Dodoma kwa kupitia Mkoani Singida katika mwaka wa fedha wa 2020/2021>>”hii itaondoa kabisa shida ya maji Dodoma na Singida”
•
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof.Kitila Mkumbo alitoa kauli hiyo kwenye hafla ya kupokea mabomba ya maji ambayo ni sehemu ya Programu kubwa inayotekelezwa kwa nchi nzima katika mikoa 17, Singida ikiwa ni moja ya Mikoa hiyo.
•
Mkumbo amesema fedha za mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kupeleka Dodoma kupitia Singida tayari zimetengwa katika bajeti ya mwaka huu wa fedha, hivyo anaamini kipindi cha miaka 5 ijayo Singida na Dodoma wanaweza kupata maji kutoka Ziwa Victoria.

Source; millard ayo
Mbona maji yako kibao Iringa/Mtera, si ingekuwa rahisi na karibu kuchukua huko?
 
Wamisri wako macho na ziwa Victoria hatari.

Ziwa Tanganyika lina maji mengi zaidi ya ziwa Victoria, kwa nini kila mradi wa kusambaza maji serikali yetu inalifikiria ziwa Victoria pekee?

Kwa nini wasitumie maji ya ziwa Tanganyika?

Ziwa Nyasa vilevile.
Mimi pia najiuliza hili jambo lake Tanganyika lingeweza kuhudumia kigoma, katavi, rukwa na Tabora.

Halafu ziwa Victoria wakaelekeza maji kwenye mikoa ya Geita, Simiyu, shinyanga, Mwanza na Mara ikiwezekana Singida ambayo asilimia kubwa ina ukame wa maji.
 
Back
Top Bottom