Kumekucha: Maji kutoka Ziwa Victoria mpaka Dodoma

Kumekucha: Maji kutoka Ziwa Victoria mpaka Dodoma

Afrika bado sana karne ya 21 hii bado tunadiscuss habari za maji
 
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo amesema Wizara hiyo inatarajia kufanya utafiti mkubwa na usanifu wa mradi mkubwa wa maji wa kuchukua maji kutoka Ziwa Victoria kupeleka Mkoani Dodoma kwa kupitia Mkoani Singida katika mwaka wa fedha wa 2020/2021>>”hii itaondoa kabisa shida ya maji Dodoma na Singida”
•
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof.Kitila Mkumbo alitoa kauli hiyo kwenye hafla ya kupokea mabomba ya maji ambayo ni sehemu ya Programu kubwa inayotekelezwa kwa nchi nzima katika mikoa 17, Singida ikiwa ni moja ya Mikoa hiyo.
•
Mkumbo amesema fedha za mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kupeleka Dodoma kupitia Singida tayari zimetengwa katika bajeti ya mwaka huu wa fedha, hivyo anaamini kipindi cha miaka 5 ijayo Singida na Dodoma wanaweza kupata maji kutoka Ziwa Victoria.

Source; millard ayo
Hiyo ni protoko ya siasa kavutia kwake hapo.
 
Juzi kwenye taarifa ya habari nimeona wananchi wa mara wanalalamika hawana maji wakati wapo karibu na ziwa inakuwaje maji yanapelekwa mbali wakati waliozungukwa na maji wanalalamika
Hiyo ni mbinu ya kujipigia kampeni kwa wananchi
 
Ni aibu sana kupeleka maji Dodoma wakati mwanza kwenyewe hapa Wanainchi hatuna maji , miundo mbinu ya maji hapa mwanza sehemu nyingi sana hazina maji
 
Acha kustaajabu kishabiki mkuu, mbona Tabora yamefika, kuna ugumu gani kuyaunganisha pale Igunga yakaingia Singida and then Dom?

Mzee mi nimeongelea Magu haina maji, huenda sio kipaombele chao... tumezoea kujichotea maji ziwani kwa baiskeli na tolori.

Kama mradi huu umefika Tabora, mbona hii taarifa haisemi kuwa wanatoa Tabora kuelekea Dodoma.?
 
Endapo Jambo Hili Litafanikiwa Hakika Ndugu Zangu Dodoma
Kutumia Maji Ya Visima Toka Mzakwe Itabaki Story
Huu Mradi Ulikuwa Unasemwa Zamani Sana


Dodoma Pia Tutachimba Mtaro Wa Maji Bahari Toka Dar es salaam Yaende Dodoma
Naunga mkono hoja ya mtaro wa maji bahari hadi dodoma. Faida ni nyingi kubwa zaidi wakazi wa dodoma watafaidi samaki wa maji chumvi. Nani kama CCM? CCM oyee.
 
Tatizo matumizi ya ya hayo maji. Egypt wanatumia maji ya mto Nile ambao chanzo chake ni ziwa Victoria na wao chanzo hicho ni zaidi ya 90% ya maji wanayotumia. Sasa unashangaa Mara?
... tuweke rekodi sawa; L. Victoria contribution to the Nile through White Nile is not more than 15%. The main source of the Nile waters beyond Khartoum is Blue Nile (originationg from Ethiopia) which contributes about 85%. Blue Nile waters usage has been a matter of dispute between Egypt and Ethiopia.
 
Wakumbushe tu kuwa wenzetu husimamia mikataba pale Mwanza kuna wamsiri kabisa na ofisi zao kwa ajili ya kutoa ripoti kwa serikali yao kile kinachoendelea pale ziwa Nyanza
Ni mikataba ya kikoloni hatukushirikishwa, na ilitengenezwa kwa maslahi yao wakoloni.
 
Wakumbushe tu kuwa wenzetu husimamia mikataba pale Mwanza kuna wamsiri kabisa na ofisi zao kwa ajili ya kutoa ripoti kwa serikali yao kile kinachoendelea pale ziwa Nyanza
Samahani Mkuu

Huo mkataba wa Masr na Tanzania kuhusu Ziwa Nyanza unahusu nini?
 
Wakuu kivipi misri anaweza kutuzuia kuvuna maji ya ziwa victori
Kuna mikataba ilisainiwa kipindi cha mkoloni, lakini haikuwashirikisha wazawa au wanufika wa maeneo husika, kama unavyojua ilikua kipindi cha ukoloni, sasa baadae Ethiopia hatambui huo mkataba kajenga bwawa kubwa la umeme, ugomvi mpya ni namna ya kulijaza, kwa tafiti inasemekana litajaa kwa kipindi cha miaka 3 mpaka 7, sasa huu muda ndio unaumiza kichwa wamisri kwasababu source kubwa ya maji ya mto nile yanatoka Ethiopia, muda wa kulijaza wanatarijia flow ya maji kwenye mto itaathiriwa pakubwa na hivyo kuwaumiza wamisri.

Misri anataka kutumia mkataba wa mkoloni, Ethiopia hautambui kwasababu hakushirikishwa kwa chochote, na pia chanzo cha maji kinatoka nchini kwake.

Kipindi cha Morsi aliwapiga mkwara Ethiopia kwamba wapo radhi kumwaga damu kulinda maji.

(Hapo nimeongelea zaidi Ethiopia kwasababu ndio chanzo kikubwa cha maji ya mto Nile)
 
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo amesema Wizara hiyo inatarajia kufanya utafiti mkubwa na usanifu wa mradi mkubwa wa maji wa kuchukua maji kutoka Ziwa Victoria kupeleka Mkoani Dodoma kwa kupitia Mkoani Singida katika mwaka wa fedha wa 2020/2021>>”hii itaondoa kabisa shida ya maji Dodoma na Singida”
•
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof.Kitila Mkumbo alitoa kauli hiyo kwenye hafla ya kupokea mabomba ya maji ambayo ni sehemu ya Programu kubwa inayotekelezwa kwa nchi nzima katika mikoa 17, Singida ikiwa ni moja ya Mikoa hiyo.
•
Mkumbo amesema fedha za mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kupeleka Dodoma kupitia Singida tayari zimetengwa katika bajeti ya mwaka huu wa fedha, hivyo anaamini kipindi cha miaka 5 ijayo Singida na Dodoma wanaweza kupata maji kutoka Ziwa Victoria.

Source; millard ayo

What a wonderful idea!! Maji ya mito Kagera, Transzoia na Yala yanatiririkia ziwa Victoria na wa Tz watayatumia kikamilifu kwa kuhudumia wana nchi wa Singida na Dodoma. Lakini tuwe makini kwani Wa Misri watatupeleka mahakamani kwa kukudumia wananchi wetu! Wahabeshi(Ethiopians) wameshitakiwa na Egyptians kwa kutumia maji ya Ethiopia kujenga bwawa la umeme!
 
Kuna mikataba ilisainiwa kipindi cha mkoloni, lakini haikuwashirikisha wazawa au wanufika wa maeneo husika, kama unavyojua ilikua kipindi cha ukoloni, sasa baadae Ethiopia hatambui huo mkataba kajenga bwawa kubwa la umeme, ugomvi mpya ni namna ya kulijaza, kwa tafiti inasemekana litajaa kwa kipindi cha miaka 3 mpaka 7, sasa huu muda ndio unaumiza kichwa wamisri kwasababu source kubwa ya maji ya mto nile yanatoka Ethiopia, muda wa kulijaza wanatarijia flow ya maji kwenye mto itaathiriwa pakubwa na hivyo kuwaumiza wamisri.

Misri anataka kutumia mkataba wa mkoloni, Ethiopia hautambui kwasababu hakushirikishwa kwa chochote, na pia chanzo cha maji kinatoka nchini kwake.

Kipindi cha Morsi aliwapiga mkwara Ethiopia kwamba wapo radhi kumwaga damu kulinda maji.

(Hapo nimeongelea zaidi Ethiopia kwasababu ndio chanzo kikubwa cha maji ya mto Nile)
Asante mkuu!
Nataka kujua kama huo mkataba unaizuia Tanzania kujenga bwawa la kuwahudumia wananchi wake?
Na je Misri ndo anamaamuzi ya juu zaidi kuliko Nchi zingine juu ya miradi ya kuchukua maji ya ziwa victoria.
Vipi kuhusu huo mkataba hauwezi kuvunjwa?
NB; ni kuelimishana tu mkuu
 
Uchaguzi uchaguzi....karopoka tu!

Everyday is Saturday......................... 😎
 
Tatizo matumizi ya ya hayo maji. Egypt wanatumia maji ya mto Nile ambao chanzo chake ni ziwa Victoria na wao chanzo hicho ni zaidi ya 90% ya maji wanayotumia. Sasa unashangaa Mara?
Why should we care about Egypt??
Uzalendo wa kweli ni watanzania kupata maji, hiyo mikataba ya Waingereza na kina Chief Mangungo na Wamisri, haituhusu!

Everyday is Saturday........................😎
 
Kama Bahari kwa zone ya Dar ingekuwa Maji baridi wana dar wote wangewezea kufuata huko baharini ?

Ni fursa hizo kwa vijana, piga kazi kuuzia maji hao wavivu.... mnalialia ajira bado mletewe maji hadi ndani.!
 
Back
Top Bottom