Kumekucha: Mchambuzi wa Michezo anayekuja kwa kasi nchini George Ambangile wa Wasafi FM asema Ukweli huu Mchungu

Kumekucha: Mchambuzi wa Michezo anayekuja kwa kasi nchini George Ambangile wa Wasafi FM asema Ukweli huu Mchungu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
" Kwa Kikosi hiki cha Simba SC kilichoishia hatua ya Robo Fainali juzi na jinsi kilivyo Imara na Wachezaji mahiri hakuna Mchezaji yoyote wa Yanga SC hii ya sasa anayeweza si tu Kucheza bali hata Kuanzia Benchi "

Ushahidi Kamili wa Kauli yake hii ipo YouTube Kipindi cha Sports Arena cha Wasafi FM ambapo aliulizwa Swali na Mtangazaji Msomi kuliko wote katika Kipindi chao hicho Ahmed Abdallah ambaye pia ni Mshabiki wa Timu Bora, Bingwa, Iliyobarikiwa na mahiri ya Simba SC.

Na kwa wale ambao mtaanza Kumchukia Mchambuzi huyu George Ambangile huku mkimnunia pia kaeni mkijua kuwa ni Mshabiki lia lia (Kindakindaki) kabisa wa Yanga SC ila kwa hili ameamua kuwa Mkweli ambao utamuweka Huru hapa duniani na Mbinguni pia.

Naona leo kuna Watu wamepiga Bomu Mochwari ya Mwadui Shinyanga na wanajisifu Kuua mara Mbili tu wakati huenda Yeye tarehe 3 July, 2021 akakumbana na Bomu la kweli kweli ambalo litamuua kama si Mara Saba basi mara Tisa kabisa kwa Mkapa Temeke.

Tafadhalini George Ambangile alindwe.
 
Mbumbu mme wako! Yaani haya mashabiki ya nyoronyoro fc hayapendi kuambiwa ukweli, hawajakimbia kipigo, bali wamejiwekea kiporo chamaumivi pengine makali zaidi kuliko kung'olewa meno bila ganzi! Kwa simba ile, ikiamua kucheza kama vile, kwama beki nyoronyoro kama ninja vile, naziona 7 au 9 kama mkuu gentamycine anavyosema hiyo july 3.
 
Ukitazama kwa makini, utagundua kuwa hapa nchini hatuna wachambuzi wa soka bali kuna watu wanaokaa kwenye vituo vya redio wakizungumizia soka, kuna tofauti kubwa kuongelea soka na kulichambua soka.
 
Ambangile huwa nampenda kwa ukweli wake tu hanaga utimu kwenye ukweli. Jamaa yuko tofauti sana wachambuzi wengine pengine hii ndio inamfanya kuwa tofauti na wengine.
 
Ukitazama kwa makini, utagundua kuwa hapa nchini hatuna wachambuzi wa soka bali kuna watu wanaokaa kwenye vituo vya redio wakizungumizia soka......kuna tofauti kubwa kuongelea soka na kulichambua soka........
Mzee hao wachambuzi sio kila muda wanachambua kuna muda wanaongelea
 
Simba hakuna holding midfield kama Mukoko.
Huwezi mfananisha babu wawa na Mwamnyeto hata dogo Job.
Kisinda anamkalisha Morrison.
Metacha bench la simba anamuondoa Kakolanya.
Yacouba ni mchezaji Bora kuliko Mugalu au Bwalya they are hopeless basi tu wanabebwa na Chama na Miquessone.



Bwalya, Mugalu
 
Ukitazama kwa makini, utagundua kuwa hapa nchini hatuna wachambuzi wa soka bali kuna watu wanaokaa kwenye vituo vya redio wakizungumizia soka......kuna tofauti kubwa kuongelea soka na kulichambua soka........
Angeisifia Yanga SC yangekutoka haya?
 
Back
Top Bottom