Kumekucha salama! Karibuni kwa sala ya asubuhi, tumshukuru Mungu

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Mungu Baba, umetuagiza katika 1 Thes 5:18 kwamba tushukuru kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi yako kwetu katika Kristo Yesu.

Tunakushukuru sasa Baba kwa kutulinda usiku kucha. Tumelala usingizi mnono na kuamka tukiwa na nguvu na uzima. Asante sana Baba kwa neema yako.

Endelea kutulinda tena leo Baba. Tunaoenda kanisani kukuabudu, uwe nasi njiani. Wanaosafiri mbali na karibu, uwaepushe na ajali. Wanaoteseka kwa magonjwa hospitali, mkono wako uwaguse na kuwaponya katika Jina la Yesu. Wakumbuke wasiokuamini, uwavute kwako leo. Asante Mungu kwakuwa utatubariki tena leo, katika Jina la Yesu Kristo, Amen.
 
Amen.
 
Back
Top Bottom