Kumekucha: Wakili msomi Peter Kibatala na Tundu Lissu kumtetea Ney wa Mitego mahakamani

Kumekucha: Wakili msomi Peter Kibatala na Tundu Lissu kumtetea Ney wa Mitego mahakamani

Wahuni tu kutafuta kick, vitu vya maslah kwa wengi huwaoni ila issue za akina wema sepegu utawaona! Lisu sio wa kujifanya anajua kutetea wanyonge ilihal vijana wanagongwa 18% loan bodi huko, angekuwa mkweli angeonekana bt ni wauza sura
Kwani anaeenda kumtetea nay ni lisu au kibatala?
 
Chadema sasa ni Chama cha kutetea wahalifu mwisho kitakuwa Chama cha magaidi dawa ni kukifuta kama vile MUSLIM BROTHERHOOD
 
Kwako mambo ya kijinga ni yapi?! WaTz wawe huru kuwaonyesha watawala mapungufu yao. Na nikuambie hata siku moja watu hawawezi kufanana mawazo .
Usingekuwa huru usingejieleza hata kwenye jukwaa hili!uhuru bila mipaka haukuabaliki hata kanisani/msikitini!nyumbani kwako kunamipaka pia!
 
Chadema sasa ni Chama cha kutetea wahalifu mwisho kitakuwa Chama cha magaidi dawa ni kukifuta kama vile MUSLIM BROTHERHOOD
kama ilivyo ccm inavyomtetea bashite zero......yaani fa fa fa fa fa fa.....
 
Wahuni tu kutafuta kick, vitu vya maslah kwa wengi huwaoni ila issue za akina wema sepegu utawaona! Lisu sio wa kujifanya anajua kutetea wanyonge ilihal vijana wanagongwa 18% loan bodi huko, angekuwa mkweli angeonekana bt ni wauza sura
Loan bodi ya wapi hiyo inagonga 0.18 au ya koromije ????? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Polisi wa Tanzania bhana:
1.Video ya uvamiz wa RC wa Dsm katika kituo cha Clouds Media hawakuiona
2. Video ya askari aliyemtishia bunduki Mh. Nape Nauye ilhali akiwa hana silaha na mikono kaweka mfukoni pia hawakuiona
3. Ila wimbo wa Ney wa Mitego wameusikiaa na wameshamkamata....
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Karibu sana nchini
 
Malaika mdogo akamwambia baba yake malaika mkuu sweka ndani ilo li sanii limeniimba akajibu mwanangu sema chochote nitatii wewe ndio remote yangu final say.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
KESI YA UCHOCHEZI YA NEY WA MITEGO NA WIMBO WAKE MPYA WAPO

NA
,Mdude nyagali

WAKILI; unasema wewe ni afisa wa polisi ney wa mitego alifanya uchochezi kwenye nyimbo yake na baadhi ya maneno yaliyopo kwenye hati ya mashtaka yameandikwa kichaa kapewa rungu hebu iambie mahakama kichaa aliyemsema ney ni yupi?

SHAHIDI PC;;kichaa aliyemsema ney ni mtukufu

WAKILI;;ifafanulie vizuri mahakama wewe ulijuaje kama kichaa aliyeimbwa na ney ni mtukufu?

SHAHIDI PC.;mimi nilihisi kuwa atakuwa mtukufu kwa kuwa ney ni timu ukawa;

WAKILI;;shahidi hivi unafahamu kuwa ushahidi wa kuhisi na kupiga ramli mahakamani haupo kwa kuwa sio kwa mganga wa kienyeji na haupo kwenye sheria yoyote?

SHAHIDI PC;;ndiyo

WAKILI;;Sasa ebu iambie mahakama bila kuhisi huyu kichaa kapewa rungu aliyemuimba ney ulijuaje ni mtukufu?

SHAHIDI PC;;kimya

WAKILI;kuna maneno mengine unayakumbuka ambayo ni ya kichochezi na yapo kwenye wimbo wa ney?

SHAHIDI PC;ndiyo
WAKILI;;unaweza kuyataja?
SHAHIDI PC;;1,kuna watu hawana malinda,,2.daudi bashite kavoji vyeti,,,3.hutaki ushauri unajifanya ndugu yake yesu

WAKILI;kwa hiyo watu kutokuwa na malinda ni uchochezi?
SHAHIDI PC;ndiyo
WAKILI;ebu iambie mahakama nini maana ya kutokuwa na malinda?

SHAHIDI PC;;kimya

WAKILI ;;jibu mheshimiwa HAKIMU anasubili a note jibu lako

SHAHIDI;;sijui ila nilisikia bungeni mbunge wa mbeya mjini mheshimiwa mbilinyi akiongea kuwa gavana akaguliwe malinda.

WAKILI ;je wewe una hiyo malinda?
SHAHIDI PC;sina na siijui

WAKILI;;Kwa upelezi wako kama afisa wa polisi ulijua ney wa mitego anamsema nani ambaye hana malinda?

SHAHIDI PC;katika kufanya upelelezi tukishilikiana na ofisi ya OCCID na ofisi ya RCO tuligundua ney alikuwa anamsema gavana wa mkoa wetu kuwa ndiye hana malinda

WAKILI;wewe ulijuaje kama ney anamsema gavana huenda alikuwa anakusema wewe na wewe si umesema hapa na mahakama ime note kuwa huna malinda?

SHAHIDI PC;hapana sio mimi ni gavana

WAKILI;;;Kwani kuna mstari wowote wa huo wimbo gavana ametajwa?

SHAHIDI PC;;hapana ila ametajwa kwa jina la daudi bashite;

WAKILI;;;kwani gavana alishawahi kusibitisha popote au kanisani ama kiapo cha mahakama kuwa jina la daudi bashite ni lake?

SHAHIDI PC;;sijui ila naona kwenye mitandao watu wanamuita hivyo.

WAKILI;;huko kwenye mitandao ni akina nani wanamuita hivyo?

SHAHIDI PC;akina Mdude Chadema Nyagali, Malisa GJ, Daniel Ezekiel Daniel Kumbusho Dawson Kagine Michael Mwaikenda Boniface Mwabukusi Yericko Nyerere Bob Chacha Wangwe Boniface Jacob Julius S. Mtatiro mange kimambi Tanzagiza Hilda Newton Chadema Karama Kaila na wengine wengi

WAKILI;;je unaweza kumleta gavana ili aje aisibitishie mahakama kuwa yeye ndiye bashite halafu ndio tuendelee na tafsiri ya neno malinda?

SHAHIDI PC.;itakuwa ngumu mheshimiwa kumleta gavana.

WAKILI;;unafahabu kwa mujibu wa sheria usipo mleta gavana kuthibitisha kuwa yeye ndiye daudi bashite ushahidi wako kuhusiana na malinda unakosa uhalali mbele ya mahakama tukufu?

SHAHIDI PC;kimyaaa

WAKILI;unafahamu kuwa kwa mujibu wa katiba serikali yetu haina dini ila wananchi wake ndio wana dini?

SHAHIDI PC;;ndiyo

WAKILI;;unakubaliana na mimi kuwa kwa mwongozo huo wa katiba ili uwe na undugu na yesu ni lazima uwe myahudi au muisrael?

SHAHIDI;;Ndiyo

WAKILI ;;sasa haya maneno unayosema ni ya uchochezi kwenye wimbo wake kuwa hashauliki ana undugu na yesu ulijua ney anamsema ni nani?

SHAHIDI;;ney alikuwa anamsema ni mtukufu kwa kuwa wapinzani hulalamika kuwa mtukufu hashauriki.

WAKILI;;kwani mtukufu ni muyahudi?au ana vitambulisho vyovyote vinavyoonyesha ni muisrael ama viashilia vinavyoonyesha ana undugu na yesu?

SHAHIDI;;kimyaaa

NINGEKUWA WAKILI MIMI HAKIKA KESI YA NEY NINGEJITOLEA KUISIMAMIA BURE.
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
hahahaha Nay ndicho alicho taka na sasa kafanikiwa...alitaka kuonana na wakina Lissu na Kibatala kupitia kiki ya matusi na watetezi wamejitokeza
Vipi hapo mkuu, kesi ipo au zuga zuga time?
 
well done!,wasipotokea akina ney JE ni nani atatusemea?...
•how can you prove kama mistari ya muziki imegusa mtu yeyote?
•HAKUNA KITU KIBAYA KAMA KUJISHUKU...!
na unaweza kosa usingizi kwa kujishuku...ila sijapata bahati ya kuusikiliza huu wimbo. Nijue kilichopo ndani yake
 
Ney katumia fasihi tu hajataja jina lolote la kiongozi na hakuna neno la kashfa lolote alilolitaja kwenye wimbo wake, anayetakiwa kukamatwa na kushtakiwa ni yule anayejihisi ameimbiwa yeye. Huwezi kumfunga mtu kwa kutoa mawazo yako kichwani na kutafsiri. Labda kama mahakama itathibitisha pasipo na shaka kuwa kiongozi fulani hapendi kushauriwa, au kiongozi fulani ni kweli amepoteza marinda hivyo kuimbwa ni kumdhalilisha, au Bashite wa kolomije ni jina halali kisheria la kiongozi fulani,
Ndipo watakapotueleza Daudi Bashite ni nani! pia wasanii huwa wanaimba matukio yaliyopo, yaliyowata hata ya kufikirika , yeye kaimba matukio ya kufikirika hajataja mtu, inawezekana ni maono aliyoana kuwa anaweza akatokea mtu wa aina hiyo.
 
Marinda ni mikunjo ambayo hufanywa kuelekea ndani ya nguo..
Mfano: Nguo ya bibi yangu ina marinda mengi.

Na mimi mtangazaji wako Honi sigara kutoka baraza la Kiswahili[emoji1][emoji1][emoji1]
 
Back
Top Bottom