Kumekuwa na wimbi la wauza maziwa mitaani na barabarani, Je maziwa hayo ni salama?

Mtindi wao huwa ni mzito kweli kweli,nambari wani.
Siri ya mtindi kuwa mzito, kwanza anza wewe kuyachunguza kwa kuyaacha yalale siku tatu, utakuta yamegawanyika maratatu chini kitu kama maziwa hiki hufanya yawe mazito, kinafuatia maji na juu kabisa maziwa ya mtindi, yanakuwa juu kwa sababu ni mepesi.
Hiki sasa ndicho hufanyika kuyaboresha, unga wa ngano hukorogwa kwenye maji kisha huchemshwa na kuacha uji huo mwepesi upowe, ukishapoa huchanganywa na mtindi na kukorogwa muda wote, mnunuzi anaponunua huuona mtindi mzito.
Kwanini hukorogwa muda wote, jibu lipo juu.
 
Sio singida tu, hata huku mkoa niliopo kanda ya ziwa wapo wanaochanganyia na maji, mengine yanakua na harufu mbaya sana.

Sijui kwanini wanatufanyia hivyo, matumbo yanauma wao hawajali.
 
Umeweka Picha ya Punda? Ili kutishia wasio kuwa na uelewa?
.
Sikiliza kwanza maziwa ya punda ndio maziwa Bora miongoni mwa maziwa yote, ukiondoa maziwa ya Mama, maziwa yanayo fuatia ni ya punda, watalamu wanasema yako sawa kabisa na maziwa ya binadamu kwa ubora.

Cleopatra malikia wa Egypt inaaminika alikuwa anaogea maziwa ya Punda enzi hizo.

Maziwa ya punda ni ghari sana,
 
Kiafya, hupaswi kununua raw milk mtaani, nchi nyingi zishapiga marufuku huu ujinga, ni nchi chache za Afrika ndio kuna huu ujinga.

Raw milk ni hatari sana na Serikali inajua sana hilo ila kwasababu wao hawatumii wanawaacha mufe
 
Ina maana unga wa ngano ni bei rahisi, mpaka mnachanganya na maziwa kisha kupata faida
 
Kunywa ASAS mkuu...

Maziwa mengi ya mtaani janja janja nyingi.

Uuzaji wa maziwa unastahili usafi wa hali ya juu,

Lakini maeneo mengi ya Dar usafi hawazingatii, ukiona ndoo za wale wamama wanaokuja ubungo kuchukua maziwa kwenda kuuza huko mtaani ni uchafu tupu...
 
Usinunue hayo maziwa kama mchuuzi hana leseni kutoka mamlaka husika, hususan Bodi ya maziwa!
 
Ina maana unga wa ngano ni bei rahisi, mpaka mnachanganya na maziwa kisha kupata faida
Wanaweka kiasi kidogo sana kutengeneza uji mwepesi, mbona wengine wanatengenezea gundi ya kutengeneza mifuko ya karatasi.
Nunua kisha fanya nilichokisema utaona nilichokielezea, ngano itajikusanya chini na maziwa yataelea juu huku maji yakiwa katikati.
 
Hao CHAWAKIM na TREASURE nilishawahi kununua maziwa kwao kipindi nipo Dar... Top class maziwa, huwa sinunui tofauti na hapo.. mtaani " i got trust issues"
 
Miaka nenda rudi wauza maziwa mitaani wamekuwa wakiuza
Ehe,vp tuachane nao na tuwe tunanunua maziwa ya kina asas na wengineo tu

Ova
 
Ni maziwa halisi kabisa tena mazuri kunywa Wala usiwe na hofu
Ni utajiri TU wa watanzania ndio unafanya kuchagua chagua vitu ila maziwa ya mbuzi ni mazuri ya ngamia ya ngombe n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…