Kumfanyisha Interview Medical Doctor aliyethibitishwa na Baraza la Madaktari (MCT) ni dharau kubwa sana

hakuna cha usenge wala nini ndiyo kawaida ufanyiwe interview ili kieleweke kama wewe uko vizuri kuliko yule mwenzako aliyeachwa.

Sasa kama muko 1000 na nafasi zilizoko ni 30 unadani mchujo utapita vipi hapo bila interview?
Mtu akishapata leseni ya udaktari tayari yuko vizuri.
 
Katika udaktari muda uliosoma ni moja ya qualification, Marekani madaktari wanasoma miaka nane ya chuo ndio maana madaktari wa Africa wakifika huko inabidi warudi tena shule pamoja na kufanyishwa mitihani mingi ili waweze kuajirika.
 
umepiga kwenye mshono😂😂😂😂
 
Haijalishi amepata izo one nk. Lakini usaili ni muhimu sana kabla ya kupata kazi kwasababu vipo vitu vingi vinavyo angaliwa zaidi ya izo one na masomo
Kwenye udaktari suala muhimu ni ufaulu tu na leseni, haya mengine ya interview ni njia ya kupunguza watu kwa sababu ya ufinyu wa ajira.
 
Kuna watu hawachuji kwa kuangalia vyeti na historia ya umwpitia wapi, wanachuja kwa kuangakia attitude ya mtu.

Usiwanyime haki yao ya kuchuja wanavyotaka.
Kama ni hivyo wangekuwa wanafanyiwa psychology tests tu, pia hii ingewafaa zaidi viongozi, wabunge, polisi, Rais n.k. Interviews kwa madaktari ni janjajanja ya kupunguza watu kwa sababu ya ufinyu wa ajira.
 
Kuna wajomba wana A kibao kwenye cheti ukimhoji ndio unajiuliza alitoa wapi hizi A
 
Wewe uko sahihi, hizo interviews kwa madaktari hazipimi chochote cha maana, ni njia ya kupunguza watu tu.
 
Unaongea wewe,mimi ndio mwenye hospitali,unataka nifate utakacho wewe?

Kwahiyo A ndio amri ya kutuamrisha wenye taasisi kwa lazima tukuajiri?

Una A lakini jambazi na evil,nikuajiri kwenye taasisi yangu kivipi yaani?

Mali yangu,unataka uje kuniletea ulazima eti ulipata A?

Fungua taasisi yako utafanya utakalo,who cares!
 
Sasa hivi fani nyingi zina mabaraza ya kuwathibitisha na kuwasajili.
Sasa kwa namna hiyo tuziondoe interview zote au ?
Wahasibu, Wahandisi , Wagavi, wagani n.k wana mabodi yao .
Acheni ujinga
Wahasibu, wagavi na Wagani ni kazi za social sciences/ngwini ambazo zinahusisha siasa, majungu, fitna na janjajanja za hapa na pale tofauti na kazi za pure science kama Wahandisi, madaktari, nk.
 
One may be good at answering selected number of questions, ila iki fika ku relate katika fani husika ni majanga mazito.

So acha wawa chuje, huenda Waka pata watu makini.
SI una elewa Kuna watu ni mabingwa wa kununua vyeti??.
Sio kwenye udaktari, mtu yeyote mwenye leseni ya udaktari hawezi kuwa majanga hata kidogo, anachoweza kukosa na experience kubwa tu, lakini akipata nafasi atazidi kuwa bora zaidi kadri muda unavyokwenda.
 
Kama ni hivyo wangekuwa wanafanyiwa psychology tests tu, pia hii ingewafaa zaidi viongozi, wabunge, polisi, Rais n.k. Interviews kwa madaktari ni janjajanja ya kupunguza watu kwa sababu ya ufinyu wa ajira.
Wenye kutoa kazi ndio wanaoweka vigezo.

Na wewe unaweza kuanzisha ajira zako na kuweka vigezo vyako.
 
Tutajie hizo taasisi za Feza zinazochukua walimu bila interview ?
 
Hivi unaweza kuajiriwa popote bila interview? Nchi hii tuna shida sana na uwezo wa watu kufikiri.
 
Wenye kutoa kazi ndio wanaoweka vigezo.

Na wewe unaweza kuanzisha ajira zako na kuweka vigezo vyako.
Sijapinga wenye kutoa kazi ndio wanaoweka hivyo vigezo, ninachosema hivyo vigezo kwa fani ya udaktari havina mashiko,
 
Mkuu a Doctor is a Healer kuna jinsi ya kumwambia mgonjwa ili a feel good huwezi kuja unamwambia mgonjwa ana ukimwi au cancer au ana siku tatu za kuishi huku unavuta fegi na kuchekelea au unatangazia watu bar kwamba fulani ana gono....

Ngoja nikupe Qoute from Person of Interest huenda ikakuonyesha what I mean....

Sameen Shaw: I watch the others. I watch the fear creep into them. I watch them make mistakes, and you think these feelings that I'm lacking make them better? You'd really rather have one of them working on you instead of me?
QMI Manager: Yes. Because if If the only thing motivating you is technical mastery, when one of your patients needs you the most, then this job just might start to bore you. That's the difference between fixing and healing. You have a brilliant mind, Sameen. And you're very gifted. But you'll never be a doctor.
 
Sijapinga wenye kutoa kazi ndio wanaoweka hivyo vigezo, ninachosema hivyo vigezo kwa fani ya udaktari havina mashiko,
Vina mashiko kwa sababu wao ndo wanajua wanahitaj daktari wa aina gani
 
Chief, sipingi usaili ila naomba nikuswalike swali

Hivi lengo la usaili ni kuchuja idadi au ubora?

Kama ni idadi vipi mtihani wakifaulu wote watatumia kigezo gani kingine kupata hao 20 out of 200
Lengo la interviews za udaktari ni kuchuja idadi tu sio ubora, kama ni ubora wangeangalia ufaulu wa darasani, hilo ndilo jambo muhimu zaidi kwa daktari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…