Hypersonic WMD
JF-Expert Member
- Apr 11, 2024
- 1,337
- 1,876
basi usifanyeJust imagine kijana kapata division one ya 7 au 10 form four kaenda high school kupiga PCB. Kapambana sana kachakaa kajitesa kajinyima kapata division one form six ya point tatu au tano.
Kaaply Muhimbili University kapitia mchujo katoboa akaanza masomo ya udaktari.
Kasoma miaka mitano bila kudisco tena kwa mateso makubwa bila kula bata mpaka kamaliza chuo.
Kabla hajaingia intern kafanyishwa mtihani wa MEDICAL COUNCIL OF TANGANYIKA katoboa kaanza interniship.
Kapiga intern kwa mwaka mmoja kisha kamaliza kisha kapigishwa pepa lingine la MCT katoboa.
Kasajiliwa na kutambulika kama MEDICAL DOCTOR na MCT.
Kijana huyu wa kitanzania aliyesoma kwa kujinyima na kujitesa tangu kidato cha kwanza leo hii anafanyishwa interview tena written interview sio prectical interview ili iweje?
Huyu kijana akikosa nafasi mnajua stress atakazopata mtaani na jamii inayomzunguka?
Hiyo michujo yote alopitia akipata ajira mnamlipa milioni moja na laki mbili ukitoa makato anabeba laki tisa bado mnampigisha interview ya nini sasa?
Hamuoni kama mnakatisha tamaa vijana waliopo shuleni na vyuoni?
Wadau