Kumficha Baba wa Mtoto lila ugomvi ni uamuzi sahihi au la?

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
22,235
Reaction score
51,111
Hivi kuna madhara yoyote mwanamke akishika ujauzito na kuamua kumficha mwanaume bila kuwa na ugomvi au tatizo lolote kati yao, kwa lengo la kumlea mtoto peke yake?

Pia, ikiwa mwanaume huyo hatakuja kufahamu maisha yake yote kwamba ana mtoto na mwanamke huyo, je, kuna kosa lolote kwa mwanamke kufanya hivyo ili mtoto awe wake peke yake?

ShesRise_1 🖐
 
Tatizo lipo ShesRise_1 linaanzia pale unapolala na mtu na kupata mimba yake alafu ukamficha kwanza hilo ni kosa sababu ni kuwa umehujumu jitihada zake za kukupa mimba .

Ila mbaya zaidi ni ukatili wa hali juu kwa kile kiumbe tarajiwa ,sababu muda ukifika atahitaji kumuoana baba yake ,kumdanganya au kumfichq baba yake ni ukatili wa kihisia ,hali ambayo sidhani unaweza kuishi na amani moyoni wala maishani mwako .

Ila kuna machaguo ya namna hii ,unaweza kuzungumza na mtu kuwa tuzalishane ila nahitaji kulea mwenyewe wapo wanaume wapo tayari kwa hilo isipokuwa ile kutambulishwa kwa mwanaye hilo jambo linakuja kufanyaika ijapokuwa baba mtu hakuhusika kwenye malezi .

Kwahivyo nahitimisha kwa kusema inawezekana japo sio sahihi na haifai maana haiko sawa kisheria na kimaadili .
 
Hakuna kosa hata kidogo.Ni vema wanawake wote,hasa ambao hawajaolewa wakahamasishana hilo.Litawasaidia Sana maishani.
NB:1-Asitokee mtu akaanza kulialia baadaye.
2-Ni kweli kabisa haujui majibu ya maswali yako?
 
Hapo mimi ntasema haifai kumficha coz ipo cku yote yatahitajika uyaweke wazi aidha kutoka kwa mtoto au huyo mtu anayemlea. Ni bora uweke wazi wachague kusuka au kunyoa.
 
Hivi kuna madhara yoyote mwanamke akishika ujauzito na kuamua kumficha mwanaume bila kuwa na ugomvi au tatizo lolote kati yao, kwa lengo la kumlea mtoto peke yake?

Pia, ikiwa mwanaume huyo hatakuja kufahamu maisha yake yote kwamba ana mtoto na mwanamke huyo, je, kuna kosa lolote kwa mwanamke kufanya hivyo ili mtoto awe wake peke yake?

ShesRise_1 🖐
Ni sawa na kusogeza matatizo mbele.
 
Tatizo lipo ShesRise_1 linaanzia pale unapolala na mtu na kupata mimba yake alafu ukamficha kwanza hilo ni kosa sababu ni kuwa umehujumu jitihada zake za kukupa mimba .
Sawa sawa
Ila mbaya zaidi ni ukatili wa hali juu kwa kile kiumbe tarajiwa ,sababu muda ukifika atahitaji kumuoana baba yake ,kumdanganya au kumfichq baba yake ni ukatili wa kihisia ,hali ambayo sidhani unaweza kuishi na amani moyoni wala maishani mwako .
Ahaa sawa
Ila kuna machaguo ya namna hii ,unaweza kuzungumza na mtu kuwa tuzalishane ila nahitaji kulea mwenyewe wapo wanaume wapo tayari kwa hilo isipokuwa ile kutambulishwa kwa mwanaye hilo jambo linakuja kufanyaika ijapokuwa baba mtu hakuhusika kwenye malezi .
Mnaweza kuzungumza vizuri baadae akaanza kuleta shobo ooh nipe na mimi mtoto nikae nae migogoro inaanzia hapo
Kwahivyo nahitimisha kwa kusema inawezekana japo sio sahihi na haifai maana haiko sawa kisheria na kimaadili .
Mi sioni tatizo kubwa
 
Hakuna kosa hata kidogo.Ni vema wanawake wote,hasa ambao hawajaolewa wakahamasishana hilo.Litawasaidia Sana maishani.
NB:1-Asitokee mtu akaanza kulialia baadaye.
2-Ni kweli kabisa haujui majibu ya maswali yako?
Kulia lia nini ?
Kwamba mtoto bila baba hakui mnajipa umuhimu sana aisee

Je baba akifa mtoto haishi
 
Back
Top Bottom