Kumficha Baba wa Mtoto lila ugomvi ni uamuzi sahihi au la?

Kumficha Baba wa Mtoto lila ugomvi ni uamuzi sahihi au la?

Ndiyo, kuna madhara makubwa na ni kosa kisheria na kisaikolojia kumficha mwanaume ujauzito na mtoto kwa makusudi, kwani sheria ya mtoto ya Tanzania ya mwaka 2009 inatamka wazi kuwa mtoto ana haki ya kimsingi ya kuwajua na kulelewa na wazazi wake wote wawili.

Kumnyima mtoto utambulisho wa baba yake ni ukiukwaji wa haki zake za kisheria, jambo linaloweza kuibua migogoro mikubwa ya kisheria na ustawi wa jamii hapo baadaye ikiwa siri hiyo itafichuka.Kisaikolojia, uamuzi huu unamjengea mtoto mgogoro mkubwa wa utambulisho wakati wa kukua, ambapo atakosa majibu ya nani baba yake mzazi na kusababisha upweke au kupungua kwa kujiamini.

Aidha, ikiwa mtoto atagundua ukweli huu ukubwani—kupitia ndugu au vipimo vya vinasaba (DNA)—kuna hatari kubwa ya yeye kujenga chuki na hisia za kusalitiwa dhidi yako kwa kumnyima fursa ya kuwa na baba yake maishani.Kibaolojia na kitiba, hatua hii inamweka mtoto katika hatari ya kukosa msaada wa haraka wa kitabibu pale inapohitajika kujua historia ya magonjwa ya kurithi kutoka upande wa baba, kama vile seli mundu au kisukari.

Vilevile, kwa kuwa mtoto hatamfahamu baba yake wala ndugu zake, kuna hatari ya kijamii ya yeye kuja kukutana na kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi au kuoana na ndugu yake wa damu (kama vile nusu-kaka au nusu-dada) huko mbeleni bila kujua.

Mwisho, uamuzi huu unamnyima mwanaume haki yake ya msingi ya kibinadamu ya kujua uzao wake na kushiriki kikamilifu katika malezi, huku ukikubebesha wewe mzigo mkubwa wa kiuchumi na kiakili wa kulea peke yako bila mfumo wa usaidizi.
Ingawa unaweza kuhisi unamlinda mtoto kuwa wako pekee, maslahi mapana ya mtoto yanahitaji uwazi ili kumpa malezi yaliyokamilika na salama kisheria
Sawa ndio maana nikauliza kama kuna namna ya kufanya hivyo

Hii kuoana ndugu haiwezekani maana mama hawezi kukubari maana atakua anajua ukoo wamtoto
 
Kumekua na migogoro mingi kuhusu watoto na inaumiza kicwa sasa nikaona niulize kama kuna uwezekano kwa mwanamke kujipatia mtoto wake binafsi bila ku share na baba mtu ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza
Yani unaandaa suluhisho la tatizo la kufikirika?Utahesabiwa uasi kabla hata haujaingia msituni.
 
nyoka ni code name.

wasiojulikana nao huitana jina hilo
Mkuu MKANGAFFU acha hizo mimi sihusiki na hayo mambo unayasema nipo zangu navuna mahindi na kahawa hapa Rushe karagwe

Karibu kaka kilimo kinalipa sana .
Najiita nyoka maana ni jina la utani naloitwa na jamaa zangu baada ya kuwa na tabia ya kukimbia mapigano huko bar ikiwa yatatokea basi uwa napotea kama nyoka ndiyo wakasema mimi sikimbii ila natambaa kama nyoka .

Kuna lingine mkuu naweza kukusimulia ?
 
Tatizo lipo ShesRise_1 linaanzia pale unapolala na mtu na kupata mimba yake alafu ukamficha kwanza hilo ni kosa sababu ni kuwa umehujumu jitihada zake za kukupa mimba .

Ila mbaya zaidi ni ukatili wa hali juu kwa kile kiumbe tarajiwa ,sababu muda ukifika atahitaji kumuoana baba yake ,kumdanganya au kumfichq baba yake ni ukatili wa kihisia ,hali ambayo sidhani unaweza kuishi na amani moyoni wala maishani mwako .

Ila kuna machaguo ya namna hii ,unaweza kuzungumza na mtu kuwa tuzalishane ila nahitaji kulea mwenyewe wapo wanaume wapo tayari kwa hilo isipokuwa ile kutambulishwa kwa mwanaye hilo jambo linakuja kufanyaika ijapokuwa baba mtu hakuhusika kwenye malezi .

Kwahivyo nahitimisha kwa kusema inawezekana japo sio sahihi na haifai maana haiko sawa kisheria na kimaadili .
Mm naomba niwe baba wa huyo mtoto. Niko tayari kuhujumiwa!

Cc. ShesRise_1
 
Back
Top Bottom