figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 28,132
- 64,416
Baada ya mkurugenzi wa mabasi ya Tilisho Safari aitwae John Tilisho (aliyevaa suti[angalia chini kwenye Video] ), kufungwa pingu kwa madai ya kukaidi agizo la uongozi wa Juu wa mkoa wa Dar es Salaam kuhusu stendi ya kimataifa ya Magufuli,
Mkuu wa Mkoa wa Dar bwana Chalamila kasema;
"...kama alivyosema amepigwa pingu kama sehemu ya onyo, natoa msahama kwa mkurugenzi wa Tilisho leo [Agasti 19,2026], nakwamba leo hii hii pia wamfungulie, na aruhusu mabasi yake yaweze kuingia na kutoka stendi ya magufuli...
kama kuna mtu yeyote anadhani nimekosea kutoa maelekezo haya, anipeleke mahakamani" Kasema Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, ndug. Albert Chalamila.
MY TAKE
Chalamila kaagiza Msimamizi wa Mabasi ya Tilisho fungwe pingu kwenye mkutano wa hadhara. Halafu akaambia waandishi wa habari wapige picha wazisambaze. Na wapambe wa Chalamila wakaambiwa wamzomee.
Nahisi wana ugomvi binafsi. Sababu hata Chalamila ni msafirishaji(transporter) kama Tilisho
Hii ni dalili ya serikali isiyofuata Sheria. Mwanasiasa anaamrisha Polisi kufanya chochote. Hata akisema ua wanaua.
Hii Video ni UVCCM wa pwani wameletwa Mbezi kushangilia maamuzi ya Chalamila. Walipofika Mbezi Stand wakajifanya eti ni Machinga. Michinga watoa wapi ngoma na mabango yenye picha ya Samia kwenye ziara ya kushitukiza?
Sasa kama muwekezaji anafamyiwa hivi, vipi sisi walala hoi?
Nalaani alichofamya Chalamila. Kalewa madaraka.
Boss kama kosa, angepewa barua ya wito? Atakimbia aende wapi?
Kapigwa pingu, kazungushwa zungungwa maeneo ya Standi kisha akaachiliwa bila kupelekwa polisi wala mahakamani wala kuchukuliwa maelezo.
Viongozi wa awamu ya Sita wana roho mbaya
WASIO MJUA JOHN TILISHO
John Tilisho ni Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Usafirishaji ya Tilisho Company Limited (Tilisho Safaris) inayofanya safari za mabasi ya mikoani kama vile Dar es Salaam kwenda Arusha, Moshi, na Rombo. Kampuni yake ni mwanachama wa wadau wa sekta ya usafiri na inahusishwa na chama cha wamiliki wa mabasi (TABOA) kupitia shughuli za usafirishaji.
Na wamiliki wa Mabasi walimtuma kwa mkuu wa mkoa awatetee. Alitaka wakae chini wajadiliane na Serikali, matokeo akapigwa pingu.