Baada ya mkurugenzi wa mabasi ya Tilisho Safari aitwae John Tilisho (aliyevaa suti[angalia chini kwenye Video] ), kufungwa pingu kwa madai ya kukaidi agizo la uongozi wa Juu wa mkoa wa Dar es Salaam kuhusu stendi ya kimataifa ya Magufuli,
Mkuu wa Mkoa wa Dar bwana Chalamila kasema;
"...kama alivyosema amepigwa pingu kama sehemu ya onyo, natoa msahama kwa mkurugenzi wa Tilisho leo [Agasti 19,2026], nakwamba leo hii hii pia wamfungulie, na aruhusu mabasi yake yaweze kuingia na kutoka stendi ya magufuli...
kama kuna mtu yeyote anadhani nimekosea kutoa maelekezo haya, anipeleke mahakamani" Kasema Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, ndug. Albert Chalamila.
MY TAKE
Chalamila kaagiza Msimamizi wa Mabasi ya Tilisho fungwe pingu kwenye mkutano wa hadhara. Halafu akaambia waandishi wa habari wapige picha wazisambaze. Na wapambe wa Chalamila wakaambiwa wamzomee.
View attachment 3653446
Nahisi wana ugomvi binafsi. Sababu hata Chalamila ni msafirishaji(transporter) kama Tilisho
Hii ni dalili ya serikali isiyofuata Sheria. Mwanasiasa anaamrisha Polisi kufanya chochote. Hata akisema ua wanaua.
Sasa kama Bosi anafamyiwa hivi, vipi sisi walala hoi?
Nalaani alichofamya Chalamila. Kalewa madaraka.
Boss kama kosa, angepewa barua ya wito? Atakimbia aende wapi?
View attachment 3653443