Kumfunika Kapt. John Komba na Katapilla ilikuwa dharau

Kumfunika Kapt. John Komba na Katapilla ilikuwa dharau

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,277
Reaction score
8,860
komba.jpg

Nimekaa na kutafakari kwa kina nimegundua ni dharau mbaya sana. Wote ni mashaidi na tumekuwa tukihudhuria maziko sehemu nyingi nchini. Lakini sijawahi kushuudia mfuniko wa kaburi unafunikwa na katapilla hiyo ni stail niliiona kwenye maziko ya Komba.

Narudia ile ni dharau pale kulikuwa na watu wengi tu waliokuwa na uwezo wa kunyanyua mfuniko ule na kufunika kaburi lile kwa heshima.
 
Nimekaa na kutafakari kwa kina nimegundua ni dharau mbaya sana
Wote ni mashaidi na tumekuwa tukihudhuria maziko sehemu nyingi nchini.
Lakini sijawahi kushuudia mfuniko wa kaburi unafunikwa na katapilla hiyo ni stail niliiona kwenye maziko ya Komba.
Narudia ile ni dharau pale kulikuwa na watu wengi tu waliokuwa na uwezo wa kunyanyua mfuniko ule na kufunika kaburi lile kwa heshima.
Labda waliconsider na uzito wake....
 
Methodius kilaini anweza kufafanua, manake inaonekana wametafsiri alivyozikwa lazarus.

Hii hata Nzigirwa anayo tafsiri na ufafanuzi, mkatoliki mwenye mitala na kanisa halikuwa na kinyongo kutoa huduma ya maziko (jambo la kiroho zaidi)
 
Mfuniko huo ni mzito tuache ushabiki na inategemea ulivyotengenezwa,,ipo myepesi ambayo hufungwa na bolt,,ipo mizito ya jig saw huwa mizito kwelikweli watu 20 hawanyenyui! Sio culvert hiyo kwamba mtai-roll!!
 
Hahahaha mkuu huo ni uzito gani ambao atuushudii tunaposhiki maziko sehemu nyingine?
Au mfuniko unawekwa kutokana na uzito wa marehemu?
Acha kutudanganya watu na akili zetu hapo makaburini kinondoni ukipita leo utakuta watu wanazika pale lakini huwezi kuona katapilla ni watu wanafunika kwa mikono yao.
 
Kama alizikwa kichama na kiserikali basi ujue pia uwezo wao wa kufikiri ndio huo.
 
View attachment 232420

Nimekaa na kutafakari kwa kina nimegundua ni dharau mbaya sana.

Wote ni mashaidi na tumekuwa tukihudhuria maziko sehemu nyingi nchini.

Lakini sijawahi kushuudia mfuniko wa kaburi unafunikwa na katapilla hiyo ni stail niliiona kwenye maziko ya Komba.

Narudia ile ni dharau pale kulikuwa na watu wengi tu waliokuwa na uwezo wa kunyanyua mfuniko ule na kufunika kaburi lile kwa heshima.

Ni kuiga mambo ya ughaibuni zaidi.

Ukienda kuzika mtoni ndio utaona vitu hivyo, ila sijaona Katapila baya kama hilo.

Kwa hiyo kwangu mimi jambo la kushangaza ni Katapila baya, si Katapila.

Nishaenda mazishi ya babu mmoja jirani familia yake iliishia funeral home tu, mimi na jirani mwingine mama wa KiJamaica ndio watu pekee tulioenda makaburini kuzika. Tulipoweka mchanga kumzika yule babu chepeo chache baadaye watu wa pale makaburini wakatumia ki tractor maalum cha kuzikia kumaliza kuzika.

Kimtoni mtoni watu wengi hawaziki, hivyo mashine hizi zinaweza kuhitajika practically.

Kibongo bongo hata kama kila mtu mmoja akipiga chepeo mbili hapo wanazika, ila tulivyozoea kuiga tutataka kuzika kwa fashion ya katapila.

Ndicho kilichotokea hapo.

Komba alishasema anataka mazishi ya kifahari.
 
Huo ni mfuniko tu mleta uzi! Wangetumia catapilla kuweka mchanga hapo ningeunga mkono hoja yako. Huo mfuniko ni mzito sana kutokana na uimara wa kaburi.
 
Jaman kwal ule mfuniko wa kabuli la nyerere ulikuwa mzito au mwepesi, mbona hatukuona ule mkatapila jamani, alafu huyu si alikuwa capten kwanini wasingefika wajeda kusaidia!
 
kushusha jeneza na kamba au na mashine napo ni dhambi?
 
Ni kuiga mambo ya ughaibuni zaidi.

Ukienda kuzika mtoni ndio utaona vitu hivyo, ila sijaona Katapila baya kama hilo.

Kwa hiyo kwangu mimi jambo la kushangaza ni Katapila baya, si Katapila.

Nishaenda mazishi ya babu mmoja jirani familia yake iliishia funeral home tu, mimi na jirani mwingine mama wa KiJamauca ndio watu pekee tulioenda makaburini kuzika. Tulipoweka mchanga kumzika yule babu chepeo chache baadaye watu wa pale makaburini wakatumia ki tractor maalum cha kuzikia kumaliza kuzika.

Kimtoni mtoni watu wengi hawaziki, hivyo mashine hizi zinaweza kubitajika practically.

Kibongo bongo hata kama kila mtu mmoja akipiga chepeo mbiki hapo wanazika, ila tulivyozoea kuiga tutataka kuzika kwa fashion ya katapila.

Ndicho kilichotokea hapo.

Komba alishasema anataka mazishi ya kifahari.

duh!!.:biggrin::biggrin:
 
Back
Top Bottom