Kumi bora ya wacheza mpira wa miguu kuwahi kutokea hapa duniani mpaka sasa

Championship

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2019
Posts
5,500
Reaction score
10,616
Wafuatao ndio wachezaji bora wa mpira wa miguu kuwahi kutokea duniani. Vigezo ni mafanikio binafsi, mafanikio kwenye timu walizochezea ikiwepo timu za taifa:

1. Lionel Messi
2. Edson Pele
3. Diego Maradona
4. Christiano Ronaldo
5. Franz Beckenbauer
6. Johan Cruyff
7. Zinedine Zidane
8. Ronaldo De Lima
9. Ronaldinho Gaucho
10. Michael Platin
 
Good list mkuu but me always charity start at home, Jella Mtwaga,Sunday Manara, Aluu Ally na mafanikio ya no 9 kwenye list yako na ninamlinganisha na Jay Jay Okocha, naona mpopo huyu yupo juu sana
Hao ni wazuri kwa level yao lakini sio kwa dunia nzima mkuu.
 
Wafuatao ndio wachezaji bora wa mpira wa miguu kuwahi kutokea duniani. Vigezo ni mafanikio binafsi, mafanikio kwenye timu walizochezea ikiwepo timu za taifa:

1. Lionel Messi
2. Edson Pele
3. Diego Maradona
4. Christiano Ronaldo
5. Franz Beckenbauer
6. Johan Cruyff
7. Zinedine Zidane
8. Ronaldo De Lima
9. Ronaldinho Gaucho
10. Michael Platin
Hivi mpaka sasa hivi ni wachezaji wangapi wanaongoza kwa magoli duniani? Ukimtoa Pele.
 
Mpaka sasa list ipo hivi:

Christiano Ronaldo 815
Lionel Messi 773
Edson Pele 762
Romario 755
Ferenc Puskas 729

*Pele huwa anaweka goli za kitaani na mechi za kirafiki ndio maana wanasema anafikisha 1300+ lakini goli za mashindano ndio hizo hapo.
 
Vyovyote iwavyo ila hakuna kama PELE.

kwenye kujilinda yupo vizuri kushambulia ndo usiseme ana dribling, skills, stamina ball control na nguvu.

anafunga kila aina ya magoli iwe tiktak, acrobatic,rabona mashuti ya mbali vilevile kwa freekick, penalt, kichwa hadi mkono.

Kijana wa miaka 18 tena mweusi kwenye miaka ya 50 kipindi ambacho ubaguzi ilikuwa jambo la kawaida lakini kutokana na uwezo wake aliitwa kwenye timu ya Taifa huku akiwa mchezaji tegemezi kwenye timu pamoja na umri wake mdogo hakuwaangusha WABRAZIL kwa kuwapa taji la kwanza la kombe la dunia yeye akifunga magoli mawili kwenye fainali.

Katika zama ambazo mwamuzi kutoa faulo hadi mtu atolewe jino kwa teke au damu itoke puani na ili mtu apate kadi nyekundu hadi amvunje mtu mguu,. kwa kifupi kandanda ilikuwa kama rugby lakini kijana alifunga goli 700+.

NB: Haya tunayoyaona kwenye video fupifupi ni 1/20 ya mambo aliyoyafanya kwenye kandanda.

HAKUNA KAMA EDSON ARANTES DO NASCIMENTO (PELE)
 
Hakuna mtu anayeweza kupinga uwezo wa Pele kwenye soka na ndio maana yupo namba mbili.

Mpira haukuwa na sheria kali enzi hizo japo sio mbaya kama ulivyodokeza. Na ukweli ni kwamba ni vigumu kufanikiwa kwenye mazingira ya sheria kali na nyingi kuliko inapokuwa free style.
 
Kweli kabisa mpira kipindi hicho haukuwa na sheria kali PELE alikuwa anapigwa mitama, ngumi vichwa na wakati mwingine kukumbatiwa kabisa ila refa hatoi kadi wala faulo .

achana na hawa mandezi wa sasa mtu anaguswa kidogo tu ila anaruka kama amepigwa bomu na mwamuzi anatoa kadi na pigo huru/penalt yani hawa vilaza laiti wangecheza enzi za kibabe za PELE hata goli 50 wasingefikisha.

NB: HAKUNA KAMA PELE.
 
Have a respect to pele Bro!!,Pele hapaswi kuwa namba mbili huyo ni namba moja,alikuwa ana kila kitu katika soka mamb aliyoyafanya Ronaldinho haya ya kupiga kanzu watu kumi Pele alishayafanya kitambi sana,Pele mmoja alikuwa na chembechembe za Ronaldinho+Messi+Cristiano Ronaldo+Zidane,magoli ya Rabona na Acrobatic kafunga sana haya...na ana kila kitu katika mafanikio ambavyo hata messi hana
 
Pele kwenye kutafuta mwanasoka bora wa karne ya 20 alibebwa na FIFA pamoja na IFFHS baada ya kuona anazidiwa na Maradona wakabadilisha polling style na ikabidi wawape wote wawili.

Alikuwa mzuri sana lakini sio kwa kumzidi Messi. Huyu ndio hasa mfalme wa soka hapa duniani.
 
Wafuatao ndio wachezaji bora wa mpira wa miguu kuwahi kutokea duniani. Vigezo ni mafanikio binafsi, mafanikio kwenye timu walizochezea ikiwepo timu za taifa:

1. Lionel Messi
2. Edson Pele
3. Diego Maradona
4. Christiano Ronaldo
5. Franz Beckenbauer
6. Johan Cruyff
7. Zinedine Zidane
8. Ronaldo De Lima
9. Ronaldinho Gaucho
10. Michael Platin

Namba 2 muweke Diego Maradona
 
Mpaka sasa list ipo hivi:

Christiano Ronaldo 815
Lionel Messi 773
Edson Pele 762
Romario 755
Ferenc Puskas 729

*Pele huwa anaweka goli za kitaani na mechi za kirafiki ndio maana wanasema anafikisha 1300+ lakini goli za mashindano ndio hizo hapo.

Nasubiri wabishi na wakaririshwaji waje wakupinge kuhusu pele😁.

My opinion, best players ever ni Diego Maradona na Messi, wanafuata wengine.
 
Vyovyote iwavyo ila hakuna kama PELE.

kwenye kujilinda yupo vizuri kushambulia ndo usiseme ana dribling, skills, stamina ball control na nguvu.

anafunga kila aina ya magoli iwe tiktak, acrobatic,rabona mashuti ya mbali vilevile kwa freekick, penalt, kichwa hadi mkono.

Kijana wa miaka 18 tena mweusi kwenye miaka ya 50 kipindi ambacho ubaguzi ilikuwa jambo la kawaida lakini kutokana na uwezo wake aliitwa kwenye timu ya Taifa huku akiwa mchezaji tegemezi kwenye timu pamoja na umri wake mdogo hakuwaangusha WABRAZIL kwa kuwapa taji la kwanza la kombe la dunia yeye akifunga magoli mawili kwenye fainali.

Katika zama ambazo mwamuzi kutoa faulo hadi mtu atolewe jino kwa teke au damu itoke puani na ili mtu apate kadi nyekundu hadi amvunje mtu mguu,. kwa kifupi kandanda ilikuwa kama rugby lakini kijana alifunga goli 700+.

NB: Haya tunayoyaona kwenye video fupifupi ni 1/20 ya mambo aliyoyafanya kwenye kandanda.

HAKUNA KAMA EDSON ARANTES DO NASCIMENTO (PELE)

Upo sahihi kwa upande wako

Messi
Diego Maradona

Halafu acheni kukariri eti old is gold, kwani binadamu wa zamani na wa sasa ni tofauti!! Wazamani walikua na miguu ya chuma vifua vya tembo!!!

Haya tunayoyaona kwenye video fupifupi ni 1/20 ya mambo aliyoyafanya kwenye kandanda.

Kwahiyo hata Maradona, Messi na zidane wameiga kwa pele? Alikua na maajabu gani kuwazidi hao!!!
 
Hakuna mtu anayeweza kupinga uwezo wa Pele kwenye soka na ndio maana yupo namba mbili.

Mpira haukuwa na sheria kali enzi hizo japo sio mbaya kama ulivyodokeza. Na ukweli ni kwamba ni vigumu kufanikiwa kwenye mazingira ya sheria kali na nyingi kuliko inapokuwa free style.

Kwa sheria za sasa na hata enzi za maradona, kufikisha hayo magoli ni mbinde, huyo pele alizungukwa na wachezaji wazuri na pia sheria nyingi hazikuwepo wakati huo ndio maana alikua anajifungia tu,

Mpaka sasa bado cjaona aliewafikia japo nusu yao tu hawa,(Messi and Diego) dribbling, skills n.k n.k, wanaufanya mpira uonekane mwepesi, hawa ndio wamenifanya niupende mpira zaidi na zaidi. So, kwangu mimi hakuna kama (Messi na Maradona)
 
Kweli kabisa mpira kipindi hicho haukuwa na sheria kali PELE alikuwa anapigwa mitama, ngumi vichwa na wakati mwingine kukumbatiwa kabisa ila refa hatoi kadi wala faulo .

achana na hawa mandezi wa sasa mtu anaguswa kidogo tu ila anaruka kama amepigwa bomu na mwamuzi anatoa kadi na pigo huru/penalt yani hawa vilaza laiti wangecheza enzi za kibabe za PELE hata goli 50 wasingefikisha.

NB: HAKUNA KAMA PELE.

Ni maoni yako tu
 
Have a respect to pele Bro!!,Pele hapaswi kuwa namba mbili huyo ni namba moja,alikuwa ana kila kitu katika soka mamb aliyoyafanya Ronaldinho haya ya kupiga kanzu watu kumi Pele alishayafanya kitambi sana,Pele mmoja alikuwa na chembechembe za Ronaldinho+Messi+Cristiano Ronaldo+Zidane,magoli ya Rabona na Acrobatic kafunga sana haya...na ana kila kitu katika mafanikio ambavyo hata messi hana

Ni maoni yako, hivyo kila mtu na mawazo yake

Ukiniuliza ni mchezaji gani kwako bora zaidi kuwahi kutokea nitakuambia Messi na Maradona, why?? Wakati wa pele hakukua na sheria ngumu, inasemekana hata sheria za offside hazikuwepo, na kwa upande wa w/cup hunishawishi nimkubali eti kwa sababu ana w/cup, kwani ajabu yake nini!! Hata giroud analo, gaucho analo, iniesta analo, de lima analo, zidane na benzema wanayo, so hawa wote wamewazidi Maradona na Messi!!🤣🤣 Though Diego analo!

Kumbuka pele alikua na wachezaji wazuri, so ile ni only team work, tofauti na maradona alikua jeshi la mtu mmoja, world cup alibeba, napoli alivyoikuta ilikua mbovu, ujio wake uliibadilisha NAPOLI na kubeba makombe ya UEFA n.k. huyu ndie Diego Armando Maradona ninaemjua jeshi la mtu mmoja.

(Messi na Diego) Best players ever, i have no doubt, na itatake many years kuwafikia hawa.
 
Back
Top Bottom