Kumi bora ya wacheza mpira wa miguu kuwahi kutokea hapa duniani mpaka sasa

Kumi bora ya wacheza mpira wa miguu kuwahi kutokea hapa duniani mpaka sasa

Bahati mbaya mwanzisha nyuzi hii anataka kubishana na dunia,zaidi ya miaka 60 hajatokea mwanadamu anayejua hii kitu inaitwa futbol-dunia nzima ilikubali na inakubali ni Pele alafu Maradona,kumbuka kizazi hicho hakikuwa na jamiiforum,Facebook,Twitter, Instagram wala Tik
 
Wafuatao ndio wachezaji bora wa mpira wa miguu kuwahi kutokea duniani. Vigezo ni mafanikio binafsi, mafanikio kwenye timu walizochezea ikiwepo timu za taifa:

1. Lionel Messi
2. Edson Pele
3. Diego Maradona
4. Christiano Ronaldo
5. Franz Beckenbauer
6. Johan Cruyff
7. Zinedine Zidane
8. Ronaldo De Lima
9. Ronaldinho Gaucho
10. Michael Platin
Bila Juma Nyosso list haijakamilika.
 
kweli kabisa pele alizungukwa na wachezaji wazuri sio kama messi ambaye barca alizungukwa na vilaza kama Puyol,D.Alves,Pique, Ronaldinho, Xavi ,Iniesta, Henry, Etoo, Ibrahimovic, Neymar,Fabrigas, Suarez ,Sanchez, na David villa huku argentina akiwa na mazezeta kama Mascherano, Aguero, Icardi, Di Maria, Dyabala na Tevez.
Hahahaha
 
Ili ueleweke ungeweka na hayo mafanikio ya kila mmoja, maana uko too general unavyosema umeangalia mafanikio binafsi hayo mafanikio binafsi ni katika category zipi?? Goals?? Assists?? Dribbles?? Sasa utuwekee hapa kila kigezo na namba za kila mchezaji uliyemshindanisha then ndo uje na conclusion maana kusema tu Messi au Pele au Ronaldo ni wa Kwanza bila kuweka ushahidi inakuwa ni nadharia tu na kila mtu ataanza kuvutia upande wake

Mfano
Assists Messi 200 Ronaldo 100 Pele 120
Dribbles Messi 1700 Ronaldo 1400 Pele 1300
Goals......................
Balloon d or..............
Puskas awards.................
UEFA trophies................
UEFA goals...................
League goals................
Most golden boots.......

Nadhan hizo ni baadhi ya vigezo unavyoweza kutumia kwenye mafanikio binafsi sasa ungetuwekea ya Kila mchezaji vinginevyo inakuwa ni kelele za ushabiki tu

Ufanye hivyo pia na kwenye national team Ila kuongea tu Kwa maneno bila kutuwekea evidences inakuwa haina mashiko, imagine mtu ambaye Hana interests na mpira bila kuweka data atakuelewa vipi?? Wataalamu wanasemaga "Numbers don't lie"
 
Mnapo jadili wachezaji bora duniani naombeni msiwe mnamuweka Pele kwani yule hakuna mchezaji wa kawaida alikuwa ni "mchawi wa kabumbu duniani."
 
Back
Top Bottom