Uchaguzi 2020 Kumkata Paul Makonda kwenye Kura za Maoni CCM, siyo maamuzi yenye akili

Kwa hiyo akikatwa ndio umuhimu wake utakuwa umeishia hapo?.
 
Kwenye siasa lolote linaweza kutokea mkuu. Ndio maana usishange tukijitokeza kuonyesha umuhimu wake. Sio tusubiri akose ndio tujitokeze kuonyesha sifa zake.
Hata wewe bila kumnadi atapita tu,sio kwamba bila yeye nchi itasimama hapana ila bila yeye haiwezekani kwa serikali yetu.
 
Ningelikuwa mimi ni mwenyekiti ningewakata Makonda, Gambo, Mnyeti alafu baada ya uchaguzi ningewateua katika vyeo vya chini zaidi ya walivyokuwa navyo kabla hawajaenda kugombea.

Ningewapeleka kuwa wakuu wa wilaya.
 
Hata wewe bila kumnadi atapita tu,sio kwamba bila yeye nchi itasimama hapana ila bila yeye haiwezekani kwa serikali yetu.


Upo sahihi kabisa
Ila ninachokifanya ni kuwa, ikiwa mahasimu wanajitahidi kumshusha, sio vibaya nami ninayeona umuhimu wake nikimsema kwa mema. Haijalishi nitaongeza nini au sitaongeza
 
Ningelikuwa mimi ni mwenyekiti ningewakata Makonda, Gambo, Mnyeti alafu baada ya uchaguzi ningewateua katika vyeo vya chini zaidi ya walivyokuwa navyo kabla hawajaenda kugombea.

Ningewapeleka kuwa wakuu wa wilaya.

Kwa nini Mkuu?
 
1) unasema hajafanikiwa ktk Mambo mengi kutokana na mipaka ya cheo chake...je wajua ukomo wa majukumu ya mbunge?
2)kajenga hofu ktkt jamii... unapenda Kiongozi anayetuletea hofu kama enzi za mjerumani?
3) unataka apewe cheo kikubwa zaidi ya mkuu wa Mkoa...katika muhimili wake vyeo vikubwa vilivyobaki ni kimoja Tu..PM.
4) Hiyo tabia ya kutoa maneno ya shombo na kujikweza sio recipes nzuri ktk KAZI za uwakilishi.
 
Umetoa mpaka namba ya simu .safi sana
 

1. Nafahamu
2. Moja ya kiongozi bora mwenye kuleta maendeleo ni kuleta hofu. Fuatilia historia utaelewa hilo. Hata hizo nchi za ulaya zilijengwa kwa hofu zilizoundwa na viongozi shupavu
3. Hata akipewa U-PM Haina shida, lakini uwaziri upo kitaifa zaidi tofauti na mkuu wa Mkoa ambapo yupo level ya mkoa yaani mipaka yake ni mkoa mmoja
4. Upo sahihi, lakini maneno ya shombo inategemea anayasema wakati gani na anamwambia nani? Hata Yesu alikuwa ana maneno ya shombo
 
Ndo alivokutuma ?
 
Kura za wajumbe ndio zitaamua kama aendelee ama awekwe pembeni
 
Sote wapemba tulimpigia chapuo Shamsi kuna manyang’au wakampitisha Mwinyi ambae hatumjui , kwasasa sisiem siwaamini kabisa badala ya Ndugulile utaambiwa kapita Makonda yule mwizi wa vyeti vya shemeji yake!! kuna wasaa huwa nasikia aibu kuwa mtanzania hasa wajinga kama Makonda wanapohodhi madaraka makubwa!!

Wewe mtoto Jana ulijitambulisha humu jukwaani JF mimi nikakuuliza ‘kwani wewe nani’, leo me myself and I ndo nimegundua kumbe umetumwa na unalipwa na Makonda kumpigia kampeni mtandaoni! au labda ni wewe mwenyewe Makonda uko nyuma ya keyboard!! wengine tumesoma shule za vipaji na tuna vyeti halisi na hatujawahi kuiba mtihani!!

mtu kuandika uzi au comment kwa kirefu hutokana na
1. motive and
2.motivation!! unajua tofauti zake?

hongera kuna watu umewapata!!
 
Makonda kukatwa ni ndoto za alinacha tena za mchana kweupe mapeema kwa wengine waweze wana nini na yeye ashindwe ana nini hamtaamini atakavyo kuja kuwa mbunge kamili tena kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi na wananchi mwisho wa siku mtazimia kama sio kustaajabu atakapo kuja kuwa waziri muda utaongea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…