Kumkumbatia Mwanamke aliyeko Eda imekaaje hii Masheikh!?

Kumkumbatia Mwanamke aliyeko Eda imekaaje hii Masheikh!?

Huyo kitumbo alisababisha Jf ikafungiwa, picha wanaachia wenyewe wataalamu wa picha wakianza kuchambua inakuwa nongwa
 
Bila shaka Eda na Udhu vinaenda sambamba! Mimi sio muislam niko tayari kuelimishwa.

Je mwanamke aliyeko Eda kukumbatiwa na mwanaume inaswihi!?
Nilitarajia kusoma picha tu, lakini naona hukutaka usomeke. Sasa hii ni mada ya aina gani hii!
 
Bila shaka Eda na Udhu vinaenda sambamba! Mimi sio muislam niko tayari kuelimishwa.

Je mwanamke aliyeko Eda kukumbatiwa na mwanaume inaswihi!?
Kama ni kiongozi haina shida mana anajitambua.
 
Mwanamke yoyote wa kiislamu hata asipokua Eda hairuhusiwi kukumbatiwa au kugusana na mtu yoyote ambaye anaweza kumuoa. Watu ambao hawawezi kumuoa ni

-Watoto wake
-wakwe zake
-kaka zake
N.k

Surat Anisai aya ya 23 mwenyeziMungu anasema
Mmeharamishiwa (kuwaoa) mama zenu, na binti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na mama zenu wakubwa au wadogo (mashangazi wa upande wa mama), na binti wa ndugu wa kiume (wapwa), na binti wa ndugu wa kike (wapwa), na mama zenu waliokunyonyesheni, na dada zenu wa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu waliozaliwa na wake zenu mliowaingilia—lakini ikiwa hamjawaingilia basi hakuna dhambi kwenu (kuwaoa watoto wao)—na wake wa wanenu waliotoka katika migongo yenu, na kuwaunganisha dada wawili (kuwaoa kwa pamoja), creates kile kilichokwisha pita. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu."
Ikitokea mfiwa akajisahau, anatakiwa afanyeje?
Zingatia Mungu wa Israel ni mtu wa msamaha!
 
Mashehe hawa hawa njaa unategemea watatoa ufafanuzi sahihi kwa hili!? Acha kuchekesha Mkuu. Unataka wafe njaa!?
 
Nilikuwa nauliza hakuna Protokali inayofuatwa kumpiga Rais picha? Maana hii naona kama inatutia aibu! Mwisho watu watasema alikuwa anangojea mtu wa kuchukua jimbo!
 
Tanzania kama Azerbaijan hakuna imani au msimamo mkali kiimani, kwa Tanzania mila za kitamaduni, asili za kiafrika, kuoleana, watoto wa kufikia n.k pia bila kuacha athari chanya za upande wa 61% umechuja imani kali ya upande 39% CIA factsheet

Ikumbukwe uhusiano umeanza kabla ya 26 April 1964 wa makaratasi ya muungano, kwani jamii za Mapumbugwe, Wangwana, Wanyamwezi, Wachewa walikuwa na mahusiano na Zanzibar kubwa kabla ya mazingaombwe ya Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume 1964 kuwa wao ndiyo walioanzisha mahusiano na mwingiliano baina ya Zanzibar na bara giza la Afrika la kingdoms (falmekabila) kibao za Tanganyika, Nyasaland, Sofala Mocambique, Zimbabwe, Congo, Baganda, UrundiRwanda n..k

Mke Kukaa Eda Ya Kufiwa Na Mumewe​


1789132251858.png



UFAFANUZI KWA MUJIBU WA KORAN
Sheikh Muhammad Mahdi-shushtari Mke Kukaa Eda yakufiwa Na Mumewe
Mwanamke mwenye kufiwa na mume kama hana mimba eda yake ni miezi minne (4) na siku kumi (10), na kama mwenye mimba eda yake mpaka azae, lakini iki wa amezaa kabla ya kupita miezi minne na siku kumi lazima akae eda hadi zipite, siku hizo.

Mwanamke mwenye eda ya kufiwa na mumewe, ni haramu kuvaa nguo za rangi; kujipamba kwa namna yo yote kwa mwili au kwa nguo kama kujitia manukato, kutia wanja machoni, mapodari, hina na kila jambo la kujipamba ni haramu kwake hata nguo nyeusi ikiwa ina nakshi au mkato wa kujipamba.

Eda huanzia siku ya kufa kwa mume ikiwa yupo hapo, na kama hayupo huanzia siku atakapopata habari hata kama kumepita muda mrefu sana. Katika muda huo wa eda hawezi kuposwa au kuolewa.

Uislamu unaamrisha unadhifu, basi wanaruhusiwa wanawake wenye eda kuoga kujisafisha na kuweka mwili safi, kukata kucha.

Anaruhusiwa kutoka nje kama ipo haja kama kununua mahitaji yake au kumwangalia jamaa au mgonjwa na kadhalika, asitoke nje paisipo na haja.

Tunaomba kwa Mola wetu atupe sote Twafiki ya kufuata maamrisho ya dini na kuepukana na yaliyoharamishwa au kufuata mambo ya Bida'a uzushi, usiona msingi.

https://al-islam.org/sw/mambo-yanay...80"]https://m.youtube.com/watch?v=lRJqKloRX80
 
Unachanganya concepts, mbaya ni pale unapoingiza mambo kwa utashi wako ..Uislamu unafanya kazi katika mfumo sio vipande vipande , ungeanza kuuliza juu ya kuwa kiongozi mkubwa wa nchi ikiwa kuna wanaume wanaoweza .

Uongozi wake tu hautambuliki kwa sababu wapo wanaume , bado unakuja sehemu ya pili .Suala hilo hauwezi kulielezea zaidi kwa sababu hapo kafuata protocal za kazi yake sio dini yake , kitendo cha kuwa Rais ni kinyume cha uislamu , kama ukivunja protocal kubwa basi nyingine hauwezi kuzielezea ..Usiongelee dini vipande vipande , kesho kama kiongozi anatakiwa kuingia kanisani na kusali kwani anawakilisha watu wote sio nchi ya kiislamu hii .

Uislamu ni mfumo sio vipande , kuna watu hauwezi kuwajudge katika uislamu kama walivunja protocal kubwa .Kwa mfano : mtu akishakuwa msanii wa muziki alishaavunja protocal kubwa , hauwezi tena kumjudge eti ametangaza pombe au anakula nguruwe , anafanya uzinzi , anakaa uchi wakati yeye ni msaani na hayo ni miongoni mwa mambo ya kisanii kwa dunia yetu .

Niwaombe , kama mnaweza jaribuni kumuelezea kama Rais kuliko kuingiza uislamu , itakuwa unafiki kwa sababu huyo ni Rais wa wote so dini yake hapo haina matter kama ingekuwa ina matter sana kikamilifu basi asingefikia hapo . Atakapostaafu basi itakuwa ni rahisi kumuelezea kama muislamu , kitendo cha demokrasia basi ni haramu .

Hakuna kitu kimekatazwa kwamba labda Mungu ananufaika , hapana ni taratibu za kimsingi , kila kitu kina madhara ya kijamii sio kwamba ukienda kinyume cha maamrisho Mungu apungukiwa ...​
 
Back
Top Bottom