Kumpeleka mtoto shule yenye ada kubwa ni kupoteza tu hela

Ni jambo muhimu sana kuacha kupangia watu matumizi, kama shule ya ada ya 5M au 15M unaiona ni kubwa kuna mwingine hiyo ni hela ya shopping ya weekend moja, kifupi kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake asianze kuchunguza kamba ya mwenzake

Mzee sjaongelea hela nimeongelea mwanafunz anapomalza shule anakuwa hana cha kufanya si bora hiyo hela umtengenezee mazngra ya baadae
 
Una mawazo kama yangu.

Mi sipeleki mtoto shule binafsi.

Nitamkazania hukuhuku shule za serikali atafaulu vizuri tu.

Kabisa hiyo hela ya kumpeleka shule za gharama ni bora umtengenezee mazingira ya baadae hil akimalza asiwe jobless
 
Wana lipi wanalojifunza huko?

Na wakitoka huko wanakuwa special kuliko wengine?

Si watakuwa mainjinia, waendesha ndege, madaktari, walimu, wafanyabiashara kama tu hawa wa Buza?

Hizo kazi je zipo au anakuja kuwa joblesss
 

Wangapi wamesomeshwa nje wapo tu nyumban wanalewa hovyo
 
Tutanatofautiana malengo mkuu,
Ningekuwa na hela ningempeleka akasome hayo mashule ya Ada 70M/yr ili aoate network na vyuo nampeleka mamtoni pia,

Akimaliza vyote namkabidhi 2B aanze maisha.

Wangap wamesoma huko leo hii wako wapi
 
Shida ni pale ambapo mzazi anajinyima hadi hatua ya mwisho plus vikoba ili mwanae asome private na akimaliza mtoto anabaki mzigo kwa mzazi na mzazi anakuwa mzigo kwa mtoto wanabaki wnaangaliana tu
 
Shida ni pale ambapo mzazi anajinyima hadi hatua ya mwisho plus vikoba ili mwanae asome private na akimaliza mtoto anabaki mzigo kwa mzazi na mzazi anakuwa mzigo kwa mtoto wanabaki wnaangaliana tu
bado hoja haina msingi maana ni sawa na kusema ningejua!!

tenda wema uende zako usingoje....
 
Kuna watu wanashindwa kukuelewa mkuu, Yaani mtu anayeingiza labda milioni 20 kwa mwezi anampeleka mtoto shule ya million 5 kwa mwaka kwake anaona amempeleka shule ya gharama ndo maana wanaropoka tu, ila wanatakiwa kuelewa mlengwa wa maada ni nani? Kwa ufafanuzi ni yule mzazi ambaye anapambana anateseka yaani anakaa njaa kabisa et anasomesha mtoto private then huyo mtoto akimaliza chuo aje akae nyumbani ateseke, kumbe bora angempeleka shule za kawaida tu akapata elimu aje mtaani kupambana na changamoto za maisha au kama mzazi amejaliwa basi yale mapambano ya kusomesha shule za gharama angepambana kumuandalia mtoto cha kuanzia pindi atakapomaliza elimu yake,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…