SHILINGI TRILIN 1.5 ZA KITANZANIA
1. Kama una kasi ya kuhesabu shilingi milioni moja kwa dakika moja. Maana yake Shilingi trilioni 1.5 utazihesabu kwa dakika 1,500,000, sawa na masaa 25,000, sawa na siku 1042, sawa na miaka 2 na miezi kumi.
2. Noti moja ya Tsh. 10000 in urefu wa Sentimita 15 na upana wa Sentimita 7.5. Ukitafuta eneo la mstatili wake ni sawa na Sentimita za eneo (mraba) 112.5 au (112Cm²).
Idadi ya noti za elfu 10 kwenye Tsh. Trilioni 1.5 ni noti 150,000,000. Ukizidisha na ile 112.5 ni sawa na eneo la Sentimita za mraba 16,875,000,000 au Mita za mraba 1,687,500. (1,687,500m²)
Uwanja mmoja wa mpira wa miguu wenye urefu wa mita 100 na upana wa mita 75 una eneo la 7500m²
Chukua (1,687,500 ÷ 7500) = 225
Maana yake, Tsh. Trilioni 1.5 unaweza kuzipanga zikafunika eneo sawa na viwanja 225 vya mpira wa miguu.
3. Kwa urefu wa Sentimita 15, kwa idadi ya hizo noti 150,000,000 ni sawa na umbali wa sentimita 2,250,000,000 sawa na kilometa 22,500.
Jumla ya umbali wa mipaka yote ya Tanzania bara pamoja na ufukwe wa bahari kutoka Tanga hadi Mtwara ni Km 4826.
Kwa hiyo ukizipanga kwa urefu pesa hizi, zinaweza kufanya mizunguko minne katika mipaka yote ya Tanzania bara (Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, Zambia, Malawi, Msumbiji na ufukwe wa bahari ya hindi kutoka Tanga hadi Mtwara) na bado zitabaki za kutosha umbali wa Km 3196.
Hizo zinazobaki unaweza kuzipanga mistari miwili kutoka ncha ya mbali kabisa ya kaskazini hadi ncha ya mbali ya kusini mwa Tanzania bara (Km 1223 X 2 = Km2446) Na bado zitabaki za Km 750. Ambazo zitapangika kutoka DSM had Tanga mara tatu na kubaki za Km 162. Hizo baki nazo mwenyewe.
4. Ikiwa Noti moja ya elfu 10 ina uzito wa gram 1, maana yake kwenye Trilioni 1.5 (noti milioni 150) zina uzito wa gram milioni 150 (150,000,000gm) au kilogram 150,000 sawa na uzito wa tani 150. Reli ya Standard Gauge inayojengwa inaweza kuhimili mzigo wa uzito wa Tani 35.
5. Zinatosha kujenga kilometa 500 za Reli ya STG kwa viwango vya ubora na gharama za sasa (kwa mfano wa hii iliyoanza kujengwa)
6. Ukipewa pesa hiyo na kuamua kutumia Tsh. Mil 10 kila siku. Zitaisha baada ya miaka 41.
[(1.5x10¹²) ÷ (10x10e8)]/365¼ = 41
7. Zinatosha kugawa TSh. 200 kwa kila Binadamu duniani, TSh 1000 kwa kila Mchina na TSh. 30,000 kwa kila Mtanzania.
8. Ukiweza kuzigawa pesa hizo 'kipedejee' kwa kuwarushia watu noti moja moja kila baada ya sekunde moja, bila kupumzika, itakubidi utumie miaka minne na miezi 9 ili ugawe zote.
9. Tsh. Trilioni 1.5 ni utajiri karibu sawa na utajiri wa Bilionea Mohammed Dewji. Ni zaidi ya fedha zilizotumika kwenye uwekezaji wa kiwanda cha Cement cha Dangote (1.3trilion). Ni nusu ya Utajiri wa Rais wa Marekani, Bilionea Donald Trump.
10. Pesa hiyo ni mara 25 ya pesa waliotumia Marekani katika kushambulia miji ya Homs na Damascus nchini Syria tarehe 14 Aprili 2018. Marekani walitumia Nyambizi inayotumia umeme wa nyuklia, ndege ya kijeshi aina ya B-1 bomber na meli moja ya kivita huku bajeti ikiwa dola Mil 26, sawa na Tshs bilion 60. Wamarekani wameandamana nchini kwao kupinga matumizi mabaya a ya kodi zao. Kwa hizi pesa zetu zisizoonekana wangeweza kufanya mashambulizi mengine 24 kama hayo.