Ninachokiona hapa ni watu kutupiana maneno kwa kebehi...
Sioni tatizo kwa Polepole kumjibu Zitto kwasababu Zitto alitoa msimamo wa chama kuhusu Taarifa ya CAG na siyo msimamo wa mbunge...
Polepole nae kama kiongozi wa chama anayo haki yakutoa msimamo wa chama chake kuhusu ripoti hiyo...
Hoja ya msingi hapa ni je Ni nani Kati ya Zitto na Polepole anahoja za msingi???
Nimemsoma Zitto na nimezisoma hoja za Polepole....
Zitto ametoa hoja 8 kutoka katika ripoti ambazo hata CAG alihojiwa Azam akakiri kuna fedha haionekani ilipo....!
Polepole amechambua kimahesabu namna hela iyo ilivyo paswa kuwa...!
Polepole pengine anaweza kuwa na hoja sina hakika sana...ninachojiuliza mimi hao waandishi waliokuwepo walishindwa kumuuliza Polepole maswali haya?
1)Yeye kama kiongozi wa Chama je hakubaliani na ripoti ya CAG kuhusu huo upotevu?
2) Kama kweli hakubaliani nao je CAG ameupotosha Umma na Bunge?
3) Je uchambuzi alioutoa leo ndivyo CAG alipaswa kuweka ripoti yake? Na kama ndivyo je4 CAG na wataalamu wake walikosea namna ya kukagua na kuweka sawa hesabu za serikali?
4) CAG ameweka dosari za matumizi ya fedha kwenye baadhi ya vyama vya siasa ikiwamo CCM na Chadema, kwa maelezo yake ametoa ufafanuzi juu ya dosari kwa upande wa CCM lakini akawalamu Chadema kwa ubadhirifu, Je anakubaliana na ripoti ya CAG kuhusu matumizi mabaya ya fedha kwenye vyama vya siasa?
5) Kama anakubaliana na CAG kwa upande wa vyama vya siasa kwann anapingana nae kwa upande wa Serikali ilihali kuna mawaziri wameanza kutoelea ufafanuzi mapungufu yaliyo tajwa na CAG kwenye wizara zao na wengine wamewafukuza kazi baadhi ya wakurugenzi na kuvunja bodi?
Kuna maswali mengi waandishi walipaswa kumuuliza Polepole...
Anyways bila shaka ripoti hii itajadiliwa bungeni...wabunge wanapaswa kuangalia maslahi ya nchi na kutoa majibu sahihi juu ya hii ripoti ili Watanzania awaendelee kuwa na imani na serikali na chama chetu...
Ni vyema pia kukawa na mijadala ya Kitaifa kujadili kwa uwazi na mapana ripoti hii....
1.5 Trilioni ni hela nyingi sana ni vyema kitendawili hiki kikateguliwa mapema...!