Kumtambulisha Nusrat Hanje kama mwakilishi wa BAVICHA huko Nyamagana ni uongo wa wazi na ni kumdanganya Rais Samia

Kumtambulisha Nusrat Hanje kama mwakilishi wa BAVICHA huko Nyamagana ni uongo wa wazi na ni kumdanganya Rais Samia

Kwanini mnakandamiza haki za binadamu nyie ..huo ndio uhuru wa maoni bwana
 
Kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kumtambulisha Nusrat Hanje kama kiongozi wa Bavicha, na kwamba ule ndio uwakilishi wa vijana wa Chadema kwenye Mkutano wa Rais na Vijana huko Nyamagana Mwanza ni kumpiga changa la macho Mh Rais .BAVICHA haikuhudhuria mkutano huo na wala haikutuma mwakilishi yeyote.

Nusrat Hanje na wenzake 18 walishafukuzwa kwenye uongozi na kuvuliwa uanachama wa Chadema kwa tuhuma za USALITI , Hawa wote kwa ujumla wao hawana uwezo wa kuwakilisha chadema kwenye jambo lolote.

Aliyetangaza jambo hili la uongo alilenga kumdanganya Rais ili ionekane Mkutano ule wa vijana wa CCM na Mwenyekiti wa chama chao ni mkutano wa vijana wote wa Tanzania, wakati si kweli. Napendekeza muongo huyo atumbuliwe haraka ili kunusuru mambo yasiharibike zaidi, ikiwa na ugeni wake Mwanza ameanza na uongo duni kama huu, itakuwaje akiachwa hapo mwaka mzima?
Katika mabinti wa BAVICHA nliokua na matumaini nao ukiacha zainab mudhihir, Dorcas Francis, Upendo peneza, Esther chisanga n.k basi huyu nilimpa marks zaidi lakini amekua disappointment kuliko nilivyotarajia.

Yaani amepinga udhalimu wa CCM kwa miaka 10 alafu leo hii anaingia bungeni kwa endorsement yao? Hvi leo mentor wake; Aplhonce Mawazo akifufuka atajibu nini? Kuna mambo hii nchi yanakera sana.
 
Huyo na wenzake akina Mdee status quo yao kwenye chadema iko pale pale hadi maamuzi ya baraza kuu la chadema litakapokaa na kusikiliza kesi yao na kuitolea maamuzi. Huwezi kuwafukuza kwa kipeperushi na bila hata haki yao ya msingi ya kusikilizwa. Baraza kuu limeshindwa kukaa kwa sababu ya ukapa, sasa nani wa kulaumiwa?
 
Kwaiyo Nusrat kuwakilisha vijana wa Chadema imekuuma sana.
 
Katika mabinti wa BAVICHA nliokua na matumaini nao ukiacha zainab mudhihir, Dorcas Francis, Upendo peneza, Esther chisanga n.k basi huyu nilimpa marks zaidi lakini amekua disappointment kuliko nilivyotarajia.

Yaani amepinga udhalimu wa CCM kwa miaka 10 alafu leo hii anaingia bungeni kwa endorsement yao? Hvi leo mentor wake; Aplhonce Mawazo akifufuka atajibu nini? Kuna mambo hii nchi yanakera sana.
Mimi binafsi katika mabinti wa Bavicha naowaamini na matumaini kwao ni wewe
 
Hivi heshima ya katiba na miongozo ya vyama kwanini inavunjwa mbele ya haraiki.Vyombo vya usalama havioni chuki hii mbele ya Rais
 
Kwakweli sijaelewa mpaka sasa lengo lao lilikua nini kmtambulisha mtu asiekua na chama
 
Back
Top Bottom