Kumtambulisha Nusrat Hanje kama mwakilishi wa BAVICHA huko Nyamagana ni uongo wa wazi na ni kumdanganya Rais Samia

Kumtambulisha Nusrat Hanje kama mwakilishi wa BAVICHA huko Nyamagana ni uongo wa wazi na ni kumdanganya Rais Samia

Kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kumtambulisha Nusrat Hanje kama kiongozi wa Bavicha, na kwamba ule ndio uwakilishi wa vijana wa Chadema kwenye Mkutano wa Rais na Vijana huko Nyamagana Mwanza ni kumpiga changa la macho Mh Rais .BAVICHA haikuhudhuria mkutano huo na wala haikutuma mwakilishi yeyote.

Nusrat Hanje na wenzake 18 walishafukuzwa kwenye uongozi na kuvuliwa uanachama wa Chadema kwa tuhuma za USALITI, hawa wote kwa ujumla wao hawana uwezo wa kuwakilisha chadema kwenye jambo lolote.

Aliyetangaza jambo hili la uongo alilenga kumdanganya Rais ili ionekane Mkutano ule wa vijana wa CCM na Mwenyekiti wa chama chao ni mkutano wa vijana wote wa Tanzania, wakati si kweli. Napendekeza muongo huyo atumbuliwe haraka ili kunusuru mambo yasiharibike zaidi, ikiwa na ugeni wake Mwanza ameanza na uongo duni kama huu, itakuwaje akiachwa hapo mwaka mzima?

View attachment 1819466
Wivu
 
Na ndivyo mtakavyoshangaa mtakaposikia kuwa Mheshimiwa Rais amefanya kikao na wawakilishi wa Chadema wakina Waheshimiwa Halima Mdee, Esther Bulaya, Nusrat Hanje na wengine katika adhma yake ya kukutana na vyama vya upinzani.

Amandla...
 
Mama asirudie mtego wa Mwendezake kudanganywa kuhusu Wapinzani. Haimuongezei sifa yoyote
 
Vijana ndio mngeanzia hapo kwa mbunge asiye na chama,mnadhihirisha hamuaminiki namtauza nchi kwa vipande vya shilingi.
Pambaneni kukemea hilo
 
Kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kumtambulisha Nusrat Hanje kama kiongozi wa Bavicha, na kwamba ule ndio uwakilishi wa vijana wa Chadema kwenye Mkutano wa Rais na Vijana huko Nyamagana Mwanza ni kumpiga changa la macho Mh Rais .BAVICHA haikuhudhuria mkutano huo na wala haikutuma mwakilishi yeyote.

Nusrat Hanje na wenzake 18 walishafukuzwa kwenye uongozi na kuvuliwa uanachama wa Chadema kwa tuhuma za USALITI, hawa wote kwa ujumla wao hawana uwezo wa kuwakilisha chadema kwenye jambo lolote.

Aliyetangaza jambo hili la uongo alilenga kumdanganya Rais ili ionekane Mkutano ule wa vijana wa CCM na Mwenyekiti wa chama chao ni mkutano wa vijana wote wa Tanzania, wakati si kweli. Napendekeza muongo huyo atumbuliwe haraka ili kunusuru mambo yasiharibike zaidi, ikiwa na ugeni wake Mwanza ameanza na uongo duni kama huu, itakuwaje akiachwa hapo mwaka mzima?

View attachment 1819466
Sikuna viongozi wa chadema mwanza na taifa kwanini wasikanushe au kwanini wewe kama wewe usimshitaki aliyejitambulisha?
 
Hatutakubali Chadema itumike kwenye mambo yao ya kijinga
Mjinga ni nani kama siyo wewe unayelalamikia kitu ambacho unatakiwa ukipinge kwa njia ileile iliyotumika sasa unakuja humu ili iweje?usaidiwe nini?
 
Rais bado anaruhusu kudanganywa waziwazi namna hii na hao wanasiasa? awe makini sana na haya mambo - unapofikia kumdanganya Rais wetu ni sawa unaudanganya umma wa watanzania. Huyu dada wa Covid 19 ashatimuliwa uanachama muda sana na hao wenzake 18 !!

Intelligensia ya Rais msiruhusu haya mambo ya kumdanganya Rais - timizeni wajibu wenu.
Ina maana wewe unamjua sana Rais kuliko alionao karibu?
 
Once ukikubali kutumika, utakuwa wa kutumika tu! Heshima yote ambayo Nusrat Hanje aliijenga aliibomoa kwa tumbo lake mwenyewe! Ona sasa anaanza kutumika kuhadaa umma kwa namna ya hovyo kabisa. Nusrat Hanje sio tu kwamba sio BAVICHA, bali sio hata mwanachama wa Chadema. Ona Hanje sasa ameanza kutumika kumchafua mama yetu Samia!
Amemchafua Samia wapi?na tangu lini Samia akawa mama yenu chadema?kwahiyo ccm ni baba yenu?
 
..aliyefanya hivyo atakuwa anaamini Raisi ni MJINGA au DHAIFU.

..tusishangilie tukidhani wanaokomolewa ni Chadema.

..Mama asipochukua hatua ipo siku yatafanyika mengine makubwa yenye madhara kupita hili.
Madhara ya hili ni nini?
 
Katika mabinti wa BAVICHA nliokua na matumaini nao ukiacha zainab mudhihir, Dorcas Francis, Upendo peneza, Esther chisanga n.k basi huyu nilimpa marks zaidi lakini amekua disappointment kuliko nilivyotarajia.

Yaani amepinga udhalimu wa CCM kwa miaka 10 alafu leo hii anaingia bungeni kwa endorsement yao? Hvi leo mentor wake; Aplhonce Mawazo akifufuka atajibu nini? Kuna mambo hii nchi yanakera sana.
Unadhani bado kuna mtu mjinga kama mawazo tena?

Kafa kwaajili ya chadema familia yake inateseka,huyu kajiongeza
 
Back
Top Bottom