Kumtamkia mzazi wako nakupenda kimaadili ya Kitanzania ni utovu wa nidhamu

Hayo ni mambo ya watu nyanyanya, au mrendamrenda!

Sisi wengine mama unamuonesha upendo kwa kumhudumia kwa mahitaji yake muhimu, hilo tu linatosha yeye kujua kuwa unampenda.
 
Siku nikienda mkumbatia mama na kumwambia nakupenda,aisee kwanza siwezi na hata yeye ataona kuna tatizo sehemu atahisi nimelewa walai ataingia maombini kuniombea.
Suala la kuwa nampenda anajua vzr tu.
Kwa mantiki hiyo,jamii yako inawaza ngono sana,wanahisi ukisema nakupend,unataka mzigo[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Kusema nakupend ni neno la kawaida tu, changamoto ni tafsiri

Kifupi ni kuwa neno kupenda katk jamii yenu inatumika ktk issue za kingono pekee hv ni vema usilitumie kwa mzaz wako
 
Umepaniki jomba, usiforce watu wote wafanane na wewe
 
Technically siwezi kumwambia mzazi nakupenda.
Sababu kutokana na malezi yangu it sounds bullshit.

Afrika neno nakupenda kwa asilimia kubwa na kwenye asilimia kubwa ya jamii linaashiria bond ya mapenzi".

Hivyo kumwambia mzazi nakupenda ina sound kama tabia mbaya ukilinganisha mapenzi kwa africa sio neno linaloonekana lina busara.
lakini technically sio tabia mbaya.

Kwa jinsi ninavyowaheshimu wazazi na malezi yangu siwezi kumtamkia mzazi nakupenda.
Na nitashindwa hata kuwaangalia machoni baada ya kutamka hilo neno.

So kinachomatter ni malezi na tamaduni za jamii husika.

Lakini mke wangu yes nitaweza kumwambia nakupenda kila baada ya dk 5 ila kwa watoto nitaendelea kuwa hard rock.

Just imagine unaenda kumwambia baba yako mwenye sura ya jiwe "baba nakupenda" Hapana aisee ukichangia mzee ni mtu wa jeshi.
Lazima akuone umebadirika na kuwa mtu wa ajabu na lazima ahisi hili jamaa limekuwa boya au lina kichaa cha mbwa.

Lakini moyoni kila mzazi anajua jinsi gani unampenda kwa matendo yako na mtoto anajua siku zote jinsi gani anapendwa na mzazi wake.

Imagine even hapa sijisikii comfortable kuandika neno "nakupenda na mapenzi".

Watu wanaolilia mapenzi nawaona hawajakamilika kama binadamu na ni dhaifu.

Seriously it makes me feel Weak.
 
Mama's boy
Sasa unaoa ili iweje,si uendelee kukaa tu kwa mama ndio atakulea vizuri.
Mwanaume familia yako kwanza.
 
unayempenda haitaji kuambiwa, anaona.... hta mm siwez kumwambia mama nakupenda , wajibu wangu ni kumjali kutimiza mahitaji yakw kwa haraka kumjulia hali n.k,kelele za nakupendq ni za watoto
Kwa asili ya binadamu tulivyo neno nakupenda lina umuhimu wake,lina nguvu yake na lina umaalum wake ukilinganisha na matendo.

Ukimwambia mtu nakupenda hawezi kusahau kamwe lakini ukimfanyia matendo matupu kuna uwezekano wa kusahau baadhi ya matendo hayo kwa kufikiri kuwa ni wajibu wako kufanya hayo matendo.
 
Mimi nikienda kijijini naenda na pesa lakini wanakijiji ndugu zangu hawaniambii we love you wananipa vindizi vichache ,vikaranga vichache ,miwa michache ambavyo kwa uwezo wangu naweza nunulia Kijiji but I feel so loved kwa kidogo walichonacho walichonipa kuliko wangeniambia we love you in English !!!

Vimaharage vyao vidogo they speak louder than English word ya We love you!!
 
Sas hbr za kijijini kwenu ndio watu wote wafuate[emoji706][emoji706]
 
Mkuu YEHODAYA umefafanua vema. Kumwambia mzazi wa kiafrika NAKUPENDA sio kosa kisheria ila ni kosa kiutamaduni. Kumkumbatia na kumpiga busu ni hatua nyingine kubwa ya uvunjifu wa maadili. Kwa mfano mababa wa kiafrika hadi kuja kuzoeleka japo kidogo ni ule muda ushamaliza chuo na kuanza kazi. Sasa utaanzaje kumpa hizo pigo za I LOVE YOU DAD?... Sema mleta uzi umechemka sana kusema mama ni namba moja kisha watoto wako halafu mke ni wa mwisho. Huna tofauti na hawa unaowalaumu. Wewe ni MAMA'S BOY.. Namwombea sana huyo shemeji kwa sababu ya kuolewa na mtoto wa mama.
 
Silazimishi African culture I love you is not a word is a deed

Wazungu I love you is a word!!!
Eleza vizuri,unaposema kwa wazungu neno nakupenda ni word unakuw na maana gani?

Pia unaposema kwa waafrika neno nakupenda ni tendo unakuwa na maana gani pia?

Eleza
 
Hapa tunazungumzia mtu kukuambia kuwa 'nakupenda' kwa kiswahili.Akikuambia kwa English huwa haina nguvu sana.
 
Sas hbr za kijijini kwenu ndio watu wote wafuate[emoji706][emoji706]
Ok fuata uzungu me I am an African I am not a photocat of Europeans and I will never be

I believe love is not a word but a deed.Europeans can say any love word but what do they do to Africa Congo etc ndio chaweza amua kusema wazungu wanatupenda au la !!!! Sio kelele za we love Africans or Tanzanians huo ujinga love is a word it is a deed wabakie nao Nchi zao
 
Mkuu nadhani nimekuelewa.

Ni hivi, upendo hudhihirishwa kwa namna mbalimbali. Muhimu ni dhamira ya upendo, na baina yenu muelewe dhamira ya uwasilishaji. Hata hao wazungu unaowasema, kuna jamii nyingine kugusanisha paji la uso ni tendo la heshima na upendo wa hali ya juu, bila hata kutamkiana maneno au kukumbatiana.

Kuna wengine wanaweza kuona uwasilishaji wa upendo wako kwa mama yako una walakini. Aidha, ikiwa wewe na mama yako mnaelewana, hewala. Vivyo hivyo, tuheshimu uwasilishaji wa wengine, ilhali haumuumizi mtu na dhamira yao ni njema.
 
Sas hbr za kijijini kwenu ndio watu wote wafuate[emoji706][emoji706]
I repeat I love you kwa African Tradition is not a word it should first be backed by action first

In Africa The word I love you is not a big word is a stupid word if is not preceeded by love action
 
Mama's boy
Sasa unaoa ili iweje,si uendelee kukaa tu kwa mama ndio atakulea vizuri.
Mwanaume familia yako kwanza.
Unaona sasa?
kila mtu anadhani yupo sahihi sababu ya tofauti ya kimalezi na tamaduni.

Mimi kwangu mama kwanza kwenye kila kitu.

Pia hili neno mtoto wa mama mnalitumia vibaya sababu watoto wote ni wamama au kuna mtu amezaliwa na baba yake humu?
Mtu anayeona kuwa mtoto wa mama ni vibaya basi bila shaka hana akili.

Mimi nasema wewe unaendeshwa na mkeo hivyo ni zoba sababu mwanaume anatakiwa awe na misimamo.

Sasa nani yupo sahihi hapa?

Ndio maana ni vizuri kila mtu kubaki na opinions, perspectives zao.
 
Nakuuliza swali jepesi mkuu nategemea utalijibu?

Wewe hujazaliwa na mama yako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…