Kumtamkia mzazi wako nakupenda kimaadili ya Kitanzania ni utovu wa nidhamu

Hili swali umeuliza ukiwa umevuta bangi? Kuna mtu anayezaliwa bila mama? Fikiri kabla ya kuuliza.
Vizuri.

Sasa kwanini unashangaa na kumuita mtu anayemtanguliza mama yake mbele, "mtoto wa mama".
kama sifa mbaya wakati unajua wazi kila mtu ni mtoto wa mama?

Wewe ni MAMA'S BOY.. Namwombea sana huyo shemeji kwa sababu ya kuolewa na mtoto wa mama.

Sasa jiulize kati ya mimi na wewe nani amevuta bangi na nani anaandika bila kufikiria.
 
Mama yangu huwa namwambia nampenda kila ninapopata nafasi ya kufanya hivo, huwa nawaza siku akiondoka duniani sitapata tena nafasi ya kumwambia kuwa nampenda.

Sent from my Infinix X606D using JamiiForums mobile app
 
Siku nikienda mkumbatia mama na kumwambia nakupenda,aisee kwanza siwezi na hata yeye ataona kuna tatizo sehemu atahisi nimelewa walai ataingia maombini kuniombea.
Suala la kuwa nampenda anajua vzr tu.
ni kweli kka na mada yangu nazungumzia mwanaume kwa mama au binti kwa baba ila wamenielewa tofaut

Sent using Jamii Forums mobile app
 
blessed mkuu kwa kweli utakuta toto kila siku ilove you mama cha ajabu hata likitumwa kidogo lianakataa which kind of love portrayed here

Sent using Jamii Forums mobile app
 
to be honestly nipo tayari kuitwa mtoto wa mama maana pia kiasili sio tusi bali ndo ilivyo, ninaamini bila wazazi nisingekuwepo leo itakuwa ngumu kuniaminisha kuwa mke ni mhimu kuliko mzazi kwa hilo kwangu sitakaa nibadilike hata siku moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ninahisi alieandika ni mwanamke labda tu nitoe rai kuwa mke wangu ni ruksa kumpenda mama yake kuliko mimi au kuliko ndugu zangu wala simuingilii kwa hilo maana mimi binafsi tumekutana ukubwani sjui profile yoyote aliyopitia na wazazi wake, kwa hiyo hilo na kwangu hata ikitokea mwanamke aniulize pengine kwa kujaribu au kwa kumaanisha kuwa yeye na mama yangu ninampenda nani nadhani hapohapo ndio nitamuandikia majibu ambayo ni talaka 5 hata kama hazipo ila yeye nitaztoa kwa mara ya kwanza, huwezi kumtanguliza mke ambae mmekutana ukubwani na kumuacha mama yako ambae amekuzaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni tatizo la mtazamo Tu.

Binafsi, sioni ubaya kumhug mama yangu na hata kumkiss.

Mitazamo tofauti huifanya dunia iendelee kuishi.
 
Mkuu ni kawaida kwa watoto wa kiume kuwapenda mama zao kuliko hata wake zao, wanawake wanawapenda kaka zao kuliko hata wapenzi walonao! wahenga walisema mke wako sio ndugu yako, ila watoto wako ndo ndugu zako. Walisema hivo ili kuziokoa nyoyo za wanaume.
 
Hata mimi siwez mwambia hayo mambo.Sio yeye tu hata dada zangu na watoto wangu wa kike siwez kufanya huo upumbavu.Ila wataona kwa vitendo tu
Safi kabisa! Nami, kama wewe, naungana na mtoa mada. Mimi hata kula sahani moja na dada zangu au mama siwezi aisee. Utaratibu wetu ni kuwa ndugu wa kiume wanaweza kula na ndg wa kiume wenzao na wa kike wanaungana na wa kike wenzao. Kutofanya hivyo ndo mwishowe tunayaona haya tunayoyaona.......watoto wa kiume wanafikia hatua ya kutwerk, wanafanya twerking!!!!!!
 
Mimi hapa ndio huwa mnanichanganya sana....! Unamlinganishaje mke na mama?? Yaani ni kama ulinganishe meli na treni vyote ni vyombo vya Usafiri ila kamwe huwezi kuviweka katika mizani sawa....! Ukianza habari za kuanza kuwalinganisha mama na mke lazima maisha ya kijamii yatakushinda tu....! Maana unalinganisha watu ambao hawawezi kuwa sawa kamwe.

Hata biblia imeagiza. "Waheshimu baba na mama ili upate heri Duniani " kwa hiyo kumbe wazazi wanahitaji sana heshima kutoka kwetu....! Mama kukuzaa na kukulea huo ni wajibu wake, hivyo na ww timiza wajibu wako wakumuheshimu.

Mke biblia imetuagiza. "Wanaume tuwapende wake zetu" kwa hiyo kumbe mke wako anahitaji upendo wako....!

Kwa mantiki hiyo ukiangalia mahitaji ya hao watu wawili ni tofauti kabisa. Mke anahitaji upendo, mama anahitaji heshima. Hawa watu kamwe huwezi kuwalinganisha

Sasa ukitokea umejichanganya mahitaji ya mke wewe unampa mama yako, hapo lazima uvurugwe sio kidogo....! Kwa sasa unaweza usione madhara lakini kwa baadae lazima uje kuona madhara yake...! Na yatakutafuna kweli kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…