Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari wakuu,
Tangu awali nilishasea huu uzungu na haya maisha ya watoto wa kishua sijui wanampango gani na vizazi vyetu,
Siku moja kuna star mmoja na mchekeshaji maarufu alifiwa na mama yake mzazi sasa jamaa alishinda akipost video alivyokuwa anaishi na mama yake mara wabusiane mara wakumbatiane mara walishane yaani hadi nilikuwa nikitazama zile video binafsi moyo unalipuka kwa kweli kwa hili mimi nitabaki kuwa mshamba kama ushamba wenyewe ndio huo basi nipo tayari kuvishwa taji la ushamba.
Mimi binafsi nimekuwa katika mazingira ya kijijini sikuwahi kuona mtu mzima kijana akimpakata mama yake au akimkumbatia mama yake na kumbusu huu ni ujinga na kukosa heshima. Hawa watoto wa mboga saba sikui akili zao huwa ziko wapi, wao wanaamini kumpenda mzazi wako ni kumbeba kumbusu na kumkumbatia kumwambia nakupenda mama kweli?
Mimi binafsi kidume wa mkoani nililelewa na single mother alinisomesha kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu, Na hadi sasa mama yangu anajua ni kiasi gani namjali sipendi niskie hata akiwa na maumivu kidogo nipo tayari kufanya lolote ili mama yangu abaki kuwa salama, nikipata hata 100 nataman nitakachokula na yeye ale hichohicho. namjali mama kuliko kitu chochote kile hapa duniani. viapumbele vyangu katika maisha ni mama yangu kwanza kisha wanafuata wanangu na anafuatia mke wangu, maana pasipo kuwa yy nisingekuwepo mimi hao watoto nisingepata wala mke. Ila kwa upendo wote huo sijawahi kumtamkia mama NAKUPENDA, wala kumkukumbatia and never ever haitakaa itokee neno NAKUPENDA huwa likinijia kichwani Huwa nachukua NOTE ya elfu 10 au 20 nampa namwambia mama hii katoe sadaka kanisani, maana ninajua mama yangu addiction yake ni kanisa tu hana mambo mengine,
Cha ajabu hawa watoto waliokulia mboga saba wanawakumbatia mama zao na kuwakiss eti ndio upendo, SHUBAMIT siwezi kufanya huo ukafili mama ni mama lazima mipaka iwepo.
neno hili tunalolitumia kila siku kwa madem na malaya ?? mm sijawah kumwambia mama yangu nakupenda, wala sijawah kumtamkia mtoto wangu nakupenda lkn hawajawah kuwa na doubt na upendo wangu kwao, nadhani hawahitaji hili neno ili waprove kama nawapenda.Kwa asili ya binadamu tulivyo neno nakupenda lina umuhimu wake,lina nguvu yake na lina umaalum wake ukilinganisha na matendo.
Ukimwambia mtu nakupenda hawezi kusahau kamwe lakini ukimfanyia matendo matupu kuna uwezekano wa kusahau baadhi ya matendo hayo kwa kufikiri kuwa ni wajibu wako kufanya hayo matendo.
Vitabu vya dini vinavyotamka uwe unabweka ohhh nakupenda nakupenda Mungu? Ni vitabu vipi?Then maadili ya Kitanzania ni ya Kipumbavu maana vitabu vyote vya dini vyatutaka tufanye hivyo
Vitabu vya dini vinavyotamka uwe unabweka ohhh nakupenda nakupenda Mungu? Ni vitabu vipi?
Biblia yenyewe inatamka wazi kabisa Yesu alisema kama mwanipenda mtazishika Amri zangu kwenye Yohana 14:15
Yesu mwenyewe na Mungu hawapendi kwa Maneno matupu ni kwa kushika Amri zao na maamrisho yao
Take noteSiwezi kukujibu maana you are not exposed to facts enough to understand , upo sahihi for your level of understanding....
Nilivyomuelewa mwandishi Ni kwamba 'parents need real love only, and not emotional love.'Acheni ungese kwani ukimkumbatia na kumpiga busu mama yako mnakuwa tayari mmeshatomb@n@?
Acheni mawazo ya kimasikini.
Siku mama yako akifa utatamani hata uende ukamkumbatie mbuzi na umpige busu.
Onesha upendo wako kwa namna unayoona inafaa kwako.
Kabisa mkuu, tunasahau kwambaSiku nikienda mkumbatia mama na kumwambia nakupenda,aisee kwanza siwezi na hata yeye ataona kuna tatizo sehemu atahisi nimelewa walai ataingia maombini kuniombea.
Suala la kuwa nampenda anajua vzr tu.
Niliwahi kumwambia mama mmoja ' nakupenda' , hakuwa mama yangu,Yani mama yangu nisimwambie nampenda? Ni vile tu hayupo ila hakuna kimfaacho kingekuwa kinapita katika macho yangu nisimnunulie[emoji28]!!!
Yes i mean it,,,i love my moms [emoji41][emoji41][emoji41] you may call it whatever nitamuonesha upendo wote hata kumbusu shavuni na kumkumbatia cause she deserve that kwa ujasiri wa kunibeba na kunilea toka nikiwa sijitambui.
Mke ni mpenzi tu ambaye tumekutana ukubwani ni patner katika maisha ya hapa duniani ila hatuna bond kama ya mzazi [emoji28] wangu wewe! Hata watoto tutakaozaa watampenda sana yeye sababu wana bond isiyofutika! Hilo nalitambua ndio maana natafta pesa!
Yaani kumkubatia tu mama yako ndio dushe lisimame na kuwaza ngono?Nilivyomuelewa mwandishi Ni kwamba 'parents need real love only, and not emotional love.'
May be because emotional love mara nyingi husababisha sex organs excitement, hivyo mwandishi anaona ajiepushe na dhambi ya ku - excite organs zake mbele ya mzazi au yeyote anaemheshimu Kama mzazi,
na pengine kwa mwanaume mwenzio Kama rafiki, Kaka nk.
But to wives and the likes you can either give emotional love, real love or both..
Aiseee mkuuu, nimekuelewa,neno hili tunalolitumia kila siku kwa madem na malaya ?? mm sijawah kumwambia mama yangu nakupenda, wala sijawah kumtamkia mtoto wangu nakupenda lkn hawajawah kuwa na doubt na upendo wangu kwao, nadhani hawahitaji hili neno ili waprove kama nawapenda.
duh mkuu hata sijui naanzaje kutamka huo utopolo asee mama anaweza kufunga mwaka bila kula akinipigia maombi na vile mama ni mtu wa dini hapa lazima hilo pepo la kizungu linakimbia jenyeweYaan nimwambie bi mkubwa nakupenda? Anaweza hata nirushia kipande cha ukuni pembeni yake kikaniumiza. "Hebu ntolee ujinga hapa kenge wee" (in my mama voice).
kuna namna Una matatizo; jaribu kuongea na watu wa karibu unaowaamini wakusaidie.Take note
You are not allowed to tell me or my family members ohhh I love you.Tell yourself and your family