Kumtisha Samia, ni kumtishia mtu mzima nyau!

Kumtisha Samia, ni kumtishia mtu mzima nyau!

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Huu ni ukweli mchungu ambao hata kama kuna watu hawaupendi, itabidi wauvumilie mpaka 2030!

Tusimung'unye maneno, Samia urais anautataka, na amewekeza kuhakikisha anaupata!

Kwenye siasa hakuna bahati mbaya! Kilichotokea kwenye mkutano mkuu, hakikuwa bahati mbaya! Ulikuwa ni mkakati uliopangwa na kuratibiwa kwa uangalifu.

Kwa walioutazama mkutano mkuu, mtoa hoja, ndugu Lusinde alikuwa kakaa karibu na Nchengelwa, na hoja ilipotolewa, mwongozo ulitolewa JK, mnadhani hii ilikuwa bahati mbaya?

Itakumbukwa huko nyuma ilishaamuliwa hawa wazee wastaafu kutoshiriki vikao vya chama, likaundwa baraza la wazee, kuwa jukwaa lao la kutoa ushauri kwenye chama. Mnadhani JK kuhudhuria mkutano huu ilikuwa bahati mbaya?

As of now, Samia ana dola, ni mwenyekiti wa chama na ana endorsement ya chama, anahitaji nini tena kuifikia ndoto yake ya urais? Hapo alipo ana mtaji wa kura 13M za wana CCM, hata akina Polepole walale wanagalagala mwenzao ashajihakikishia ushindi.

Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu haswa ndani ya CCM, kama haridhiki na uteuzi wa Samia, ushauri wa bure ni akae kimya kunusuru future yake kwenye siasa. Maana kwa hali ilivyosasa, anachosubiri Samia ni kuapishwa tu.
 
Back
Top Bottom