Uhuru usio na mipaka ni uhaini.
Kuna kundi la wanasiasa, wanasheria, na baadhi ya viongozi wa dini,wanaojiita wanaharati wamegeuza uhuru wao wa kutoa maoni na kuwa jukwaa la kutoa matusi na kijaribu kumdhalilisha mh. Raisi.
Ninaomba mamlaka husika ziingilie kati na kuwachukulia hatua wanaotoa matusi Kwa kisingizio Cha kutoa maoni. Pia vyombo vya habari na mitandao ambavyo huandika matusi vipelekwe Baraza la habari kujieleza.
Watu watoe maoni bila kumtukuna mtu. Narudia uhuru usio na mipaka ni utumwa.
Sisi pia ni wananchi Tunakuomba Mh Rais chukua hatua kwa wanaokutusi najua hua unapitia hapa ni matumaini yangu tutaona hatua zikichukuliwa kwa haraka.
cc waziri wa mambo ya ndani
cc IGP
cc waziri wa habari
Ukikataza rais kutukanwa hadharani, unaukaribisha mipango ya kumuua rais kwa siri.
Usifikiri nchi zilizoendelea ni wajinga kuweka uhuru mkubwa wa kutukana viongozi.
Usifikiri wameweka uhuru huo kwa sababu wanapenda tu watu kuwa huru.
Uhuru huo umewekwa kwa falsafa kubwa.
Watu waliopewa uhuru wa kuongea, mara nyingi hupata nafasi ya ku let off steam kwa kuongea, hawaendi kufanya mapinduzi ya nguvu. Wanatumia njia za kidiplomasia za mazungumzo zaidi.
Watu wanaonyimwa uhuru wa kuongea huishia kupanga mipango ya kupindua serikali na kuua viongozi.
Na kadiri serikali inavyominya uhuru wa kujieleza, ndivyo inavyozidi kujizuia yenyewe kwenye vyanzo vya kupata habari kuhusu mipango dhidi yake.
Leo hii ukienda Clubhouse watu wa upinzani na wanaharakati wana uhuru wa kuongea, wanaongea mpaka wanajisahau wanapanga mikakati yao nyeti online, mpaka ma shushushu wa serikali wanawasikiliza.
Serikali ikifungia Clubhouse, hata majasusi wa serikali na wapelelezi wa polisi watakosa chanzo hicho cha habari kwao.
Kwa hivyo, unaweza kuona kufungia uhuru wa kujieleza ni jambo zuri katika kuendeleza order, lakini kwa kweli, in a very counterintuitive way, ukifungia uhuru wa kujieleza, unainyima hata serikali nafasi ya kujua kinachoendelea.
Usiwaone Wamarekani na Waingereza ni wajinga kwa kuruhusu uhuru wa kujueleza na kumtukana rais sana bila hofu.
Wanajua wanachofanya.
They are olaying the long game.
They are playing chess, not checkers.
Lese-Msjeste laws are an indult to press freedom and freedom of expression.
View attachment 2682727