Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,809
- 6,948
Inahitaji akili ya ziada kung'amua kuwa alichokisema na anachokifanya Mbunge wa Kawe Josephat Gwajima ni "high level propaganda" yenye nia ya kuwalinda wale wale anaoonekana kuwatuhumu.
Mara ngapi inapotokea hali fulani ambayo haina taswira nzuri kwa serikali unasikia mtu anasema "Rais kuna watu wako wa karibu wanakuchafua" na maneno kama hayo. Hapa nia ni kumuondoa Rais na lawama za kile ambacho watu hawapendezwi nacho bila kumuwajibisha. Hiki hakina tofauti na alichokifanya Gwajima.
Kusema kuna kakikundi kanakojitegemea kanakofanya utekaji halafu unasema hakihusiani na vyombo husika ni njia ya kuwatakasa wahusika na kuwaondoa katika lawama ya kile kinachoendelea.
Niliwahi kusema CCM walichoamua kufanya muda mrefu uliopita ili kusalia madarakani ni kuhakikisha wapo kila upande wa shilingi katika mada yoyote, nyanja yoyote na sekta yoyote. Watakuwa CCM lakini pia watakuwa vyama vya upinzani. Watakuwa Yanga lakini pia watakuwa Simba. Watammiliki Diamond lakini pia watammiliki Alikiba. Wataongoza serikali lakini pia wataongoza vyama vya wafanyakazi. Wanahakikisha wanaopingana ni watu wao wenyewe. Hata pale yanapoonekana mabishano na ushindani ni mkali, hii inakuwa rahisi ku "control outcome". Kama suala linaenda "out of control", wanatumia watu hao hao kulimaliza na chama kinabaki salama.
Hiki ndicho kinachotokea kwa Gwajima.
Watu wasiojulikana wametakaswa na wataendelea kutojulikana. Kazi yao inataka wasijulikane, kuna nini cha ajabu?