Kumuamini Askofu Gwajima ni kutopevuka kisiasa na kuuzwa kirahisi katika propaganda

Kumuamini Askofu Gwajima ni kutopevuka kisiasa na kuuzwa kirahisi katika propaganda

Fulsa ya wanayoitumia CCM ni ileile waliyoisoma kwa kipindi kirefu kuwa sisi ni mabingwa wa kujizima data kusahau kila kilichopita.
Ndio maana leo hii wapo wengi wasemao kuwa "Gwajima ana madudu mengi ila kwa hili tunasafiri nae"
Wakasahau kimya chake cha kipindi cha risasi za Lisu pia tukajisahaulisha mkakati wa lowasa kuletwa CDM na athari kubwa iliyopatikana ya watu kutoamini wanasiasa kwa kuwakatisha tamaa mtu walokampa matumaini kwa kupita njia iliyoaminiwa ya CDM.
Haitoshi tukasahau mkakati wa mzee MEMBE na ACT hata kama haikuleta athari kubwa ila marudio ya MEMBE kurudi kwao ccm pia ilikuwa ni fulsa kuwafungua WATZ kujua ni namna gani ccm inacheza na akili zetu.

Mfano wa hili la juzi kesi ya Lisu inakaribia kwenda mahakamani ghafla linaibuka la Gwajima na kilichojiri ni kile asubuhi yake kwenye Front page za magazeti yanayowekwa kipaombele ni KUFUNGIWA KWA KANISA tena uandishi ukafanana as if mhariri ni mmoja utabaini kabisa huu ni mkakati.
Kinachofuata kutekelezwa mikakati yao ni pale siku ya kesi ya Lisu ilipopangwa tar. 16 wao wakaweka mechi ya dabi ni tar. 15 hii ni kwa nini..
Ni kwasababu inafahamika wazi baada ya matokeo ya mechi hiyo asubuhi yake ni mijadala tu vijiweni kuhusu mechi ya jana yake ni wachache mno wenye kufuatilia hayo mambo ya kesi.
Hapo ndo chama tawala wamepashika vizuri.

Nimalize kwa kusema kumwamini muongo eti kwa kuwa kasema kweli ni sawa na kuinywa sumu iliyopakwa rangi nyeupe ukaaminishwa maziwa.
Ilitosha kusimama na maneno ya akina heche, kitima, Ponda na mfano wa hao ila kwa huyo jamaa wa misukule wa mchongo hapana kwa kweli.

GWAJ B HATA AKISEMA ILE NI BAHARI YAPASWA UKAHAKIKI OTHERWISE LITAKUWA DIMBWI
 
Watz hatutaki Imani Kwa mtu yeyote!!coz mtu aweza disappoint wakati wowote ule!!
Tunataka tuuamini mfumo ambao unaweza simamia yeyote yule bila kujali anatoka chama gani!!!

Kuwekeza Imani Kwa MTU ni kufeli Kwa ubongo kufikiri !tunataka mfumo ndio umuendeshe kiongozi!!

Sasa !!?

Hata kama Gwajima haaminiki ndio jeshi la polisi lizunguke kanisa na vyombo vya moto na mabomu ya machozi !!?Lina pambana na nani!!?alshabaab!!?alqaida!!?

TUMIA UBONGO WAKO SAWA SAWA!!
 
Inahitaji akili ya ziada kung'amua kuwa alichokisema na anachokifanya Mbunge wa Kawe Josephat Gwajima ni "high level propaganda" yenye nia ya kuwalinda wale wale anaoonekana kuwatuhumu.

Mara ngapi inapotokea hali fulani ambayo haina taswira nzuri kwa serikali unasikia mtu anasema "Rais kuna watu wako wa karibu wanakuchafua" na maneno kama hayo. Hapa nia ni kumuondoa Rais na lawama za kile ambacho watu hawapendezwi nacho bila kumuwajibisha. Hiki hakina tofauti na alichokifanya Gwajima.

Kusema kuna kakikundi kanakojitegemea kanakofanya utekaji halafu unasema hakihusiani na vyombo husika ni njia ya kuwatakasa wahusika na kuwaondoa katika lawama ya kile kinachoendelea.

Niliwahi kusema CCM walichoamua kufanya muda mrefu uliopita ili kusalia madarakani ni kuhakikisha wapo kila upande wa shilingi katika mada yoyote, nyanja yoyote na sekta yoyote. Watakuwa CCM lakini pia watakuwa vyama vya upinzani. Watakuwa Yanga lakini pia watakuwa Simba. Watammiliki Diamond lakini pia watammiliki Alikiba. Wataongoza serikali lakini pia wataongoza vyama vya wafanyakazi. Wanahakikisha wanaopingana ni watu wao wenyewe. Hata pale yanapoonekana mabishano na ushindani ni mkali, hii inakuwa rahisi ku "control outcome". Kama suala linaenda "out of control", wanatumia watu hao hao kulimaliza na chama kinabaki salama.

Hiki ndicho kinachotokea kwa Gwajima.

Watu wasiojulikana wametakaswa na wataendelea kutojulikana. Kazi yao inataka wasijulikane, kuna nini cha ajabu?
Huna akili ya kuelewa alichoongea Gwajima, upeo wako ni mdogo san kumuelewa ni kheri ukae kimya usubiri chakula cha Wazazi ule kesho uende Shule na nadhani mnafunga Shule trh06/06/2025
 
Hao wabunge wengine wamefanya kitu gani?
Mimi nilizungumzia jimbo letu la Kawe. Hao wabunge wengine watazungumziwa katika majimbo yao.
 

Attachments

  • Screenshot_20250530_153435_Chrome.jpg
    Screenshot_20250530_153435_Chrome.jpg
    301.9 KB · Views: 24
Fulsa ya wanayoitumia CCM ni ileile waliyoisoma kwa kipindi kirefu kuwa sisi ni mabingwa wa kujizima data kusahau kila kilichopita.
Ndio maana leo hii wapo wengi wasemao kuwa "Gwajima ana madudu mengi ila kwa hili tunasafiri nae"
Wakasahau kimya chake cha kipindi cha risasi za Lisu pia tukajisahaulisha mkakati wa lowasa kuletwa CDM na athari kubwa iliyopatikana ya watu kutoamini wanasiasa kwa kuwakatisha tamaa mtu walokampa matumaini kwa kupita njia iliyoaminiwa ya CDM.
Haitoshi tukasahau mkakati wa mzee MEMBE na ACT hata kama haikuleta athari kubwa ila marudio ya MEMBE kurudi kwao ccm pia ilikuwa ni fulsa kuwafungua WATZ kujua ni namna gani ccm inacheza na akili zetu.

Mfano wa hili la juzi kesi ya Lisu inakaribia kwenda mahakamani ghafla linaibuka la Gwajima na kilichojiri ni kile asubuhi yake kwenye Front page za magazeti yanayowekwa kipaombele ni KUFUNGIWA KWA KANISA tena uandishi ukafanana as if mhariri ni mmoja utabaini kabisa huu ni mkakati.
Kinachofuata kutekelezwa mikakati yao ni pale siku ya kesi ya Lisu ilipopangwa tar. 16 wao wakaweka mechi ya dabi ni tar. 15 hii ni kwa nini..
Ni kwasababu inafahamika wazi baada ya matokeo ya mechi hiyo asubuhi yake ni mijadala tu vijiweni kuhusu mechi ya jana yake ni wachache mno wenye kufuatilia hayo mambo ya kesi.
Hapo ndo chama tawala wamepashika vizuri.

Nimalize kwa kusema kumwamini muongo eti kwa kuwa kasema kweli ni sawa na kuinywa sumu iliyopakwa rangi nyeupe ukaaminishwa maziwa.
Ilitosha kusimama na maneno ya akina heche, kitima, Ponda na mfano wa hao ila kwa huyo jamaa wa misukule wa mchongo hapana kwa kweli.

GWAJ B HATA AKISEMA ILE NI BAHARI YAPASWA UKAHAKIKI OTHERWISE LITAKUWA DIMBWI
Sahihi kabisa. Sakata la derby lilipangwa kimkakati sana. Lissu kuja kutoka ni miaka 4 ijayo maana tunazubaishwa na mambo mengi sana.

Inasikitisha sana.
 
Watz hatutaki Imani Kwa mtu yeyote!!coz mtu aweza disappoint wakati wowote ule!!
Tunataka tuuamini mfumo ambao unaweza simamia yeyote yule bila kujali anatoka chama gani!!!

Kuwekeza Imani Kwa MTU ni kufeli Kwa ubongo kufikiri !tunataka mfumo ndio umuendeshe kiongozi!!

Sasa !!?

Hata kama Gwajima haaminiki ndio jeshi la polisi lizunguke kanisa na vyombo vya moto na mabomu ya machozi !!?Lina pambana na nani!!?alshabaab!!?alqaida!!?

TUMIA UBONGO WAKO SAWA SAWA!!
Sioni nilipogusa ufungaji wa kanisa.
Nimestick kwa Gwajima kama Gwajima sio kanisa lake labda urudie kusoma kilichoandikwa.

Pia hoja ya kuamini mfumo sahihi na sio chama fulani.
Mimi ni moja ya waTZ wanaotamani hicho kitu ndio maana sikubaliani na vyama vya siasa vyoooote kwa kuwa wengi wao hawaishi kwenye kauli zao bali ni kututumia kama njia za kushika dola na kuyafanya wanayoyataka wao.
 
Narudia tena, hawa watu wengine wametumwa ili hali ikienda out of control, wapate "soft landing"

CCM haina dhamira ya kujenga taifa la haki na kufuata misingi ya demokrasia. Kama dhamira haipo, mengine yote ni kazi bure na upotevu zaidi wa pesa tu.

Gwajima anawakingia kifua watendaji wa vyombo eti "wakisema watafukuzwa kazi", halafu bado anawaita "competent" utadhani maana ya kuwa competent imebadilika.

Eti anasema Rais aendelee kuwateua ila asiweze kuwafukuza kirahisi bila idhini ya kamati ya Bunge. Wakati huo huo, Bunge lenyewe wamelichafua limekuwa kibogoyo.
 
Back
Top Bottom