Big "NO..."
Mimi sikubaliani na wewe...
Safari hii tunakwenda kupata majibu, shetani aliyeikalia Tanzania ameshindwa, amepigwaaa....
Mch. Josephat M. Gwajima ni mtumishi wa Mungu na Yesu Kristo kamili na wa kweli. Nimempima kwenye vipimo vya Neno la Mungu, amethitibika, maana imeandikwa "...
mtawatambua kwa matendo na matunda yao..."
Huyu:
➡Si Mwalimu wa uongo
➡Si Mchungaji wa uongo
➡Si Nabii wa uongo
➡Si Mtume wa uongo
➡And above all, huyu si tapeli wa kidini kama unavyotaka kutuaminisha hapa.
Rafiki ndugu
Keynez, fanya homework yako ya kutafsiri mambo ktk muktadha wa ulimwengu wa roho vizuri...
Na nakuambia jambo moja, kuwa, wakati wa kila mtu kujua ni kwanini huyu mtumishi wa Mungu aliye hai - Mch. Josephat Gwajima aliamua kuingia kwenye siasa na kupata nafasi ya uongozi wa kisiasa (ubunge) tena kupitia chama chenye tuhuma na shutuma za uchafu mwingi - CCM, basi majira ya kupata majibu yake ni sasa....
Mungu Yehova ana njia zake tofauti kabisa na za wanadamu za kufanya mambo yake...
Na Mungu hutumia watu usioweza kuwadhania na njia zisizoweza kueleweka kirahisi kwa wenye hekima ya dunia ktk kutimiza kusudi lake lolote kwa wanadamu...
Nani aliyedhaniaga kwamba yule Rahabu - kahaba wa kwenye Biblia ambaye kila mtu alimuonaga ni mchafu asiye na maadili ya kingono, kwamba Mungu angemtumia huyohuyo kuwa sehemu ya kina mama waliomleta Yesu Kristo duniani na kuukomboa ulimwengu...?
Bila shaka huijui vyema historia ya Mch. Josephat Gwajima alikotoka na mpaka hapo alipo...!
Na kwa taarifa yako, hata huyu mama (Bi Samia) alifanywa na Mungu mwenyewe Rais wa nchi hii ili aikamilishe njia ya uharibifu na anguko la utawala wa CCM wa miaka karibu 64 sasa...
Haya ndiyo majira na nyakati zake. Ukombozi wa Tanganyika umefika
You just wait and see...