Kumuenzi Baba wa Taifa: CCM, Serikali, Viongozi na Watanzania kwa Ujumla. Je, tunamuenzi kwa Mawazo, Maneno na kwa Vitendo? Tunamuishi?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995

Karibuni tena kwenye makala zangu za “Kwa Maslahi kwa Taifa”, zinazozungumzia mada mbalimbali kuhusu taifa letu ziwe ni za kisiasa, za kiuchumi au za Kijamii, baada ya leo ni kuhusu kumuenzi Mwalimu Nyerere, kwa vile Tarehe 14 October ni Nyerere Day, leo naomba tutafakari jinsi sisi Watanzania, tunavyo muenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, jee tunamuenzi kweli, kwa mawazo maneno na matendo?,

Mwalimu Nyerere sio tuu alikuwa ni muasisi wa CCM, mpaka kifo chake aliiamini CCM, hivyo hata baada ya nchi Tanzania, kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa ile 1992, bado Mwalimu aliamini kuwa Wapinzani wanaweza kuleta wabunge bora, na hili tumelishuhudia kwa baadhi ya wabunge wa upinzani,walikuwa ni wabunge bora kabisa, lakini kwenye uraisi wa JMT, Mwalimu Nyerere aliamini “Rais bora atatoka CCM pekee”. Jee kuna Wana CCM wanao maishi Baba wa Taifa kwa mawazo, maneno na matendo?, ama watu tunamuenzi Mwalimu kwa mawazo na maneno tuu, lakini matendo na kumuishi....!.

Mimi ni mtu wa mastory mastory, yaani ni story teller, hivyo kama wewe sio mtu wa mastory story, katishia hapa, nenda mwisho, wale wa mastory mastory, tuendelee...

Jinsi Nilivyo Mfahamu Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Baada ya sekondari nikajiunga na chuo cha Uandishi habari TSJ, ndipo Jumapili moja asubuhi, nikaja kuamshwa na mlinzi wa hostel, kuna nina mgeni!, si unajua tena mambo ya ujana, na hostel, ukisikia tuu una ugeni basi unajua ni ugeni wa type gani, ila asubuhi, tena Jumapili, asubuhi ni hatari!, kunaweza kutokea ajali!.

Kufika nikakuta jamaa fulani mweupe ana bonge la afro na gari sports car nyekundu na kujitambulisha Mimi ni Madaraka Nyerere, mtoto wa Nyerere, anahitajika Msasani kwa Nyerere!.

Naomba niishie hapa, tukutane wiki ijayo mjue niliitiwa nini Msasani kwa Nyerere?, Jee nilikwenda?, Nilimuona Mwalimu Nyerere?.

Nawatakia Nyerere Day Njema.

Paskali.
 
Paskali, nimependa uandishi wako, kweli wewe ulisoma Vipaji, Jamaa wa kijani nimegundua leo ndy saababu hawatakupa uteuzi asilani, sababu ziko mbili ila sitaztaja hapa, moja umeitaja hapa nyingine ni kwa utashi wangu ila Ni ya ukweli. MAYALA KULE KWETU NI NJAA? mimi sikubaliani na usemi ule!!
 
Tunamuenzi kwa maneno lakini kumuishi hiyo ni sifuri bin sifur !!
 
Nyerere muumini wa ujamaa wenye ujima, mwanae anaendesha sport car miaka hiyo mmmmm, kuna kipindi nilifiatuliaga sana blog yake pale Butiama kwa sasa ni No
 
tumuenzi na kula ugali wa yanga tumuenzi kwa kugawiwa dawa ya mswaki 1 kila kaya tumuenzi kwa kupewa sabuni ya kuogea 1 na sukari kilo1 kila kaya tumuenzi kwa uhujumu uchumi tumuenzi kwa kutaifisha majumba ya watu
 
Mtu mkweli huwa hapendwi !!
 
tumuenzi na kula ugali wa yanga tumuenzi kwa kugawiwa dawa ya mswaki 1 kila kaya tumuenzi kwa kupewa sabuni ya kuogea 1 na sukari kilo1 kila kaya tumuenzi kwa uhujumu uchumi tumuenzi kwa kutaifisha majumba ya watu
Tumuenzi pia kwa kutufanya wamoja na tumuenzi kwa kusoma bure na kupewa kila kitu bure huko mashuleni mpaka na warrants za kusafiria za return !! Na pia pamoja na yote watu walikuwa wakiishi kwa furaha bila stress yeyote ile !! Peace of mind ilikuwa imetamalaki !! Kulikuwa hakuna panya rodi wala panya buku. !!
 
Mwalimu alikuwa Binadamu sio Malaika,ataenziwa kwa Yale mema na sio kila mawazo yake basi yanafaa zama hizi..

Mfano falsafa yake ya Uchumi ilishindwa kipindi kile na Sasa haiwezekani..

Ila Kwa neno la umoja tutamuenzi daima.
 
Wanabodi,
Kwa maslahi ya Taifa Jumapili hii

Karibu tena, kwenye makala nyingine ya “Kwa Maslahi kwa Taifa”, leo hii ni makala mwendelezo iliyoanzia wiki iliyopita, Kumuenzi Baba wa Taifa:CCM, Serikali, Viongozi na Watanzania kwa Ujumla, Je Tunamuenzi Baba wa Taifa kwa Mawazo, Maneno na kwa Vitendo?, Tunamuishi?. ikizungumzia kumuenzi muasisi wa taifa hili, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kufuatia kumbukizi ya Baba wa Taifa kila Tarehe 14 October ni Nyerere Day, nikitafakari jinsi sisi Watanzania, Viongozi wetu na Chama chake CCM, tunavyo muenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, na kuuliza tumuenzi vipi Baba wa Taifa?. Jee tuendelee lumuenzi kwa mawazo mazuri tuu na kwa maneno tuu, kwa kupiga blah blah, "Mwalimu alikuwa hivi, Mwalimu alikuwa vile", au sasa tumuenzi kwa matendo kwa kuendelea kutenda kama Mwalimu, na ikiwezekana viongozi wetu wamuenzi Mwalimu kwa kumuishi!, na sio kwa hizi blah blah zinazoendelea sasa?.

Ukiondoa baadhi ya wazee wetu kama kina Ibrahim Kaduma na David Wakati waliotangulia mbele ya haki ambao walimuishi Mwalimu, na wachache waliobakia kama Mzee Joseph Warioba na Mzee Butiku, ni kiongozi gani mwingine yeyote aliye madarakani sasa ana muishi Mwalimu Nyerere?. John Pombe Magufuli angalau angalau Magufuli kama Nyerere: Ni mtu wa watu, hapapasi, hamung'unyi, ni kazi tuu, ila pia sio kama Nyerere!

Mimi ni mtu wa mastori story, hii simulizi ya Mwalimu, niliianza wiki iliyopita na niliishia nikiwa hostel za Chuo cha Uandishi wa Habari, TSJ enzi hizo kiko Ilala Shariff Shamba, nikapata ugeni wa kutembelewa na mtoto wa Mwalimu, Madaraka Nyerere, kunijulisha ninahitajika Msasani nyumbani kwa Mwalimu Nyerere!, wale wa mastori mastori tuendelee, wale wa short and clear, unaweza ku jump into conclusion.

Kazi za Uandishi Kumcover Mwalimu
Mimi ndie mwandishi wa mwisho wa habari kusafiri na Mwalimu safari ya Uswisi kwenye mkutano wa South South Commission uliofanyika jiji la Bern nchini Uswisi. Hivyo mimi ndie mwandishi wa mwisho wa habari kufanya mahojiano na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere niliyoyafanyia jengo la The Bundes House, mjini Bern

Baada ya kurejea kutoka Uswisi, ndipo akaanza kuugua.

Mwalimu alipozidiwa na kupelekwa kutibiwa hospital ya St. Thomas, jijini London nchini Uingereza, ni mimi tena ndie mwandishi pekee wa Tanzania, aliyemtembelea St Thomas Hospital, nikiwa ndie mwandishi pekee wa Tanzania kutoka private media, aliyeandamana na Rais Mkapa ziarani Marekani kwenye Unga, wakati wa kurejea nchini tukapitia London kumuona Mwalimu na kurejea nyumbani ambapo mwanzoni mwa Octoba na haikupita wiki, Mwalimu akafariki.

Niliandaa a video documentary ya msiba wa Baba wa Taifa, tangu kuwasili kwa mwili, kuagwa uwanja wa taifa, nikamsindikiza mpaka Butiama kwenye makao yake ya milele.

Swali la kumhusu Mwalimu, je viongozi wetu wanamuenzi kwa kumuishi, au wana muenzi kwa mawazo tuu na maneno lakini sio kwa vitendo? Naombeni mnitajie hata kiongozi wetu mmoja tuu anayemuishi Nyerere kwa mawazo, maneno na matendo?

Jee chama alichokiasisi na kukiacha Mwalimu Nyerere, Chama cha Mapinduzi, CCM, kinamuenzi Mwalimu kwa vitendo?, kinamuishi kwa kufuata falsafa yake?, Jee hii CCM ya sasa ndie ile CCM aliyoiacha Mwalimu?.

CCM ya Mwalimu ilikuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi, sifa ya kugombea uongozi ilikuwa ni uwezo wa uongozi na uzalendo wako kwanza kwa nchi yako, kisha kwa chama chako, Jee sasa sifa ya kuchaguliwa kuwa kiongozi CCM bado ni zile zile au sasa ili kuchaguliwa kiongozi sifa kuu ni una mkono mrefu kiasi gani kuwapatia takrima wajumbe?.

Mwalimu aliichukia rushwa kwa dhati, baada ya kufariki, tukaibariki rushwa kwa kuipa jina zuri la “takrima” tukapitisha na sheria kuiruhusu!. Kelele zikapigwa, sheria ile ikafutwa, lakini sasa chama alichokiasisi Mwalimu zile takrima zimegeuzwa ni michango ya lazima ya kuombea fomu ya uongozi, sasa fomu ya kugombea ubunge CCM inauzwa kwa Shilingi milioni 1!, kuna wakulima wangapi na wafanyakazi wanayo hiyo milioni moja ya kujaza fomu ya Ubunge?. Mwalimu Angekuwepo haya yangefanyika?.

Hitimisho

CCM, serikali yetu, viongozi wetu na Watanzania kwa ujumla, tumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, sio tuu kwa mawazo, na maneno, bali kwa matendo na ikibidi kumuishi, tutabarikiwa, na Taifa litabarikiwa!, tukiendelea kumuenzi hivi kwa mawazo tuu na maneno, lakini matendo ni tofauti, taifa letu na chama chetu na viongozi wetu, tutaendelea kupata kichapo cha bakora za kitu kinachoitwa karma.

Wasalaam.

Paskali
 
Naunga mkono hoja

Mkapa aliona hilo akamwambia hayati jpm Kwamba

Tunataka kusikia Serikali ya CCM imefanya HIVI na vile sio mtu kafanya hivi na vile!

Tunajenga majina ya WATU KULIKO Taasisi matokeo yake wanaojengwa hujiona WAKUBWA KULIKO chama na kutengeneza mazingira ya kuimbwa na WATU KWA kutoa Takrima za uteuzi na fedha Ili wasifiwe WAO KULIKO chama na taasisi KWA UJUMLA!

Hata sasa linaimbwa jina KULIKO chama anachotoka mtu!katibu wa chama mwenezi anaimba jina KULIKO CHAMA na kukweza jina KULIKO CHAMA!!

RUSHWA au Takrima tumeitengeza KWA kukuza WATU KULIKO Taasisi! tutarajie sarakasi nyingi ZAIDI KULIKO!!!

Pole pia hata juzi wewe kukosa kale kaubunge ni matokeo yale yale!

Nakuambia live kabisa KWA wewe ulivyo na mchango wako wa uandishi wako Katika jamii sio wa kuwa hivi hivi tu ulipaswa upewe Ili uonyeshe KWA vitendo KWENYE field ya maendeleo na siasa KWA ujumla na sio KWA hukumu ya Moja KWA Moja eti wewe ni timu mamvi kama fimbo ya kukupigia kukosa nafasi!!

Mawazo huru!
 
Mayalla unaonekana kuwa na "connection" huko CCM lakini nashangaa kwanini bado hawakutambui, au ni lile swali lako kwa yule jamaa ndio lilitia doa lisilofutika? don't know!.

Anyway, suala la viongozi wetu wa sasa kushindwa kumuenzi Nyerere linachangiwa na mambo kadhaa, na sidhani kama itakuwa rahisi kuibadilisha hiyo hali, zaidi wataendelea tu kumuimba midomoni.

- Kupenda kwao anasa; kama matumizi yao ya misafara ya magari ya bei mbaya, huku wakiwa wamezungukwa na wananchi masikini, bila kuona aibu yoyote, hawa viongozi wetu wa sasa ni kama vile wanashindana kwa utajiri, na hawawezi kuichukia rushwa, au ufisadi, kwa sababu hivyo ndivyo huwafanya waendelee kuwa matajiri, mfano wa hili ni harusi ya Lowassa ulioutoa.

- Kukosekana sheria madhubuti za kuwabana, na viongozi jasiri wa kuzisimamia; ajabu siku hizi hata sheria zenyewe hazifuatwi, tena viongozi ndio wanaongoza kuvunja sheria, sasa kwenye mazingira haya, ukichanganya na kulindana, ni vigumu sana viongozi wetu kumuenzi Nyerere kwa vitendo.

Kwa mtazamo wangu, hawa viongozi wetu wanatakiwa kulazimishwa kumuenzi Nyerere kwa vitendo, na hilo litafanikiwa endapo tu itapatikana Katiba Mpya, hasa ile Rasimu ya Warioba. Naamini ile ndio itakuja kuwakumbusha kwamba, kuwa kiongozi wa serikali ni kuwatumikia wananchi, na wala sio kujilimbikizia mali wao binafsi.
 
Mwalimu alikuwa muumini wa serikali mbili kuelekea moja. Rasimu ya Warioba inataka serikali tatu. Tunamuenzije kwa kupitia rasimu ya Warioba?
 
Kuna doa FULANI wakati akiwa pale TBC,ndilo linalomtafuna!,aliwahi kuandika humu! Mamvi ameponza wengi Sana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…