Kumuita Diamond msanii wa kimataifa ni kichekesho

Kumuita Diamond msanii wa kimataifa ni kichekesho

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
2,255
Reaction score
1,565
Kwa sie wapenzi wa Ndomo,yawezekana itachukua muda mrefu sana kulisahau hili tamasha la fiesta 2014 maana limekuwa kama mkuki kuchoma kwenye kidonda,wakati mashabiki wake tukijua na kuamini Diamond yuko
kwenye PEACK ( au climax yenyewe ile) ghafla hatuamini wala kusadiki kile kinachotokea usiku wa jana pale leaders club.

Kwa mara ya kwanza Diamond aka sukari ya warembo anazomewa akiwa jukwaani,na kibaya zaidi anazomewa karibu na umati wote,..inahuzunisha sana,inatia hasira sara,inafedhehesha sanaa,INAUMIZA zaidi pale Ally Kiba anapomfunika Dimond kwa mbali sana,Ally Kiba kashangiliwa sana,..yaani mtu ambaye siku mbili zilizopita Dimond alitangaza kumsaidia kufanya collabo ili amuinue ndiye anamfunika..hii haita kaa kamwe itoke kichwani kwa Dimond na mashabiki wake.

Baada ya tukio hili,ambalo naweza sema ni baya sana kibiashara kwa Diamond hapa Tanzania,yamejitokeza makundi ambayo yanataka kumtetea Diamond au kugeuza hali halisi ya jana kuwa tofauti,baadhi yao wamekuja na hoja dhaifu kabisa kama vile
1/Mashabiki walitengenezwa kumzomea Dimond
2/Dimond anachukiwa na Watanzania
3/Dimond ni wakimataifa hata watanzania tukimchukia mataifa mengine yatamuabudu
4/clouds wametengeneza watu wazomee kumshusha Dimond
5/Watanzania hatujui vizuri ndio maana wamemshangilia Kiba
6....

Kiukweli ukiangalia hizo sababu hapo hata moja yenye mashiko haipo,hazina msing wala hazina ukweli,DIMOND SI WA KIMATAIFA kumlinganisha hata na Davido,acha hao wa kimataifa wenyewe,wala huwezi mlinganisha hata na Jay D, Dimond bado ana kazi kubwa ya kufanya kufikia kuitwa wa kimataifa,kwenda kuwaaimbia wabongo wanaoish marekani etc haitoshi kujiita wa KIMATAIFA.

Dimond,yawezekana umeanza kuchukiwa na Watu,sio kwa sababu yako,ila kuna timu yako unawalipa kwaajili ya PR wanashinda kwenye mitandao hao ndio wanaokuharibia,hawajui misingi ya PR..wanapost utumbo watu wakiponda wanarudi kuwajibu kwa kejeli na matusi hatimaye hasira zaja kwako,change hiyo timu ya PR,muangalie Jay Dee anafanyaje kwenye mamabo ya PR...

Kila la kheri Dimond..
 
Huyu wa kimataifa davido haja shangilia na yeye pamoja na kusema make noise for Diamond
 
Ndo umeamka saizi.
Kumeshakucha mda hapa.
Hayo uloandika tushayadili kwa kina.
 
  • Thanks
Reactions: ora
Ndo umeamka saizi.
Kumeshakucha mda hapa.
Hayo uloandika tushayadili kwa kina.

kama unaishi kwa shemeji yako (dada ako ndio kaolewa) huwezi kulala usiku,maana muda wote shemeji akikohoa unadhani anapita kwenda ku pee lazima ushituke usogeze mattress pembeni..na saa kumi na moja lazima uwe ushaamka maana shemeji anaamka kuangalia Tv sitting room unapolala
 
hahahaha,,Pole , i didnt mean to disturb.
 
Ally kibba aliwafunika diamond, davido na T.I na hata angekuwepo lady JD ungemfunika.ila hao waliokushangilia jana Leo hii wamekaa majumbani mwao wanasikiza nyimbo za davido,diamond na lady JD.wewe walishakupa kisogo jana
 
mi niko nasikiliza mwana dsm
 
kama unaishi kwa shemeji yako (dada ako ndio kaolewa) huwezi kulala usiku,maana muda wote shemeji akikohoa unadhani anapita kwenda ku pee lazima ushituke usogeze mattress pembeni..na saa kumi na moja lazima uwe ushaamka maana shemeji anaamka kuangalia Tv sitting room unapolala

Hahaha...Haaaaaaaaa nimecheka uwiii...this made my day watu mna hasira humu hatareeee
 
Kila kitu kina mda wake kwa nini diamond ndio time yke imekataa ivyo.
 
Ally kibba aliwafunika diamond, davido na T.I na hata angekuwepo lady JD ungemfunika.ila hao waliokushangilia jana Leo hii wamekaa majumbani mwao wanasikiza nyimbo za davido,diamond na lady JD.wewe walishakupa kisogo jana

Acha upimbi wewe
 
basi sawa diamond kashazomewa na kiba ameshangiliwa, then what?????? kwani tukiwasapoti wote itakuaje??? kwanini tunataka mmoja ashuke ndio mwingine apande? kwani itakuwaje wote wakawa juu??hicho kiti cha king sijui kipo kimoja tuu??
 
Back
Top Bottom