PreGE2025 Kumuombea kheri rais Samia ni uzalendo kwa nchi yetu- Kikwete

PreGE2025 Kumuombea kheri rais Samia ni uzalendo kwa nchi yetu- Kikwete

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
397
Reaction score
445
Wosia huu umetolewa na Mh. Ridhiwani Kikwete , Mbunge wa Chalinze na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu wakati akiwahotubia Wananchi waliojitokeza kuomba dua kuiombea Nchi na Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nyumbani kwake Msoga, Chalinze.

Akizungumza na umma wa Watanzania waliojitokeza kwenye dua hiyo, Mh. Kikwete amewashukuru kwa kujitokeza na kumuombea dua Mh. Rais. “ ukimuombea Rais Samia, umeiombea Tanzania, kutokana na umuhimu wa nafasi yake na yeye akiwa ndiyo mshika maono ya Nchi”.

Mh. Kikwete alitumia nafasi hiyo pia kuishukuru serikali ya awamu ya 6 kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka hii ya Rais Samia Suluhu Hassan ambapo Elimu,Afya, Miundombinu n.k na kutumia nafasi hiyo pia kuwaomba wanachalinze waendelee kumuamini na kumchagua tena kwa kura nyingi.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Wakizungumza baadhi ya masheikh waliohudhuria shughuli hii, wamepokea maombi ya Mbunge wao kwa furaha na hivyo watatekeleza kwa ari kubwa.

Dua na Futari ni utaratibu ambao Mbunge wa jimbo la Chalinze amekuwa anafanya kila mwaka kipindi hiki cha Mfungo.

FB_IMG_1742829901198.jpg
FB_IMG_1742829905639.jpg
FB_IMG_1742829903603.jpg
 

Attachments

  • FB_IMG_1742829907750.jpg
    FB_IMG_1742829907750.jpg
    87.4 KB · Views: 31
  • FB_IMG_1742829909831.jpg
    FB_IMG_1742829909831.jpg
    60.1 KB · Views: 35
  • FB_IMG_1742829912499.jpg
    FB_IMG_1742829912499.jpg
    86 KB · Views: 33
  • FB_IMG_1742829914916.jpg
    FB_IMG_1742829914916.jpg
    74.5 KB · Views: 37
  • FB_IMG_1742829917791.jpg
    FB_IMG_1742829917791.jpg
    88.8 KB · Views: 34
  • FB_IMG_1742829920102.jpg
    FB_IMG_1742829920102.jpg
    90.1 KB · Views: 33
  • FB_IMG_1742829922256.jpg
    FB_IMG_1742829922256.jpg
    61.5 KB · Views: 35
  • FB_IMG_1742829924650.jpg
    FB_IMG_1742829924650.jpg
    58.3 KB · Views: 28
Hana jipya huyo, ni muendelezo tu wa siasa za kusifu na kuabudu zilizoshamiri katika siasa za chama kijani
 
Wosia huu umetolewa na Mh. Ridhiwani Kikwete , Mbunge wa Chalinze na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu wakati akiwahotubia Wananchi waliojitokeza kuomba dua kuiombea Nchi na Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nyumbani kwake Msoga, Chalinze.

Akizungumza na umma wa Watanzania waliojitokeza kwenye dua hiyo, Mh. Kikwete amewashukuru kwa kujitokeza na kumuombea dua Mh. Rais. “ ukimuombea Rais Samia, umeiombea Tanzania, kutokana na umuhimu wa nafasi yake na yeye akiwa ndiyo mshika maono ya Nchi”. Mh. Kikwete alitumia nafasi hiyo pia kuishukuru serikali ya awamu ya 6 kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka hii ya Rais Samia Suluhu Hassan ambapo Elimu,Afya, Miundombinu n.k na kutumia nafasi hiyo pia kuwaomba wanachalinze waendelee kumuamini na kumchagua tena kwa kura nyingi.

Wakizungumza baadhi ya masheikh waliohudhuria shughuli hii, wamepokea maombi ya Mbunge wao kwa furaha na hivyo watatekeleza kwa ari kubwa.

Dua na Futari ni utaratibu ambao Mbunge wa jimbo la Chalinze amekuwa anafanya kila mwaka kipindi hiki cha Mfungo.
Kikwete familia nzima iko kwa samia serikali, sishangai Kikwete akisema hivyo!
 
Catholic watakapoanza nao kumuombea Tundu Lissu msije kusema dini inachanganywa na siasa
 
Hakuna uzalendo wowote kwa kumuombea rais.

Nchi haiendeshwi kwa maombi.

Kama mtu anapwaya arekebishwe ndio utakuwa uzalendo.

Utasemaje kumuombea mtu aliyeuza bandari na kuwaruhusu wezi kuiba kwa kusema wale kwa urefu wa kamba yao ndio uzalendo?
 
Catholic watakapoanza nao kumuombea Tundu Lissu msije kusema dini inachanganywa na siasa
Ridhiwani Kikwete ni sheikh we mpuuzi?!! Catholic hao watakaokaa na kumuombea lissu hawana kazi?!!! Anyway, catholic wa maana wote wapo ccm
 
Hakuna uzalendo wowote kwa kumuombea rais.

Nchi haiendeshwi kwa maombi.

Kama mtu anapwaya arekebishwe ndio utakuwa uzalendo.

Utasemaje kumuombea mtu aliyeuza bandari na kuwaruhusu wezi kuiba kwa kusema wale kwa urefu wa kamba yao ndio uzalendo?
Mamamamamamamae! Nasemaje, haters wa mama mwaka huu mtatokwa na hedhi kwenye madaladala.....mama amewashika pabaya mno!
 
Mamamamamamamae! Nasemaje, haters wa mama mwaka huu mtatokwa na hedhi kwenye madaladala.....mama amewashika pabaya mno!
Kwa akili hizi wala huwezi kuelewa nilichoandika..

Mama amemshika nani pabaya kwa kusema watu wale kwa kamba?

Wanaoumia ni walipakodi nyie machawa akili mmemuuzia huyo mama.
 
Back
Top Bottom