Kumuona Xi Jinping akizungumza tofauti na kuhutubia ni sawa na jogoo kutaga

Nataka kumuona Xi akiongea akiwa amejiachia kama binadamu wengine.
 
Huyo Wang Yi humu pacha wake yupo nafikiri kama wewe oya Wang Yi kuna siku ulipigwa maswali na reporter fulani hivi wa Canada ulijaa upepo

View: https://youtu.be/qikBsQ1h4S8?si=4S-u0j7bTaJ3bjEG
 
Hakuna mahali nimesema azungumze sana, sijawahi kumuona akijibu maswali ya waandishi wa habari, sijawahi kumuona kwenye mkutano wa majadiliano na watu wengine kama ambavyo viongozi wengi wakubwa huwa wanafanya.
 
Nataka kumuona Xi akiongea akiwa amejiachia kama binadamu wengine.
Kiongozi wa mwisho wa China aliyekuwa anweza kufanya hivyo maybe Deng Xiaoping mara kadhaa alifanya hivyo ila Xi nafikiri ni aina fulani hivi ya wazee wakoloni akiingia ndani watoto wote chumbani
 
Hakuna mahali nimesema azungumze sana, sijawahi kumuona akijibu maswali ya waandishi wa habari, sijawahi kumuona kwenye mkutano wa majadiliano na watu wengine kama ambavyo viongozi wengi wakubwa huwa wanafanya.
Ndio hivyo kuna sources kibao na News outlet zinazoonyesha policies na perspectives za China sio tu short term bali long term, vilevile na think tanks za kutosha (watu hawapo busy talking the talk bali walking the walk)

Hata wengine ingekuwa bora kama huo muda wa kupiga talalila wangetumika kufanya vya kufanya; na information zozote ziwepo sehemu mtu unajipakulia; Anyway kila mtu ana style zake (Reagan Msanii alikuwa the entertainer, Trump more talk without substance) so long as libeneke linakwenda that's all that matters..., ingawa kwa Trump libeneke analikwamisha kwa ukasuku wake....
 
Mrembo Peng Liyuan yuko poa anaendelea na majukumu yake rasmi kama kama public figure na first lady of China ndani ya mjengo Zhongnanhai​
Hakika mkuu nitakuja kutoa posa kwa binti yenu Xi Mingze msinifanyie hiyana tu.
 
Hapo ni kazi tu na matokeo chanya ndio kipaumbele. Longolongo na majungu ni ya Trump na himaya zinazo kufa.
 
Huyo zaidi ya kichina ana lugha nyingine anayojua kuzungumza ?...
ANAJUA LUGHA NYINGINE HILA HAPENDI KUTUMIA LUGHA YA WENGINE,HATA PUTTIN ANAWEZA ENGLISH NA GERMAN LAKINI HUWEZI KUMSIKIA ANAONGEA HZO LUGHA ZAIDI YA LUGHA YAKE.
 
Labda katiba hairuhusu, maana sijawahi kumuona hata akiongea chemba na Rais mwingine kwenye mikutano, kama wenzie

Yeye ni Hotuba tu aliyoandaliwa basi
Hata Malaysia alipoenda na pia hotuba ya mwaka mpya 2025 alisoma tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…