Kumwacha jela kifungo cha mwaka kutasaidia kutoa sumu ya ulevi wa pombe?

Kumwacha jela kifungo cha mwaka kutasaidia kutoa sumu ya ulevi wa pombe?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
UPDATE: Nimepewa wazo na Mshana Jr na Daudi Mchambuzi kumuacha Polisi au mahabusu muda mrefu, Bado naendelea kupokea maoni

Kuna ndugu yangu ni mlevi sana, Mara kwa mara nimelazimika kumtoa kituo cha polisi kwa kuwapa pesa za kubrashia viatu ma afande ambao tunajuana, Matatizo hayo yanatokea kwasababu ya ulevi wake wa pombe.

Kazi anafanya za ujenzi wa nyumba, kuchoma na kuuza matofali, kufyatua matofali , n.k n.k, Ni kijana mchapa mwenye mwili wenye misuli iliyojaa na mchapa kazi ila pombe inamharibu.

Sasa nimeona labda aende tu huko gerezani maana kosa lake ni la mwaka 1 na nuu hivi gerezani endapo nisipomtoa.

Kesi yake nimeshaifatilia huwa inasikilizwa haraka mahakamani na hukumu hutolewa papo hapo,

Sasa nimeona huenda akienda huko jela hio sumu ya uraibu itamtoka.

Je, nichukue huu uamuzi?
 
Ingawa mwaka mmoja ni mwingi lakini huoni baadaye itakuwa kama uhasama kwamba hujamsaidia? Ila ni funzo akitoka akili itamkaa sawa
 
Jela kila kitu kinapatikana mzee akiwa na sabuni za kutosha anafanya biashara ya kubadilishana tu hata ganja atanyonga ila kama hana kitu na anapenda pombe akikubali tu kuwa mke wa mtu hata ugali maharage atauskia kwa wenzake ye atakua anakula rosti tu na kazi ngumu hafanyi
Sasa kuwa makin asije kurudi akiwa bwabwa.
 
Huko unamuharibu zaidi.

Unamtengeneza azidi kuwa mlevi na katili sana. Mara Mia yake.

Msaidie hicho kifungo halafu ahame kwako akajitegemee zake mbali
 
Jela kila kitu kinapatikana mzee akikubali tu kuwa mke wa mtu hata ugali maharage atauskia kwa wenzake ye atakua anakula rosti tu
Sasa kuwa makin asije kurudi akiwa bwabwa.
Umejuaje mkuu?
 
Jela kila kitu kinapatikana mzee akikubali tu kuwa mke wa mtu hata ugali maharage atauskia kwa wenzake ye atakua anakula rosti tu
Sasa kuwa makin asije kurudi akiwa bwabwa.
Pole sana kwa yaliyo kukuta huko jela mkuu, Huenda ulizoea kazi za kalamu ila huko jela kazi za nguvu ulizishindwaikabidi usaidiwe .

Kwa upande wa huyu sio lele mama, Ni ngangali haswaa, kazi zake ni kuchoma matanul ya matofali, kufyatua matofali, Kulima n.k
 
Sio lele mama huyu, Ni ngangali haswaa, kipato chake anakipata kupitia kuchoma matanul ya matofali, kufyatua matofali, n.k sio a kuzunguka na viti
Hata angekua anafanya kazi za kuvunja vyuma ila kama ni mlevi na anapenda kitonga jela hata pombe atapata ila muda huo atakua mke wa mtu na wana wanamuita shemeji. Jela siyo kuzuri msaidie huyo jamaa yako.
 
Hata angekua anafanya kazi za kuvunja vyuma ila kama ni mlevi na anapenda kitonga jela hata pombe atapata ila muda huo atakua mke wa mtu na wana wanamuita shemeji
Jela siyo kuzuri msaidie huyo jamaa yako
Pole sana kwa yaliyo kukuta huko jela mkuu, Kuna watu mnatoa kirahis mno rinda, siku nyingine pambana mkuu,

Hata uende Dubai hawauzi marinda, yakitoka yametoka
 
Mwache akapumzike akirudi atakuwa kanyooka.. Mitaa ninayoishi kuna mmoja alikuwa hivyohivyo..kaswekwa mahabusu wiki tatu tuu karudi kanyooka kama rula nyumbani anaingia saa 12
Kuna lock up ya polisi na mahabusu, ilikuwa ni mahabusu mkuu ?? So aliachiwa au walitoa kitu kidogo
 
Dawa za kuacha pombe mbona zipo?;ni kitu nimehakikisha na ni shuhuda kwa macho yangu.
Huyu kashawekewa mara 2 dawa za kuacha pombe na dada yake lakini wapi? Pombe ni uraibu ambao hausikii dawa
 
Pole sana kwa yaliyo kukuta huko jela mkuu, Huenda ulizoea kazi za kalamu ila huko jela kazi za nguvu ulizishindwaikabidi usaidiwe .

Kwa upande wa huyu sio lele mama, Ni ngangali haswaa, kazi zake ni kuchoma matanul ya matofali, kufyatua matofali, Kulima n.k
Kwa profession aliyonayo huwa tunasema: "Atakula shushi". Maana siku hizi kuna miradi mingi ya kufyatua na kuchoma tofali. Kwa hiyo atapendwa sana. Atakuwa msimamizi wa miradi.
 
Back
Top Bottom