Kumwacha jela kifungo cha mwaka kutasaidia kutoa sumu ya ulevi wa pombe?

Kumwacha jela kifungo cha mwaka kutasaidia kutoa sumu ya ulevi wa pombe?

Mpeleke hospitali ya Mirembe

Gharama zao kwa mwezi ni 450000 - huduma za dawa na msaada wa kisaikolojia kutoka kwa watalaamu.

Mwisho wa siku atatoka huko akiwa na mawazo ya kujenga na si kunywa Pombe tena. Mlipie akae hata miezi 4 badala ya kukaa mwaka mzima gerezani akipigwa miti

Ukifanya hivyo utarudi hapa kutoa mrejesho.
Unahisi mtoa mada anaweza kumudu hizi gharama?
 
Huyo ni kumchanganyia madawa kwenye pombe tu atapike mpaka akili inayomtuma aende bar!
Sisi tulimlaza mjomba wetu makaburini baada ya kuzima na ulevi, alivyoamka asubuhi alitoka mbio bila kujua anakoelekea, toka siku hiyo aliacha pombe
 
Sisi tulimlaza mjomba wetu makaburini baada ya kuzima na ulevi, alivyoamka asubuhi alitoka mbio bila kujua anakoelekea, toka siku hiyo aliacha pombe
Hahahahaha mjomba aliona sasa kinachofuata ntajikuta nimezikwa kabisa
 
Sisi tulimlaza mjomba wetu makaburini baada ya kuzima na ulevi, alivyoamka asubuhi alitoka mbio bila kujua anakoelekea, toka siku hiyo aliacha pombe
Haha haha daah nimecheka sana mjomba wenu mlimkomesha kisawasawa
 
Anahitaji msaada wa kiroho na si vinginevyo.

I am sure ukifuatilia chimbuko, ni kama anakua amepokea kijiti kutoka kwa mtu fulani kwenye familia yenu.

Sasa, suluhisho sio kumtesa yeye bali anapaswa kusaidiwa kuondokana na kinachomtesa.

Nashauri apelekwe kwaajili ya maombezi ya deliverance ili aweze kuwa huru maana kinachomsibu, ni beyond uwezo wake wakuji- control.

Anahitaji maombi.
 
Dawa ni ndogo tu mVuNjie yAi kuna jamaa yangu kaacha Pombe kabisa.
Mwingine alivunjiwa yai asubuhi akasema sio inshu Wala nini maana Kama Ni bikra ya mknd wake inatolewa na mavih kila siku Maisha yake yote.
 
Mwache akapumzike akirudi atakuwa kanyooka.. Mitaa ninayoishi kuna mmoja alikuwa hivyohivyo..kaswekwa mahabusu wiki tatu tuu karudi kanyooka kama rula nyumbani anaingia saa 12
Huyo ni kijana wa Dar nini?

Kuna mmoja huyo wa mkoani bi mkubwa wake alikaza baada ya kuona anamsumbua sana. Akawekwa ndani kwa miezi 6. Ile kutoka hadi leo ile Familia wanaishi kama digi digi. Jamaa alipiga kiberiti nyumba yao yote. Hakuna kilicho weza kuokolewa hata kijiko maana aliisimamia hadi ikateketea akiwa na bonge la kwanja/fekeo ambalo alilinoa pande zote kama Sime.
 
Fanya PROB Analysis .. Nimekuwa afisa jela .. Kabla kuwa afisa ushirika .... Anachotaka kufanya jamaaaa kitamgharimu maisha yake yote .... Maafisa jela ni zaidi ya watu ... Amini ...
Simulia Mkuu mabaya ya huko ili watu wajue.
 
Ulevi ni roho ikishakuvaa kutoka huko bila deliverence ni ngumu sana unaweza ona kumpeleka je la utamsaidia lakini mark my words akirudi atakuwa na tabia zile Zile baada ya mda atarudi katika hali yake hiyo hiyo aliyoizoea hiyo kiu ya ulevi haiwezi muacha mpaka roho umuachie ya huo ulevi unaweza kuhadhibu mwili wake lakini bila hiyo roho kumuacha hawezi badilika kirahisi
 
Mkuu kuna kitu kinaitwa Sober house na Hospitali kuna kutengo cha Saikolojia. Kaonane nao kwanza na huyo ndugu yako kabla hujafikia uamuzi wa kwenda kumlaza MChongoma [emoji22]
 
Kwa profession aliyonayo huwa tunasema: "Atakula shushi". Maana siku hizi kuna miradi mingi ya kufyatua na kuchoma tofali. Kwa hiyo atapendwa sana. Atakuwa msimamizi wa miradi.
Na asishangae anakuwa waziri wa ujenzi
 
Siku zikiisha: "Hapana, hii ni fitna tu, nimekuja juzi tuu!! Hapana, hapana huu ni wivu!"
 
Jela siyo kuzuri, mpeleke popote ila siyo jela...
 
Back
Top Bottom