Kumwacha jela kifungo cha mwaka kutasaidia kutoa sumu ya ulevi wa pombe?

Ngome, Ndichi, kama unampenda ndugu yako na unaweza kumtoa usiruhusu akakkae jela sio kuzuri kabisa
 
Mkuu hakuna chenye utafanya wewe kimzuie huyo nduguyo kunywa pombe.

Siku zote mabadiliko ya aina yoyote huanzia ndani ya nafsi ya mtu mwenyewe. Bila yeye kuamua hakika nakuambia hataacha.

Unachoweza kumsaidia ni kumtafutia mtaalamu wa counseling ili azungumze nae. Wao wana mbinu nyingi za kuweza kuongea na mtu na kumshawishi aone maisha katika angle ya toauti.

Counsel ya mtaalam inaweza kuwa ndio chanzo cha inner drive ya yeye kujitafakari na kufikiri kuhusu kuacha pombe.

Kumwacha aende gerezani haitakuwa suluhu zaidi itakuwa ndio umeongeza tatizo. Gerezani sio sehemu nzuri.
 
[emoji134][emoji134][emoji134][emoji134],Jela hakufai.
 
Utakuta pombe anazotumia ikizidi sana bei yake 2000 ambiance’s,shumwaa na balimi.

Mwambie hatumie Jack daniel !

Sijawahi kuona walevi wa pombe kuanzia 70 wanamambo ya kijinga
 
Kuna kijana alipokea mshahara akanywea wote pombe. Asubuhi alipoamka akasema sinywi tena pombe, ilikuwa 2018 hadi leo hajagusa pombe.

Uamuzi wa kuacha pombe, punyeto, bangi, umalaya n.k inabidi utoke ndani ya mtu mwenyewe.
 
Pia utofautishe mlevi na muhalifu. Ndugu yako ni muhalifu ndio maana kila siku anakamatwa.
 
Mwache akapumzike akirudi atakuwa kanyooka.. Mitaa ninayoishi kuna mmoja alikuwa hivyohivyo..kaswekwa mahabusu wiki tatu tuu karudi kanyooka kama rula nyumbani anaingia saa 12
Kuingia nyumbani saa 12 nalo ni tatizo kubwa zaidi
 
Jela za kitanzania ndugu hapana, najua inachosha sana kubeba matatizo yake lkn nakuomba usimwache aende jela.
 
Huyo ni kumchanganyia madawa kwenye pombe tu atapike mpaka akili inayomtuma aende bar!
 
Pombe kama ni mlevi haswa , hata akae miaka mingapi akitoka ataendelea. Labda awe willing kuacha.

Nina ushuhuda na ndugu yangu mmoja yeye alikaa miezi sita akarudi akaendeleza vyombo kama kawaida
 
Usimwache apelekwe huko mambo yatazidi kuwa mabaya zaidi
 
Talking from experience!.

Nina mdogo wangu 34 years. Nimehangaika naye sana. Ni chapombe kupitiliza.

Alikuwa mfanyakazi mzuri sana, pombe zikamlemea. Akaachishwa kazi. Akaanza kufanya biashara, jioni ikifika hela ya mauzo anaenda kunywea.

Ana mke na watoto wawili, hela anazo biashara inafanyika lakini mahitaji hawapati.

Mbaya zaidi, akilewa wala halegei. Anakuwa na nguvu balaa.

Nimehangaika naye sana. Kuna dawa nilipewa, akaacha kabisa kunywa kwa wiki tatu. Akarudia tena kwa nguvu zaidi.

Nimeamua kumpeleka Gereza la Karanga kwa miezi mitatu. Ndo kwanza ana mwezi, ila ninaumia sana yeye kuwepo huko.

Ngoja tuone akitoka hali itakuaje. Nitaleta mrejesho..
 
Huyu kashawekewa mara 2 dawa za kuacha pombe na dada yake lakini wapi? Pombe ni uraibu ambao hausikii dawa
Mjomba wangu ana hiyo dawa. Kwa ndugu huwa anawapa bure. Hakuna aliyenyweshwa hiyo dawa akaendelea kunywa pombe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…