Kumweleza Ukweli, Mtu Anayedanganywa ni Kumsaidia!, Asante Balozi Dr. Nchimbi Kuwaambia Ukweli CHADEMA

Eti wahariri au genge la UVCCM
 
Huyu sio yule Paskali ninaemjua, Kwa haya mnayoyafanya Nyie na vizazi vyenu mtalipia hii haki mnayodhulumu watanzania.
 
Hakuna mhariri wenye akili timamu angepelekwa Songea kwenda kumsifia Nchimbi, Songea nadhani ni sehemu ambayo elimu iliingia mapema lakini ndiyo sehemu masikini Tanzania sababu ya kukumbatia ujinga na kutukuza koo chache, kimsingi lilikuwa ni kusanyiko la wala rushwa na wasaka fursa wala hapakuwa na mhariri hata mmoja. Ameni
 
Tatizo lako Pascal Mayalla ukisikia harufu ya fedha za serikali unalainika kama mkate mgumu mbele ya chai.
 
Yeye mwenyewe anajua bila Chadema kushiriki uchaguzi, huo uchaguzi utakuwa batili, hapo anajifariji tu, anaona kama Chadema inamcheleweshea yeye kupata umakamu ambacho ndo kitu kilichotawala akili yake, no Reform no Election inamtafuna Kwa ndani na inawezekana hata usingizi haupati vizuri
 
Endelea tu kuwadanganya. Hata kama hawatafanikiwa mwaka huu haina maana kuwa tatizo litakwisha. Wanachokifanya CCM ni kuahirisha tu na kuyaongezea madai nguvu zaidi huko mbeleni.
Period....

Ndio science na fact yenyewe, walishaona watanzania ni wapole na wajinga tangu miaka ya ukoloni bado wanaamini ni walewale tu, wanasahau kwamba kizazi cha uhuru na kizazi cha Nyerere ndio kinaishia hivyo, wadanganywa wanaendelea kupungua deile, watakuja kushtuka washachelewa
 
Inasemwa kua wewe ndie DALALI wa TEF na balile ndie CONNECTION

""" How can you eradicate this embargo"""
 
JUA NI KALI SANAAAA KWA MACCM😆
 
Mungu ni Mkuu kuliko hila za mwanadamu.
Ndugu yangu Pascal, usisahau kuwa mamlaka yote duniani hutoka kwa Mungu. Hakuna cheo, heshima, wala nafasi yoyote ya uongozi inayopatikana bila mapenzi ya Mungu kuruhusu, lakini pia hakuna udhalimu wowote unaoweza kustahimili mbele ya uso wa haki ya Mungu milele.

Ni vizuri kusherehekea demokrasia na uchaguzi, lakini pale ambapo uongo, upendeleo, au tamaa ya madaraka vinatawala mioyo ya watu, basi hapo ndipo tunapomchukiza Muumba wetu. Kwa kila neno la hadaa linalotamkwa hadharani, kwa kila msimamo unaochochea kukata tamaa kwa wapinzani au kupuuzia sauti ya walio wengi, kuna laana ya Mungu inayotembea kimya kimya juu ya wale wanaojifanya miungu wa dunia hii.

Ukuu wa Mungu hauwezi kushindaniwa na siasa za dunia. Na yeyote anayeacha kweli na kutafuta uongo ili kuendeleza maslahi yake binafsi, huyo amejihukumu mwenyewe. Heri afundishwe sasa kwa upole kuliko ahukumiwe mbele ya kiti cha hukumu cha haki isiyo na upendeleo.

Tamaa ya madaraka haijawahi kumletea mtu baraka ya kweli. Kuna njia moja tu ya kuliongoza taifa kwa haki — njia ya uadilifu, ukweli, na kutokupendelea upande wowote.

Tafadhali usiitumie kalamu yako kueneza woga au kukatisha tamaa waliokataliwa, bali itumie kama chombo cha kuhubiri haki, amani na maridhiano. Kalamu ya mwandishi ni upanga mkali — na Mungu atakuuliza uliandika nini na kwa maslahi ya nani?

Ukiona ukweli na ukaamua kuuficha kwa sababu una maslahi ya muda, Mungu atakuvua nguo mbele ya mataifa. Maandiko yanasema, "Ole wao waandikaji wa uovu, waufanyao uovu kwa kalamu zao" (Isaya 10:1).

Ndugu yangu Pascal, tubu. Badilika. Tumikia nchi na watu kwa uaminifu, si kwa tumbo lako wala kwa hofu ya wale walio juu yako. Kwa sababu hata wao pia ni wa muda tu. Ukuu wote ni wa Mungu.

Mungu Ibariki Tanzania — kwa haki, kwa upendo, na kwa viongozi waaminifu.
 
Miaka mitano ya awamu ya Sita imeisha lini ?
Awamu ya sita mpaka sasa ina miaka mitatu ?
Sasa kwa nini awamu ya sita Rais akae madarakani miaka Nane badala ya kumi ?
Kwa nini muhula wa kwanza wa awamu ya sita uwe ni miaka mitatu badala ya mitanoa?

Kwa nini mnasema mitano tena ?
Hiyo mitano ya kwanza imeisha lini ?
Yeyote ni kwa sababu ya katiba inayotumika matumbo ya watu wachache badala ya umma wa watanzania .

Uchaguzi unawezekana kusogezwa mbele kwa sababu bunge awamu ya sita alilolizindua Rais Samia katoka awamu yake ya maendeleo ya miaka mitano bado halijafikisha miaka mitano mpaka sasa ?

Kama vile wananchi walivyolazi ishiwa kuwa nchimbi atagombea umakamu basi nao watalazimisha uchaguzi uahirishwe mpaka yafanyike mabadiliko ya kisheria yenye tume isiyoegemea upande mmoja
 
🚮🚮🚮
 


Mayala, uchawa wa uzeeni kiasi hiki, unakufanya uwe mzee useless.

Uutumie uzee wako kwa hekima kuliko ufanyavyo, hakuna kikubwa cha pekee utakachofaidika nacho kupitia uchawa, kwenye umri huu. Tengeneza jina litakaolishi, uchawa na kuikimbia haki, uchawaunaua jina.
 
No reform no election mzee paschal. Subiri utaona kinachofanyika. Lissu alisema uchaguzi utavurugika. Na jana kalegeza kauli kua ataitisha maandamano ili kujilinda na kauli ya mwanzo. Ila najua lissu ni genius, atakachofanya tusubiri
Kwanza Mkuu Kilambi, kilambimkwidu , kwa ruhusa yako, naomba kuitumia hii
post yako kama mbegu ya kuoteshea bandiko langu fulani.

Pili, nakubaliana na wewe Lissu ni genius fulani,ila ni genius wa sheria na pia ni bingwa wa kuongea ana very high convincing power ya power of speech ambayo mpinzani wake hana!,tena Lissu anauwezo fulani mkubwa sana wa kitu fulani ambao naomba nisiutaje hapa,ambapo akiutumia uwezo huo,anaingia ikulu ndani ya dakika sifuri!Uwezo huo ndio uliopelekea mimi nikamshauri Lissu

Lissu anaweza kabisa kuwa ndie chaguo la Mungu kwa Tanzania 2025,na Mungu alimuandaa siku nyingi,hata ile siku anashambuliwa,zilifyatuliwa risasi full magazines mbili,kwa kumiminwa mfululuzizo,gari la Lissu lina matundu 37 ya risasi,risasi 16 zikampata!,ni Mungu alizuia kwa kuzikwepesha kwenye vital organs,na mpaka sasa kuna risasi moja Mungu ameisimamishia 2mm from a vital organ,its too risk to remove it,wameamua kuiacha, hivyo Lissu pale alipo anatembea na risasi mwilini mwake!。

Kwa vile lengo la shambulizi lile lilikuwa ni kumtoa Lissu duniani kwa kumuua na kumtoa roho,ni Mungu ndie aliyemgia kifua kwa kutuma malaika wake kuzielekeza kila risasi zipite wapi,ila Lissu na watu wengine wengi wanadhani amepona kwa bahati nasibu tuu ya kudra tuu ya Mwenyeenzi Mungu,hawajui kuwa Lissu ameokolewa ili atimize kusudi fulani la Mungu。

Baada ya kushambuliwa Lissu aliogopa kurejea nyumbani Tanzania,kwa kuhofia wale wabaya wake watamalizia kazi yaokutimiza lengo lao la kumtoa roho,hivyo akamwandikia IGP barua ya kumhakikishia usalama wake ndipo arejee,IGP hakuijibu ile barua kwasababu jeshi letu polisi haliwajui hao wasiojulikana hivyo hawawezi kumhakikishia usalama wake,wakajikausha kimya,ni mimi tena ndie niliyemhakikishia Lissu usalama wake kupitia andiko hili
ndipo Lissu akakubali kurejea kuja kutimiza ule ushauri wangu wangu wa

Hivyo Lissu ni chaguo la Mungu kwa kusudi fulani,na kusudi hilo kwa maoni yangu ni kwa Lissu kugombea urais 2025 na kuingia ikulu straight siku ya uchaguzi by saa 4 tuu asubuhi,Lissu anakuwa amemaliza kazi!。

Lakini sasa shetani ameingilia kati mpango huu,kwa kumzuia Lissu asigombee,kutimiza mapenzi Mungu,hii NRNE ni li pepo Lissu ametupiwa na shetani,kuzuia uchaguzi ni mpango wa shetani ili Lissu asigombee urais 2025,ili kumzuia asiingie ikulu na mapenzi ya Bwana yasitimie!。

Kwa sisi wenye jicho la tatu,tunamuona jinsi Lissu alivyo na
Bonge la fursa kubwa 3 adimu na adhimu, kwa uchaguzi wa 2025, Lissua anazo kete fulani tatu
nikizitaja hapa watu wapiga kelele tutatafutana humu!.

A Way Forward
Watu wenye jicho la tatu wanao
haya mimi ninayo yaona kuhusu
fursa za 2025 kwa Lissu, tumsaidie
Lissu aombewe, pepo la No Election, lililomkumba limtoke, Chadema waingie dimbani kwenye uchaguzi Lissu with a Full
Force by The Big Bang!, isimamishe wagombea ubunge majimbo yote, na kata zote, wala hawahitaji kupiga kampeni yoyote, YEYE Pekee ndie atasimamia hili na siku ya uchaguzi, ni YEYE atasimamia kura za Lissu, na amini usiamini, kwa uweza wake YEYE, Antipasi Tundu Mugweri Lissu anatinga Ikulu, kwa muujiza, na anaye muingiza Lissu, sio Chadema, sio Watanzania bali ni yule yule YEYE, aliyemponya na shambulio lile, akapita chini ya bonde la uvuli wa mauti, na kubaki salama, akamsimamia matibabu, akasimama tena, ayaache mapenzi ya Bwana yatimie juu yake, watu washuhudie jinsi LILE JIWE LILILOKATALIWA NA WAASHI LITAFANYWA KUWA JIWE KUU LA PEMBENI!.

Mungu Mbariki Tundu Lissu, hilo pepo mchafu wa No Election limtoke!

Mungu ibariki Chadema ishiriki uchaguzi kwa kuweka wagombea majimbo yote, kata zote!

Mungu Ibariki Tanzania!.

Paskali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…