Kuna baadhi ya graduates wanaomba connection ukiwapa wanakuangusha

Kuna baadhi ya graduates wanaomba connection ukiwapa wanakuangusha

Iko hivi
Kuna mdogo wa ex wangu kamaliza chuo mahali huu ni mwaka wa 3 au 4 kana sikosei.

Basi juzi kati hapo nikakutana na huyu ex wangu akaniambia kama ofisini kwetu au namjua mtu yeyote nimsaidie mdogo wake apate kazi.
Basi bana kuna mdau flani hivi namjua ni hr kwa kampuni hizi za wachina nikampandia akaniambia dogo atume cv,bahati nzuri siku hiyo hiyo wakamfanyia online interview dogo akawa kapata ile nafasi.

Akaambiwa aje Dar kwa ajili ya kusaini mkataba na training ya kama mwezi hivi..dogo kafika dar akaambiwa mshahara ni laki 5, kituo cha kazi kitakua songea ila watamsafirisha wao,watampa allowance ya siku 10 kila siku 55k na pia watamlipia kodi ya nyumba mwaka mzima,akaambiwa nyumba atakayopanga isizidi elfu 80 kwa mwezi.

Cha kushangaza dogo baada ya kuambiwa hivyo kumbe hakuridhika na ule mkataba,wakamuambia ajitafakari mpaka asubuhi ya leo awe amewapa majibu ili mchakato uendelee, so mimi asubuhi hii nimempigia kujua alichoamua cha ajabu ananiambia eti yuko njiani kurudi mkoani kwao kwani mkataba ule hajaupenda akasema yeye alitegemea kituo cha kazi kingekua huko huko mkoani kwao Dodoma coz kuna mambo yake mengine bado anayaweka sawa huko dodoma hivyo kwa sasa hayuko tayari kuishi nje ya mkoa wao.

Aisee nimeshikwa na hasira sio poa,nimempigia dada ake nimemwambia live next time asije akaniambia ujinga wa huyu mdogo wake kwa hiki alichokifanya.

Mkipewa connection zitumieni vizuri wakuu otherwise mnatukatisha tamaa.
Duh nipe Mimi hiyo connection nisawazishe makosa
 
Watu wanakosa uungwana kabisa, kuna wakati fulani jamaa yangu alikuwa anataka kumsafirisha demu wake aende Dsm kutoka nyanda za juu kusini.

Basi jamaa akaniomba nimfanyie mchakato shemu apate usafiri, nikamcheki mpiga debe mmoja pale stendi nafahamiana naye, nikampa story nzima akasema poa nimpe namba huyo shemu amcheki yeye(mpiga debe).

Nikamvutia waya shemu, hakupokea
Nikatext hakujibu ikabidi nimrudie bro, nikamchana mbona shemu hapokei wala hajibu sms ,akasema labda yuko busy ngoka nimcheki.

Akamcheki, akanirudia hewani kuwa shemu wako bado hajasepa, nikampigia tena shemu hakupokea ila jamaa akimpigia wanaongea freshi.

Huku nako yule mpiga debe akaanza kunisumbua kuwa gari imepatikana mbona huyo mtu hamtafuti, nikamjibu nishampa namba yako atakucheki, hakumcheki mpiga debe ,jamaa sasa akawa ananisumbua mimi, nikampotezea.

Tangu siku hiyo, hatujawahi tena kuongea na yule shemu hadi leo tunachekiana tu statuses
 
Ofa yao ilikuwa na hicho kipengele, nilitaka kumtumia msg yule mzungu maana nilikuwa na email yake na pia yeye ndiye alinifuataga linkedin, so alikuwa kati ya watu ambao nimeconnect nao. Ila baadaye nikaamua niache tu.
Ila walipata watu walikuwa wanataka watu 15 wakawa wanawalipa 720k kwa mkataba wa miaka miwili japo baadaye baada ya miaka miwili waliwaongeza maslahi at least now si mabaya.
Kwahiyo hapa ndo ule usemi ukitaka kula lazima uliwe kwanza, shida mbaya sana.
 
Madogo wanataka wakianza tu waanze na mshahara wa million 5.
 
Back
Top Bottom