Kuna baadhi ya graduates wanaomba connection ukiwapa wanakuangusha

Duh nipe Mimi hiyo connection nisawazishe makosa
 
Watu wanakosa uungwana kabisa, kuna wakati fulani jamaa yangu alikuwa anataka kumsafirisha demu wake aende Dsm kutoka nyanda za juu kusini.

Basi jamaa akaniomba nimfanyie mchakato shemu apate usafiri, nikamcheki mpiga debe mmoja pale stendi nafahamiana naye, nikampa story nzima akasema poa nimpe namba huyo shemu amcheki yeye(mpiga debe).

Nikamvutia waya shemu, hakupokea
Nikatext hakujibu ikabidi nimrudie bro, nikamchana mbona shemu hapokei wala hajibu sms ,akasema labda yuko busy ngoka nimcheki.

Akamcheki, akanirudia hewani kuwa shemu wako bado hajasepa, nikampigia tena shemu hakupokea ila jamaa akimpigia wanaongea freshi.

Huku nako yule mpiga debe akaanza kunisumbua kuwa gari imepatikana mbona huyo mtu hamtafuti, nikamjibu nishampa namba yako atakucheki, hakumcheki mpiga debe ,jamaa sasa akawa ananisumbua mimi, nikampotezea.

Tangu siku hiyo, hatujawahi tena kuongea na yule shemu hadi leo tunachekiana tu statuses
 
Kwahiyo hapa ndo ule usemi ukitaka kula lazima uliwe kwanza, shida mbaya sana.
 
Madogo wanataka wakianza tu waanze na mshahara wa million 5.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…